Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.

Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.

Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake

Karibuni sana

Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania

View attachment 225786

Nashauri zile mada kubwa zilizoanzishwa ndani ya uzi huu uweke links zake kama ulivyofanya kwa hizo mbili hapo juu. Itakua rahisi saana kwa wageni, au new interest kujua waanzie wapi, au kupata ishu wanayotaka kujua kuhusu magari.
 
mndughu Mshana jr. urewedi? nami pia naomba niunge kwenye grup kwa no. 0658 542409.ahsante
 
Mkuu gari yangu ni Toyota Allion inapiga sana kelele kwenye stering nimeshapeleka kwa fund mara kibao lkn wakigundua hiki baada ya siku 2 tu inaanza kelele tena nn tatizo Mkuu mnisaidie
 
Mkuu gari yangu ni Toyota Allion inapiga sana kelele kwenye stering nimeshapeleka kwa fund mara kibao lkn wakigundua hiki baada ya siku 2 tu inaanza kelele tena nn tatizo Mkuu mnisaidie

Binafc cjakuelewa, inapiga kelele ukiwa unafanya nn? Na hzo kelele zinatokea sehemu gan??
 
Wakuu samahani sana nina shida kidogo, kesho natarajia kusafiri kwenda Tunduma kutokea Dar.(naombeni dua zenu)
Sasa naombeni ushauri kuhusu route,kama inavyojulikana kipande cha barabara toka kibaha mpaka chalinze ni kibaya mno mno mno urefu wake ni kama km 70 hivi (kibaha-chalinze)
Je kupitia bagamoyo-msata-chalinze vipi? Je ni umbali gani?
Natanguliza shukrani
 
Habari za kazi wadau wa magari.

Nimeyapenda gari hizi ; Ford escape na Mazda tribute kwa kuangalia umbo lake la nje tu, kwa kweli ningependa siku za usoni kumiliki moja ya magari hayo. Naomba mnisaidie je? kwa uzoefu wenu lipi ni bora kwa kuangalia upatikanaji wa spea na unafuu wa bei, ulaji wa mafuta, kudumu na mengineyo.

Natanguliza shukrani
 
Hivi kwa mfano ukinunua gari Japan afu ukapitisha bandari ya Mombasa...ni lazima ulipe kudi kandamizi ya Tz?.Msinicheke;Nisaidieni...
 
Na vipi hawa Real Motors ambao wako registered under Trade Car View.Gari zao ni bora kiasi gani?
 
Habari ya jpili wadau! Naomba mnisaidie,hii taa ikiwaka kwenye dashboard inaashiria nini?
 
Attachments

  • 1441534021038.jpg
    1441534021038.jpg
    36.5 KB · Views: 369
Na vipi hawa Real Motors ambao wako registered under Trade Car View.Gari zao ni bora kiasi gani?

Real motors gari zao ni nzuri sana.Yaani kila nikiingia trade car view kuagiza gari huwa natafuta za kutoka kampuni ya real motors.Nimesha agiza gari 5 tofauti kutoka real motors na zote nimezipokea zikiwa kwenye Excellent condition.Usiwe na wasi wasi na hiyo kampuni.Director wake wa sales Anaitwa Miha Matsouka.Pia
Kuna Real motors jr hao sina uzoefu nao.
 
Ahsante sana mkuu.Kwa maelezo yako Murua.
 
Mkuu gari yangu ni Toyota Allion inapiga sana kelele kwenye stering nimeshapeleka kwa fund mara kibao lkn wakigundua hiki baada ya siku 2 tu inaanza kelele tena nn tatizo Mkuu mnisaidie

Kwenye stering ukimaanisha miguu ya mbele.....?.....hebu cheki mambo haya......

stabilizer bush.......
stabilizer link.....
booty rubber.........
rack hand.........
kama haya yote umepitia.......sema......tuendelee na maelezo..........
 
Back
Top Bottom