Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Pale kwenye gearlever kuna kirungu kidogo kimeandwa 2WD na 4WD unachagua, nafikiri mbele ni 2WD na nyuma ni 4WD

Okay thanks...

Je ni Ushauri UPI unanipa katika kutumia njia hizo? Kwamba 4wd na 2wd IPI bora kutumia muda wote?

Je ulaji Wa mafuta kwa 2wd na 4wd unatofautiana?
 
Pale kwenye gearlever kuna kirungu kidogo kimeandwa 2WD na 4WD unachagua, nafikiri mbele ni 2WD na nyuma ni 4WD

unakuta gari imeandikwa speed180 mayb,wanakuandikia ina produce hp kadhaa na kw kadhaa,hizo ni nin?
 
Kaka Mshana, hongera kwa kazi ya kutuelimisha kuhusu magari. Naomba kujua wapi naweza kupata engine na gear box mount ya pajero mini na bei zake zipoje. Pia kama nitapata contacts za wauzaji wa hicho kifaa utakuwa umenisaidia sana.
 
Wakuu niko na honda crv i5, miezi michache iliyopita ilipunguza nguvu yake mara siku zinavozidi kwenda inaanza kusinzia kupandisha miinuko, mbaya zaid siku hizi inashituka kila inapobadili gear. Tukafikiri labda ni plugs lakin pia baada ya kubadilisha plugs hali iko vile vile haiwezi kubadili gear bila kushituka. MSAADA WADAU
 
Okay thanks...

Je ni Ushauri UPI unanipa katika kutumia njia hizo? Kwamba 4wd na 2wd IPI bora kutumia muda wote?

Je ulaji Wa mafuta kwa 2wd na 4wd unatofautiana?

Nafikiri tumia 2WD kwenye barabara za kawaida na tumia 4WD pale inapobidi, ambapo pia nadhani ulaji wa mafuta huongezeka kidogo
 
Hilo ni tatizo la gearbox aidha hydraulic imepungua au inahitaji service, nakushauri onana na mafundi wajuzi wazoefu
 
unakuta gari imeandikwa speed180 mayb,wanakuandikia ina produce hp kadhaa na kw kadhaa,hizo ni nin?

HP ni kifupicho cha Horse Power, yaani nguvu ya msukumo inayotoka kwenye engine
 
Kaka Mshana, hongera kwa kazi ya kutuelimisha kuhusu magari. Naomba kujua wapi naweza kupata engine na gear box mount ya pajero mini na bei zake zipoje. Pia kama nitapata contacts za wauzaji wa hicho kifaa utakuwa umenisaidia sana.

Kwa bei sina hakika lakini nakushauri tembelea njia ya Tandale uzuri wanakata sana magari ya aina mbalimbali kule (samahani upo Dar lakini?) Au ukikosa nenda Ilala
 
Kwa bei sina hakika lakini nakushauri tembelea njia ya Tandale uzuri wanakata sana magari ya aina mbalimbali kule (samahani upo Dar lakini?) Au ukikosa nenda Ilala

Nipo Dar kaka. Asante kwa ushauri
 
Hilo ni tatizo la gearbox aidha hydraulic imepungua au inahitaji service, nakushauri onana na mafundi wajuzi wazoefu

Mshana jr. Nashukuru kiongozi ngoja nicheki mafundi kwa hiyo gearbox ila service niko makini sana kuifanya sipitishi klm.
 
Mshana jr. Nashukuru kiongozi ngoja nicheki mafundi kwa hiyo gearbox ila service niko makini sana kuifanya sipitishi klm.

Pouwa lakini pia zingatia hili kwamba wakati wa service unakuwepo mwenyewe, unaweza kuwa makini na service lakini ukawa unamtuma kijana au fundi ni hatari kwakuwa huwezi jua atafanya kama unavyotaka au inavyotakiwa
 
Mkuu nilikuuliza 4WD kwenye ESCUDO unawekaje au ni full time 4WD huwezi itoa?

Sorry nadhani sikupita nikaliona swali lako mkubwa, uzuri wadau washajibu hapo mostly Suzuki nyingi 4wheel yake una-engage via shift stick tofauti na all time 4wd kama kwenye baadhi ya Toyotaz na brands nyinginezo...
 
Jamani wanajamvi naomba kujua mambo ya msingi ya kuangalia ili kujua kama gari ni nzima au kimeo kwani nahitaji kununua na kuuza used cars...Asanteni sana kwa ushirikiano!

Njia muhimu na inayofaa kuliko zote hakikisha gari linakuwa checked sio na fundi uchwara!
magari ya siku hizi yanahitaji mafundi wenye professional skills na uzoefu ktk magari kwa sababu mengi ni computerized na complicated + yanakuja na new technological advances kila uchao.

Mpate fundi mahiri kama hutojali njoo pm nikupe vijana, au wapate kwenye garage zinazojitambua for checkups, kulijua gari inahitaji system scanner ya kueleweka ili kucheck mifumo kama iko okay,tunacheck kama hakuna leakages za fluids,tunacheck torque levels,transmission workability,industrial chassis balances,na kufanya minor au major diagnosis kama inahitajika.
Kimsingi yanaangaliwa mambo mengi japo laymen huangalia mileage,body condition,yr of mnfctr,fasheni mambo ambayo ni very minor...Injini yako ndo gari lako...ili hiyo business isidode nakushauri seek technical assistance mkuu.
Hata hivyo kuna viashiria vichache kama mitetemo,kuchelewa kuchanganya,kuvuta upande,kunywa mafuta kuzidi kawaida,oil kuisha haraka,overheating,kusinzia kwa viashiria kwenye dashbodi,silencer isiyo-maintain kwa kitambo,kuchakaa matairi upande mmoja,gia kutobadilika kwa haraka/muda mrefu km ni auto,,,dah mambo ni mengi ila jua kwamba second hand vehicle always ina ubovu fulani so get it checked kabla hujainunua au kuuza
 
Viongozi mbarikiwe kwa maswali na majibu mazuri, uzi huu ni mmojawapo ambao wachangiaji wametanguliza hekima na busara kwa aina yeyote ya swali najibu lake inapendeza kwa kweli, asante Mshana kwa uzi huu,
Wandugu nina Toyota landcruiser 1HZ manual , nimeinunua serikalini kwa kweli imetumika vibaya sana na imechoka, nahitaji kuifufua ili iwe vzr jee niende gerage gani ama nimuone fundi yupi kwa ushauri then matengenezo, niko dar, nashukuru sana wanaJF
 
Wakuu naombeni mwenye uzoefu wa kuendesha CVT transmision anipe utofauti wake na AT transmission
 
Wakuu naombeni mwenye uzoefu wa kuendesha CVT transmision anipe utofauti wake na AT transmission

Tafadhali naomba muwasiliane na N'yadikwa na Kaizer lakini pia naamini watapita hapa muda si mrefu
kuhusu hiyo land cruiser je inatembea?
 
Last edited by a moderator:
Kwa mahitaji ya rally car tuwasiliane, pia tunaweza transforming gari yoyote from it's origin to Rally car (vehicles) Example hii ni Suzuki swift na Mazda demio
 
Mkuu Nenda Toyota watafute wale mafundi wapo vizuri sana kwenye hizo Cruiser unaongea nao watakufanyia kwenye karakana zao,ukishindwa Nenda keko garage pia wanazielewa vizuri sana cruiser
 
We kweli nyadikwa mkuu...maana yake mbegu kwa lugha ya mama yangu mzazi.....na sifa ya mbegu lazima ipandwe na kuzaa HAHAHAH NTAKU-PM MKUU
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…