RugambwaYT
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 1,397
- 1,899
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania
View attachment 225786
Nashauri zile mada kubwa zilizoanzishwa ndani ya uzi huu uweke links zake kama ulivyofanya kwa hizo mbili hapo juu. Itakua rahisi saana kwa wageni, au new interest kujua waanzie wapi, au kupata ishu wanayotaka kujua kuhusu magari.