Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali


Kesi za traffic huwa hazichukui muda kwa uzoefu wangu kama daladala ndio mwenye makosa keshafanya yake na mpelelezi hasa kama bima yake si halisi
Cha kufanya usipoteze muda zaidi katengeneze gari yako kwakuwa hata ukishinda wewe utapata usumbufu mkubwa kwenye malipo kwakuwa hiyo sio bima yako
 

Pole mkuu kwa masaibu hapo check upepo kama daladala ndo mwenye kosa mi nashauri usamehe yeshe then ukatengeneze gari,but helpful advice next time go for comprehensive mkuu
 
Habari za jioni wadau, kama kichwa cha habari kinavyo zungumza, ni na ndugu yangu anahitaji kujua ubora wa hizi gari kwenye utumiaji mafuta, uimara wake kwa ujumla na huwa zinasumbua nini zinapokuwa na matatizo, yeye anaishi Mbezi mpiji Magohe bara ni changarawe ila si mbaya sana, anaombeni ushauri ipi iko bora. naamini katika mawazo mazuri.ASANTENI.
 
Mkuu kwa jinsi ilivyo Mazda Demio ni imara shida inakuja kwenye spare parts zake ni expensive kidogo..na hiyo Passo ni nzuri sana kwenye fuel consumption shida siyo imara na kwa sisi tunaoishi huku Mpiji Magohe ni barabara yetu inamahandaki kinoma..tafuta gari ya juu kidogo ambayo inaendana na mazingira yetu..achana ni hizi mbili utalia mkuu
 

Nkushukuru Gogo La choo..vipi kuhusu utumiaji wa mafuta wa hii Mazda?
 
Habar wadau na brother mshana!naomba kuuliza,hivi gari za Alteza mbona zinauzwa bei chini sana,yani unakuta M 6 mpaka 8,wakati mi naona huwa ni gari nzuri kwa na yenye mvuto,Je ni kwanini iuzwe cheap sana,je huwa zinakasoro gani kubwa,Ahsante
 
Habar wadau na brother mshana!naomba kuuliza,hivi gari za Alteza mbona zinauzwa bei chini sana,yani unakuta M 6 mpaka 8,wakati mi naona huwa ni gari nzuri kwa na yenye mvuto,Je ni kwanini iuzwe cheap sana,je huwa zinakasoro gani kubwa,Ahsante

Mmh Investigator hili ni geni kwangu, bei poa ya Altezza niliyowahi kuona ni million 9! Nitafuatilia
 
Last edited by a moderator:
Tugari tudogo cc650-2000 ni gari za madada, most likely 'wamehongwa'

Mara nyingi mawazo na mitizamo yetu katika maisha yanachangiwa na vitu vingi ikiwemo mazingira ya asili tulikozaliwa kwa hiyo kwa kauli hii sikulaumu nalaumu mazingira ya asili uliyotokea
 
Habari, Nashukuru sana mleta mada kwa kaunzisha uzi hu muhimu. Mie nina shida na injini ya gari aina ya Mistubishi Pajero V24, inatumia injini aina ya 4D56, naomba mwenye uelewa zinapopatikana hapa mjini pamoja na bei yake anielekeze, au kama anafahamu kampuni ninayoweza kuagiza moja kwa moja nje ya nchi au njia ipi ni bora kununua hapa hapa bongo au kuagiza Japan. Nashukuru.
 

Nikumbushe kesho nikutumie contacts za Nairobi au ingia online moja kwa moja www.mitsubishikenya.com, weka model ya gari na part number nk
 
Habari za wakuu,
mshana jr naomba kujuzwa uimara wa Nissan Xtrail hizi za kuanzia 7/2007 (NT 31). Upatikanaji wa spear parts na mafundi wenye ujuzi nazo. Msaada tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
päiva;12287704 said:
Habari za wakuu,
mshana jr naomba kujuzwa uimara wa Nissan Xtrail hizi za kuanzia 7/2007 (NT 31). Upatikanaji wa spear parts na mafundi wenye ujuzi nazo. Msaada tafadhali.

Kwangu ni gari nzuri lakini kwa wengi zinakandiwa kwa ubovu ngoja tuone wajuzi wengine watupe uzoefu wao kwenye hili

Kwa spare kidogo bei iko juu na hii ni kwa Nissan zote! Mafundi inategemea gari ina shida gani
 
Last edited by a moderator:

Alternatively unaweza waona BF Tz pale Chimara Road wanaimport engines pia watakusaidia
 
naomba kuuliza kama nitaeleweka gari ambayo model yake ni 240gl manake nini

240 gl ni aina mojawapo ya gari aina ya volvo ambazo zipo kwenye kundi la 200 series iliyokuwa upgraded kutoka 140's series,kwa hapa Tanzania ni nadra sana kuziona zilikuwepo chache miaka ya 90 but kwa sasa zipo chache ktk version hiyo 240 ndo ilikuwa yenyewe kama peugeot 504 enzi zake,spare zake hapa bongo ni adimu sana
 
Mara nyingi mawazo na mitizamo yetu katika maisha yanachangiwa na vitu vingi ikiwemo mazingira ya asili tulikozaliwa kwa hiyo kwa kauli hii sikulaumu nalaumu mazingira ya asili uliyotokea

Hahahaha we acha kupredict maisha yangu, hujui hata najuana vip na huyo nimemjibu. Pole lakini ka imekugusa, jitahid tu uache baby walker😪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…