Mada maalum kwa wanandoa

Mada maalum kwa wanandoa

Hivi hujuagi kuwa ubaya ndo huwa unavuma kuliko wema? Wapo wenye ndoa njema kibao tu, sema wengi wao hawanaga muda hata wa kuandika. Na hata wakiandika kusifia ndoa zao, tunakuwa wa kwanza kuwaongelea mbovu, sijui ndoa yenu ina miaka mingapi blah blah blah. In short binadamu hatupendi habari nzuri
Hapa pia pana ukweli.....
IMG_20190125_124158.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa

Mkuu kama mimi huyu wangu naweza kutaka kuzungumza naye ili tujadili maisha yetu kiujumla ananijibu, "KWA SASA SINA MUDA NINA SHUGHURI ZANGU/NIMECHOKA/NALALA/KESHO NAFANYA USAFI" yaani kwa sasa naamua hata kufanya swala la maendeleo kwa ajili ya maisha yetu ya baadae mwenyewe au namshirikisha Dada yangu

Sijaona faida ya kuwa katika ndoa zaidi ya kuepuka dhambi ya kuzini

Ndoa ndo kwanza ina MIEZI MIWILI

Nafikiria kutoa Talaka nirudie maisha yangu ya usela

Ninachokiona hapa umeshakuwa too negative na mkeo pamoja na ndoa yako kutokana na sumu mbalimbali na baadhi ya matendo yake!

Nakushauri, ndoa bado changa sana. Hebu kaeni muyajenge kwa kuongea na kuonyana na kupeana miiko. Inaonekana yeye anaona kafika tayari mipango yote ni mume kuendana na maisha aliyoishi pengine kumbe mngekaa na kuongea serious anaweza kubadilika na kuwa mke bora kabisa kwako
 
Nilishawahi mara nyingi tu, sema mkifika huko baada ya nusu saa anaanza kuboa na raha yote inakuwa karaha, utasikia ohoo mbona kama tunapoteza tu hela, siturudi tu nyumbani, mara mbona pesa ya kulipa hela ya bima ya gari unasema huna mpaka tunatembea nalo usiku tu kama wanga alafu hapa tunazipoteza tu bure, mtu gani huna mipangilio ya expenditure zako ! Dah yani kero zinakuwa nyingi mpaka naamuua kwa hasira turudi tu home kwani hapo nakuwa nshakwazika sana.

Mbona anakushauri vitu vya msingi kabisa hapa, sema umemchukia huyo mwanamke sababu labda wewe ni si mtu wa malengo na yeye ana malengo!

Inawezekana approach yake pia si nzuri labda sababu ya kabila au malezi! Mfano unataka uoe Mkurya au Mchaga then utegemee lugha laini kama ya Mbondei ni ndoto!!

Huyo ni maendeleo oriented, msikilize mtatoboza hata kama ni mie unaspend 50,000 wakati gari hujalipia bima nakuchapa makofi kabisa!!

Akili gani hizo halafu unaambiwa unasema anakuboa, unataka mke gani tena?
 
Ndyo lakini kujipa furaha ni lazima ndoa ni furaha si mateso mmoja wenu anapofanya jambo la kuwaleta pamoja kma wanandoa mfurahi pamoja huwezi sema anapoteza pesa vp kma angetoka nalo usiku bila ww kuwepo na akatumia iyo pesa bila ww kuwepo na gari likapakiwa apo ndani mda mwingine nyie wanawake mnakuwa kero na wachungu kama pili pili

Sent using Jamii Forums mobile app

Akili matope, hivi akili gani hizi?

Yaan umepata mke anakushauri maendeleo na vitu vya msingi unalalamika?

Mwanamke anakushauri kupunguza matumizi mabaya ya pesa ufanye vya maana unakasirika unaona hafai?

Hivi ungepata mke komba akifika hapo anagida pombe mpaka senti ya mwisho ndiyo ungefurahi??

Anakushauri punguza matumizi ulipie bima uwe free kudrive muda wote unakasirika? Hivi hata huo usiku ukipata ajali itakuwaje? Bado hujaona alichokiona mke hapo??

Grow up guys, siongeagi vibaya lakini hapa utanisamehe!! Kwa statement hiyo uliyotoa hapo bado huna akili ya kuoa!!
 
Hahahahaaaa! Kuoa bila mipango au kulenga ishu moja tuu matokeo yake ndiyo hayo!!

Kabla ya kuoa ulipaswa kujua au kujifunza utaishi vipi na mkeo na hata baadae wanao! Yanayobaki muachie Mungu

Mie nina zaidi ya miaka 10 kwenye ndoa, mwanzoni nilipata ugumu flani coz kuna mmoja wetu kabadili dini so kufundishana na kuwekana sawa ilikuwa shida kidogo! Pia nilikiwa mnywaji, kurudi usiku hakuna muda na familia napo vilichangia kuweka gap kwenye ndoa yangu na wakati huo kipato kilikuwa chini, so tukawa na matamanio yasiyotimia matokeo yake ni stress na kugombana!

Kabla ya kuoa nilipanga kuwa na familia yenye furaha, outings na vacations na safari ni vitu napenda sana kiukweli!! Nilihitaji mtu wa kufanana nae!

Nilipoanza kazi na NGO moja hivii inadeal na maswala ya ndoa! Nilikuja kugundua visababishi vya vikubwa vya migogoro ya ndoa ni nini! Kimoja wapo ni kitendo cha kila siku kurudi nyumbani usiku wa manane, umelewa wanawake wanaumia sana ila basi tu! Yakimzidi ndipo nae hutafuta faraja kwa namna ingine au hubadilika tabia na ndipo hapo, migogoro inaanzia!

Niliamua kubadilika, pombe nikaacha na familia yangu ikawa ndiye rafiki zangu wakubwa!!

Naishi kwa amani na nafurahia maisha ya ndoa to maximum!! Sijutii kwa hakika na naamini hata mke wangu vile vile!!

Tunatoka outing wote, tunasafiri tunavyopenda tunafanya yanayotupasa yaan ni full furaha! Namshukuru Mungu kwa kweli.

Ndoa ya furaha inawezekana ila kwa jitihada za pande zote mbili!! Ukiona unaleta furaha ila upende mwingine hauhitaji uwe hivyo hilo ni tatizo na hapo inabidi kuchukia hatua!

Kikubwa tumia muda mwingi kuchunguza utayetaka kuoa au kuolewa nae. Kama ana tabia usiyoipenda jikatae mapemaaaa! Usitarajie atabadilika akishaingia kwenye ndoa, na hili ndiyo kosa la wengi!!


Hongera sana sana mkuu...!nataman wanaume wote wajitmbue wenyew kwa comment km hii...
 
Mbona anakushauri vitu vya msingi kabisa hapa, sema umemchukia huyo mwanamke sababu labda wewe ni si mtu wa malengo na yeye ana malengo!

Inawezekana approach yake pia si nzuri labda sababu ya kabila au malezi! Mfano unataka uoe Mkurya au Mchaga then utegemee lugha laini kama ya Mbondei ni ndoto!!

Huyo ni maendeleo oriented, msikilize mtatoboza hata kama ni mie unaspend 50,000 wakati gari hujalipia bima nakuchapa makofi kabisa!!

Akili gani hizo halafu unaambiwa unasema anakuboa, unataka mke gani tena?

Mkuu nakuelewa vizuri sana, ishu ni approach ila pia siyo kwa kuwa kuna majukumu muhimi hujatimiza basi usijipe mda wa kupumzika na kula starehe hata kidogo, hii inakera sana sometimes


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni siku nyingine tena imepita, tumerudi salama majumbani mwetu, kuungana tena na wapendwa wetu, familia na watoto pia... Baadhi yetu hatujarejea, tuko mishe na viti virefu... Baadhi tuna sababu za msingi na nyumbani wanafahamu na tumewapa taarifa, wanatusubiri watupokee kwa upendo, kwa furaha kwa bashasha kuu

Baadhi hali ni tofauti, hatungependa kuchelewa nyumbani.... Tungependa tuwahi, tuungane na familia, tuimalize jioni kwa furaha kuu kabla hatujaungana kwa dinner na maombi ya usiku.... Lakini hali ni tofauti tunapoteza muda nje saa zisogee ili tukifika tu ni chakula kuoga na kulala... Tunakimbia kero na malumbano yasiyoisha
Ndoa haina furaha.... Ndoa haina amani, majuto ni mengi mno moyoni.. Kila mmoja anajutia kivyake... Hakuna upendo tena... Hakuna kuaminiana tena... Ni mwendo wa kutuhumiana na kuviziana.... [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]baba ana chumba chake.. Mama naye ana chake... Ama la chumba ni kimoja lakini kila mmoja ana kitanda chake...
Hakuna upendo, hakuna sharing, hakuna majadiliano ya changamoto, ya maumivu ya kushinda na kushindwa, ya kutiana moyo na kufarijiana... Kila mtu kivyake... Kila mtu na lwake... [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji24][emoji17][emoji17][emoji17]

Karibuni wanandoa wote.. Ni mada ya kupeana faraja na kushare maumivu... Itambueni nguvu ya kuongea... Kuongea hupunguza maumivu mengi... Kupitia mada hii utajiona hauko pekeyako na pengine utaona kuwa kumbe wewe una nafuu kubwa ukisikia ya mwenzako. Jisikie huru ufunguke....
Funguka kwenye ndoa yako iliyoumizwa na kujeruhiwa sana, iliyotiwa vidonda na makovu ya kila aina
Ya usaliti
Ya kuchapiwa
Ya kusingiziwa
Ya kunenewa mabaya
Ya kudharauliwa kutukanwa na kudhalilishwa
Funguka upate nafuu
Funguka upate faraja
Funguka upunguze sumu mwilini
Funguka upate kupona sasa....
Karibuni wanandoa wote

Jr[emoji769]
Mshana Jr, katika ulimwengu wa sasa wa TEHAMA, ni zaidi ya hayo katika ndoa maana mawasiliano yamekuwa ni vidole kwenye simu ya kiganjani wakati wote.

Hali ni mbaya sana maana watu wanajifaraji kwa kupapasa simu.

"Video Clip" hapa chini inatoa changamoto za hizi simu katika mahusiano hata na Mwenyezi Mungu.
View attachment VID-20190124-WA0002.mp4
 

Attachments

Mshana Jr, katika ulimwengu wa sasa wa TEHAMA, ni zaidi ya hayo katika ndoa maana mawasiliano yamekuwa ni vidole kwenye simu ya kiganjani wakati wote.

Hali ni mbaya sana maana watu wanajifaraji kwa kupapasa simu.

"Video Clip" hapa chini inatoa changamoto za hizi simu katika mahusiano hata na Mwenyezi Mungu.
View attachment 1005105
[emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Hii ni kwa wanaume njia pekee ya ndoa kubaki salama ni mfumo dume tu si wa kumkandamiza mwanamke ila wakuonyesha

Simba wafamilia uko ukiiunguruma lazma faraja iwepo na huzuni iwepo kma kuna ujinga umetndeka
.
Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi kwa asilimia 99.9999999999999999999999999999999999999999999999999999% Bila shaka mwanamke anahitaji redirection kila wakati. Isifike mahali akawa ndio kichwa cha familia. Familia na ndoa kwa ujumla Itayumba kama mianzi kwenye upepo mkali. Big up kamanda shikilia uskani vyema barabara yetu inahitaji dereva asiyeyumbishwa na abiria
 
😛😛😛😛😛 hahahaha Jr acha basi haahhaha nimejikuta nacheka ujue
Si jambo baya wawili wanapojenga nia ya kuwa mwili mmoja[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom