Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Msaada wenu gari timing belt ilikatika nikaivuta mpaka mjini sasa nimebadili hiyo timing belt gari imewaka ina misi ya hatari kabisa sasa hawa mafundi wananiambia itakuwa imeharibu vitu vingi sana kwenye engine maana ilipo nizimikia nilijaribu kuiwasha sasa fundi anasema ndio nilifanya makosa hapo sasa amenitajia vitu vingi Mimi sio fundi sivijui ghalama yake anasema inafika 500000 na gari ni cresta gx100 vvti
 
Mmh sidhani kama ni kweli
cc: LEGE
 
Nitafute njoo hapa Mwenge jirani na Dispensary ya Mwenge litapona usiogope call 0712115220 ukifika.
 
Swali kwann spacious new model zikienda safar ndefu uchemka?nini cha kufanya kuzuia tatizo hilo?
 
Ni kweli mkuu fundi yupo sahihi.
Kwanza nianze kukulaumu na kuseme huo ni uzembe wa hali ya juu sana .

Kwa upande wangu hapo najua kitu ambacho kimeharibika ni valve lazima zitakuwa zimepinda ndio maana gari ina miss sana na hiyo pesa usilalamike wala sio nyingi kama ni jumla kwa kazi zote pamoja na garama ya kifundi.ina maana hapo lazima ufungue cyrinder head ubadili valve zilizo pinda,ubadili valve seal,cyrinder head gaskate,na kuifanyia service kbs.

Au kama vipi kanunue engine nyingine mswaki kama laki 7 au 8 hivi weka hapo..


Maana gx100 huwa inakuwa na kamiss flani hivi kanakera sana.hutokana na valve.
 
Swali kwann spacious new model zikienda safar ndefu uchemka?nini cha kufanya kuzuia tatizo hilo?
Safari ndefu hiyo unayoizungumzia ni kutoka wapi mpaka wapi mkuu.

Na kama ni hivyo basi usihangaike sana mkuu nifahamuvyo mm unaweza ukatoka na gari from dar to mwanza kama iko powa haina shida na haiwezi chemsha labda kama kuwe na shida kwenye gari yako.labda cooling systerm haijakaa sawa.
 
Gari imeleta mushikeli kadri ninavyokanyaga accelerator ile gear box inapiga kelele kama vyuma vinapigana, awali iliwekwa ATF isiyo sahihi, baada ya kuiweka ATF sahihi mlio wa kelele umepungua kiasi lakini bado nahitaji msaada zaidi kujua nini kimeathirika na inatibikaje. Msaada tafadhali wandugu
 
Mkuu hembu nyoosha maelezo basi yaliyo nyooka ni sawa na kumwambia dr naumwa.au najisikia vibaya.
Gari aina gani
 
Asante ndugu kwa ushauri mzuri mpaka sasa bado sijafanya maamuzi maana kunamajukumu yamenibana keshokutwa jumamosi ndio nitafanya kazi hiyo nitafungua cylinder head niangalie kama zimepinda na kufanya maamuzi ya kununua engine nyingine ama kulekebisha huku kwetu geita engine hizo zinauzwa 13000000
 
Nakushauri ukiwa tayari , fanya kazi na huyo mdau LEGE pamoja na kuwa na uhakika na matengenezo based on ushauri wake, pia utakuwa umemuunga mkono kwenye futari/ mkate.
 
Hiyo gharama ni complete ya 1.3 nahisi itakuwa, umeaambia na bwana LEGE nunua mswaki,nilivyoelewa ni engine isiyo na makandokando yake mfano.stering power, self,alternator n.k huko kanda ya ziwa ni maarufu kama half engine, nakushauri kanunue half engine ni almost 7.5 k.
 
Asante sana ndugu kesho ndio nitafanya zoezi Hilo nashukuru kwa ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…