Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ni kweli mkuu hazihimili mikiki, huwa naiangalia hususani kwenye rough road sio nzuri kivile, na pia haitaki kubebeshwa mzigo mkubwa, watu wanne zaidi haitaki. Lakini nilichoipendea ni kwenye consumption inakula kidogo saana hasahasa kwenye long safari, pia siti zake ndani zipo comfortable hauchoki kwa safari ndefu, kikubwa zaidi bei yake ya ununuzi ni attainable.
 
Roughrider na mtu mwenye mishemishe nyingi Spacio haimfai kabisa! Ni gari ya shughuli zenye ukomo hapo utaipenda na kuifurahia
 
Heshima kwenu nyote.

Nimevutiwa sana na muonekano au muundo wa haya magarii gari madogo ya kutembelea yanayoitwa Daihatsu Terios (CC 1290), Daihatsu Terios Kid (cc 650), Daihatsu Terious Lucia (cc 650). Lakini shida niliyonayo ni kwamba sina taarifa zozote kuhusiana na uimara, uzuri, upatikanaji wa spea zake jijin Dar es Salaam nk. Naombeni msaada wenu wadau wenye uzoefu na haya magari ili kama vipi niachane nayo au nichukue moja wapo kati ya hizo. Picha zake hiz hapa

http://image-cdn.beforward.jp/large/201503/483394/BF378206_4b7b55.jpg (Daihatsu Lucia cc 650)

Used TERIOS KID DAIHATSU for Sale | BF373707 | Japanese Used Cars Exporter BE FORWARD (Daihatsu Terios Kid cc 650)

Used TERIOS DAIHATSU for Sale | BF371450 | Japanese Used Cars Exporter BE FORWARD (Daihatsu Terios cc 1290)
 
ABS (automatic breaking system), hii maana yake ni kwamba unapofunga break inabidi tyre zote zifunge break proportional kuepuka gari kupinduka, ukiona imewaka basi kuna matatizo. ni vizuri umpelekee fundi kwa uchunguzi zaidi.

Mkuu gulf umemshauri vizuri apeleke gari kwa fundi...ila.ABS maana yake ni Anti Lock Breaking System. Ukifunga brake kwa ghafla inazuia locking ya matairi au kujifunga kwa matairi yakaacha kuzunguka.. hivyo kuzuia skidding na pia kumpa dereva uwezo wa kumudu gari kwenye mazingira hatarishi ya kufunga brake gafla. Mfumo huo, unapunguza umbali wa braking ijapokuwa kwa mazingira mengine kama kwen snow umbali unaongezeka ila dereva analimudu gari.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu gulf umemshauri vizuri apeleke gari kwa fundi...ila.ABS maana yake ni Anti Lock Breaking System. Ukifunga brake kwa ghafla inazuia locking au kujifunga hivyo kuzuia skidding.

Nilishawahi kubisha kuhusu hilo lakini hiyo ndio tafsiri sahihi ya ABS
 
Last edited by a moderator:
Kwamba kirefu cha ABS ni automatic break system kumbe ni Anti break system

Hahahaa pole mgosi wengi wanadhani ni automatic kiredu chake ijapokuwa inafanya hiyo kazi automatically bila dreva kujua
 
Hahahaa pole mgosi wengi wanadhani ni automatic kiredu chake ijapokuwa inafanya hiyo kazi automatically bila dreva kujua

Yeah na kwakweli kiuhalisia ndio maana yake
 
Nahitaji engine ya rav4 3s manual transmision,gearbox yake,control box yake pamoja na waya zake.
Pia nahitaji fundi anayeweza kuifungakwenye freelander
 
Nahitaji engine ya rav4 3s manual transmision,gearbox yake,control box yake pamoja na waya zake.
Pia nahitaji fundi anayeweza kuifungakwenye freelander

Fika maduka ya spare used Ilala na Tandale uzuri utasaidika
 
pia niliwahi kusikia kuwa ABS power transmission katika inajitegemea kwa kila mguu/tairi, na ina uwezo wa kutambua mwenendo wa usukani kulinganisha na mwendo wa gari lenyewe

Yeah na ndio maana tunaita Automatic
 
wakuu nahitaji kwenda mwanza nataka niende in two weeks time na nataka nitumie siku mbili tu maana nitaenda na vitz yangu je haitanisumbua kwa lugha nyingine naweza kwenda na vitz from dar to mwanza kwa kutumumia siku moja au mbili pekee???????
 
Fanya service ya uhakika chapa mwendo wa wastani utakapoona unechoka pumzika!
 
wakuu nahitaji kwenda mwanza nataka niende in two weeks time na nataka nitumie siku mbili tu maana nitaenda na vitz yangu je haitanisumbua kwa lugha nyingine naweza kwenda na vitz from dar to mwanza kwa kutumumia siku moja au mbili pekee???????

Kama ni ya cc 1300 shaka ondoa utafika ndani ya siku moja tena mapema kuliko mabasi,,,cha muhimu chunga rpm
 
anaesema anti lock break system yuko sahihi na anaesema automatic break system pia yupo sahihi haya mambo ya lugha hasa kwenye magari yana vary sana nchi kwa nchi kule marekani ukiwaambia about changing the gears from number one to five hawakuelewi wao wanajua shifting the gears from first gear to fifth gear so ni kama hivyo tu.
 
wakuu nahitaji kwenda mwanza nataka niende in two weeks time na nataka nitumie siku mbili tu maana nitaenda na vitz yangu je haitanisumbua kwa lugha nyingine naweza kwenda na vitz from dar to mwanza kwa kutumumia siku moja au mbili pekee???????

Mkuu unless gari ina tatizo unaenda siku moja tu...ukitoka saa 12 unakula Dodoma then una km 700 saa nne tano usiku unaingia kama sio mvivu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…