Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mshana Jr,asante kwa thread hii.Swali langu ni je ntajuaje kuwa gari inakula Oili kuliko kawaida yake? Ishara za gari kula oil ni zipi? Asante.
Gari za kisasa zina sensor Lakini kama ni ya kizamani
1. Utajua kupitia dip stick unapocheki kiwango cha oil
2. Moshi mweupe kwenye exhaust
 
Tofauti ni mbwembwe tu za matoleo.. Ila shida kubwa ya hizo gari ni gearbox
 
Swali Kwa wazoefu barabarani. Ikiwa ndio naingia barabarani Kwa mara ya kwanza. Na sipendi niguswe au niguse gari Ingine...ni nini cha kuzingatia.
Sheria na kanuni za usalama barabarani.. Baki kwenye mstari wako na umbali rasmi toka gari hadi gari ni mita 4
 
Gearbox ina shida mostly chekeche ni chafu haijafanyiwa service muda mrefu
 
Gari za kisasa zina sensor Lakini kama ni ya kizamani
1. Utajua kupitia dip stick unapocheki kiwango cha oil
2. Moshi mweupe kwenye exhaust
Kuna nyingine.hazitoi mosh but zakula oil..but labda cha kuongeza anaweza check spark plugs akikuta zina oil ujue oil inafika kwa combustion chamba ...au apige less kidogo injini aone aina ya moshi unaotoka kwa exhaust pipe, kama moshi wa blue maana YAKE oil inachomwa...au injini ikiwa imewaka nenda kwenye exhaust sikilizia harufu ya exhaust pipe kama unasikia.harufu tofauti na petrol iliyo chomwa maana yake injini inachoma oil..
 
Sawa sawa [emoji1545]
 
Gari yangu haitulii barabarani hasa inapofika spidi 40 kwenye lami,na 60 kwenye changarawe,while allignment nimefanya,upepo huwa napima mara Kwa mara.Ushauri wenu tafadhali.Ni Suzuki old model.
 
Gari yangu haitulii barabarani hasa inapofika spidi 40 kwenye lami,na 60 kwenye changarawe,while allignment nimefanya,upepo huwa napima mara Kwa mara.Ushauri wenu tafadhali.Ni Suzuki old model.
Ball joints ziko sawa?
Stabilizer links je umecheki ziko ok?
 
Gari yangu haitulii barabarani hasa inapofika spidi 40 kwenye lami,na 60 kwenye changarawe,while allignment nimefanya,upepo huwa napima mara Kwa mara.Ushauri wenu tafadhali.Ni Suzuki old model.
Haitulii kiaje mkuu ili upewe ushauri mahususi kutokana na changamoto gari yako iko nayo
 
Habari wanajamvi.
Nina plan ya ku upgrade sedan yangu to Suv
Sababu kubwa ni safari nazofanya 3 times a year (km 3500 go and return)
Nimekuwa nikitumia Premio second generation (inafanya poa highway perfomance na confortability)
But kwenye mizigo na rough road ndo mahali ime prove failure kila nikifanya hizo safari hata 1 nakuta bush zote zimekufa. Na inagusa na kugonga sana chini
Nawaza kuamia kwenye mid range suv
Naomba ushauri ni gari gani ni best mid suv ya kuanzia 2009 to 2012 ikiwa nazingatia dursbility na fuel consumption.
Machaguo yangu adi sasa ni
1.Rav 4 (2007/09) engine 2az
2.kluger v engine 2az
3.harrier tako la nyani engine 2az
Angalizo(bado ni hard fun wa toyota)
Kama kuna machaguo zaidi kwenye hizo gari upande wa Toyota share hapa
Kabla sijafanya maamuzi
Nikiamin hapa.kuna waliotumia hizo gari ama wana weza recomend any other car within range hiyo lakin toyota
Brand nyingine usipoteze muda kunishauli mm ni toyota damu.
 
Go for Klugger hutajuta ni gari ya kazi hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…