Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali


Nafikiri tatizo laweza kuwa engine mount. ..waangalie ka ziko poa ...hope wataalamu zaidi watapita
 
Msaada
Kwa wenye uzoefu makadirio ya kodi ya magari kwa TRA ukiingiza specification zote ndo gharama halisi ukipeleka documentation ukiagiza gari Japan?
Kati ya autorect na Befoward ni company gani wana quality cars?
Mwisho ukiagiza gari una save kiasi kizuri cha fedha ikilinganisha na kuchukua showroom bongo?
Asanteni kwa michango yenu!
 
Kwanzaa the best company for used car ni Ile wanayokuonyesha inspection sheet, uliza kampuni zote kama watakuonyesha hii, but ni only AUTOCOM JAPAN LIMITED USED CARS IMPORTERS.
For the case of tra tax just nipe Gari model /mwaka call /whatssap 0767328063 I can help
 
Autocom Japan Tanzania Used car Importers, located QUALITY Center, Nyerere Road Dar es salaam almaarufu kama uchumi supermarket, call /whatssap 0767328063 or ask for Msuya
 

Attachments

  • 1432574933708.jpg
    46.4 KB · Views: 481
Last edited by a moderator:

kwa jinsi ulivyoandika huwezi kupata.
fanya hivi:

1.andika part number ya spare unayotaka wenye nayo watakutafuta
2.weka details za gari na jina sahihi la spare unayotafuta.
mfano :
natafuta CRANKSHAFT POSITION SENSOR ya
2003 toyota rav 4
chasis number ACA/SXA.........
2000CC
Automatic
 
Aisee huyo fundi aliyechomoa wire wa gauge ya temperature usisome ni jambazi na muuaji mkubwa wa hiyo gari
Hebu tafuta fundi makini acheki yafuatayo
-wiring
-radiator n water system ikiwemo pump
-radiator fan
-engine block
-radiator cap

Ahsante mkuu nimetafuta fundi akafunua head cylinder akaichonga pia kuna ile ckumbuki jina lake ina wembamba wa kadi ila ina matundu kama manne inakaa katikati inaozuia maji yasiingie kwenye piston ilikua imekatika so maji yakawa yanaingia
 
Jamani mwenye uzoefu na Volkswagen toureg or Tiguan hapa bongo. Vipi mafundi wanazimudu?
 
Jamani mwenye uzoefu na Volkswagen toureg or Tiguan hapa bongo. Vipi mafundi wanazimudu?

Ukiwa unataka kuinunua please let me know, we are Autocom Japan Tanzania. Car importers from Japan, we are located QUALITY Center, Nyerere Road Dar es salaam almaarufu kama uchumi supermarket. Call /whatssap 0767328063 for more details.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu msaada nina kausalifiri kangu ka kunitoa sehemu moja kwenda nyingine aina ya premio e, cc 1800,nahitaji kujua pale kwenye gear liver kwa pembeni kuna button inaitwa ect power na ect manu inavyoapear kwenye dash board nahitaji kujua ni wakati gani zinatumika asante.
 
Wadau nauliza kati ya toyota allion na axio ipi ni bora na sababu gani? Mafundi bongo wana ziweza? Zote cc1500
 
Wadau nauliza kati ya toyota allion na axio ipi ni bora na sababu gani? Mafundi bongo wana ziweza? Zote cc1500

Una wasiwasi wa kupatikana kwa mafundi kwa gari za Toyota TZ, hao ndio wamejaa!!
 
Una wasiwasi wa kupatikana kwa mafundi kwa gari za Toyota TZ, hao ndio wamejaa!!

Wasiwasi ni kusikia kuna gari mafundi zinawasumbua ambqzo umeme mwingi
Nishauri hapo ubora na ubovu wa hizo gari tajwa
 
wadau kuna gari mbili hapa mnishauri ninunue ipi kwa uzoefu wenu kati ya toyota corola altis na toyota cresta ,mrejesho nitauleta hapa
 
wakuu heshima kwenu:
kuna ka vx nataka kumvua mtu ila turbo yake imekufa.Naomba mnisaidie ushauri kwa maswali haya:
1: Gari aina ya VX ambayo ilitengenezwa na turbo kama turbo ikifa ni tatizo kubwa sana kwenye gari kwa maana ya kwamba inaweza kuuwa kitu kingine ikiendelea kutumika bila kurudishia hiyo turbo?
2: Je turbo inaweza kuwa cancelled for good na isilete madhara au hitilafu kwenye gari?
3: Nini faida/hasara ya turbo kwenye gari?
 

Mkuu Turbo mpya si chini ya m.8
 
Mkuu Turbo mpya si chini ya m.8

Mkuu nashukuru kwa kunijuza bei ya turbo,lakini hebu jikite kwenye maswali yangu matatu halo juu utakuwa umenisaidia sana.
Cc:mshana jr,RRondo na wengineo mkuje huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…