Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mmh!!!kweli Watanzania tuna shida sana,hapa naamini 90% ya waliocomment hawajawahi kumiliki hii gari!anyway nnachotaka kusema ni hivi,hii gari ni bora kuliko wengi mnavyofikiri ndio SUV inayotumika zaidi Marekani,hii gari brand yake inaitwa Isuzu trooper,imetengenezwa na Mjapani kati ya mwaka 1981-2005,hii gari imekuwa ikisambazwa kwa engine moja yenye uwezo tofauti huku ikijulikana kwa majina tofauti kulingana na sehem husika ,majina hayo ni pamoja na Isuzu Bighorn, Isuzu Trooper, Isuzu Trooper II, Caribe 442, Acura SLX, Chevrolet Trooper,Subaru Bighorn, SsangYong Korando Family, Honda Horizon, Opel/Vauxhall Monterey, Holden Jackaroo, pamoja na Holden Monterey.

Watanzania wengi tunapenda kuangalia swala la mafuta bila kujua gari ina engine ya aina gani!,hizi gari zina engine zinazotumia petrol na zingine za diesel,kuna zenye cc 2500,2900,2999,3500,4000,4500 n.k kwa petrol na diesel,kwa hiyo utumiaji wa mafuta itategemeana na wewe umenunua ipi,kwa mfano ukinunua inayotumia petrol na yenye cc 4500 ni nini unatarajia??

Kwa upande wangu mimi nilianza kutumia Nissan Murano,then nikatumia Rav4 1998,alafu nikatua kwenye Isuzu Bighorn 1999 inayotumia diesel na yenye cc 2900,yani toka mwaka 2001 sijatoka hapa na sidhani kama nitatoka tena,hii gari nimekuwa nikienda nayo mikoani kwa miaka zaidi ya kumi sasa na ina km 450,650,lakini mafuta ni 1ltr per 11km,hata rav4 niliyokuwa natumia haifiki hapa.spear za hii gari zipo kuliko watu wanavyofikiri...kkoo kuna maduka manne makubwa yanayouza spear za Isuzu Bighorn tu.

Ushauri wangu ni kwamba, ukiipata hii gari inayotumia diesel, alafu ina cc 2900,alafu in Turbo charger,nakuhakikishia hutajuta kamwe,na gari pekee itakayoyokuacha barabarani ni V8.
 
Wadau hivi karibuni nimenunua ISUZU BIG HORN SUV ya mwaka 1998 imetembea 280,000 kms daah sasa nimeanza kutembelea inakula mafuta kama JINI MAHABA ya 1 ltr = 3kms yaani pamoja na kufungua vioo na kuweka FREE mara kibao imekuwa hatari. Najutaa kununua huu mgari na hela ya mkopo jamaa wa NMB ndo wameanza kukata mwezi huu
.Usifanye kosa kama langu mdau

Mkuu hii gari kama uko serious,weka specification zake hapa alafu tufanye biashara leo leo.
 
Mkuu haitaki kuwa na digrii kung'amua gari kimeo, Formula ni rahisi ukiona gari ambayo serikali haijanunua (ikiwemo BIGHORN) ujue hapo MSALA. Eti wengine wanadai ubadilishe ENGINE ndo lengo la kununua hiyo gari?
 
Habari zenu wakuu.
Natafuta gari ya kununua hapa Bongo. Kuna matangazo ya uuzwaji wa magari kupitia mtandao wa Zoom na nimeona ni bora kupata hapa usafiri.
Kwa mwenye ujuzi na uzoefu wa magari ni mambo gani ya kuzingatia/kuangalia kujua ubora wa gari ambalo limekwishatumika.

Naona uagizaji wa usafiri kutoka japan ni gharama zaidi ukizingatia dola ilivyopaa. Nimeandaa m8 kwa ajili ya IST.
 
Nissan X-TRAIL (SIMTANK) ni janga haswaa maana kwanza body yake ni PLASTIK ukiw unalipitisha kwenye rough road lazima lichoke mapema, sasa kimbembe ukwaruzane na gari nyingine linapasuka kama ndoo ya maji. halafu linasumbua sana kwenye SENSOR.
 
Kuna uzi humu unaohusu magari hebu jaribu kuutafuta
 
Mkuu haitaki kuwa na digrii kung'amua gari kimeo, Formula ni rahisi ukiona gari ambayo serikali haijanunua (ikiwemo BIGHORN) ujue hapo MSALA. Eti wengine wanadai ubadilishe ENGINE ndo lengo la kununua hiyo gari?


Mkuu Serikali hainunui magari used hizi gari toleo la mwisho ni la mwaka 2002,na hizi gari ni ngumu kuipata mpya,hata hivyo kuna office kibao bado zimebakiwa na hizi gari kama hujui,viongozi wetu wanapenda gari mpya zinazotoka sasa hivi,ndio maana unaona mashangingi yamejaa serikalini, vile vile point yako bado haina maana kwa kuwa sio lazma serikali inunue gari ndio uone ni bora,kaa ukijua kuwa the most reliable SUV of all time ni Range Rover,je ushawahi kuona serikali imenunua hii gari??je inamaana ni mbovu?? kwa taarifa yako serikali ndio inaongoza kwa kununua magari mabovu...kwa mfano Ashork leyland,hyundai,ford,Kia...n.k
 
Mkuu Lusungo tofauti na hawa Toyota je naweza Pata wapi at least fundi mzuri wa kunitengenezea hiyo gari, nilichomwelewa mkuu N'yadikwa ni kuwa gari haitengenezwi chini ya mwamvuri wa Toyota bali ninakubaliana na fundi wa Toyota then kazi hiyo inafanyika kwenye gereji/eneo nje ya Toyota lakini na wataalam hao hao wa Toyota ,
Asante wakuu



Waone hawa.... nimekopi hii thread kutoka jukwaa kazi;




Yesterday
sisi ni vijana watatu kutoka toyota tz
,tunatengeneza
engine aina zote hasa za V8.Yeyote mwenye
kuhitaj huduma yetu tuwasiliane no.0766981308
tunakufuata ulipo DAR
 
Wadau hivi karibuni nimenunua ISUZU BIG HORN SUV ya mwaka 1998 imetembea 280,000 kms daah sasa nimeanza kutembelea inakula mafuta kama JINI MAHABA ya 1 ltr = 3kms yaani pamoja na kufungua vioo na kuweka FREE mara kibao imekuwa hatari. Najutaa kununua huu mgari na hela ya mkopo jamaa wa NMB ndo wameanza kukata mwezi huu
.Usifanye kosa kama langu mdau

Kwani mkuu hakuna namna ambayo mafundi wetu wanaweza kutengeneza ikawa inatumia mafuta kidogo?
 
Waone hawa.... nimekopi hii thread kutoka jukwaa kazi;




Yesterday
sisi ni vijana watatu kutoka toyota tz
,tunatengeneza
engine aina zote hasa za V8.Yeyote mwenye
kuhitaj huduma yetu tuwasiliane no.0766981308
tunakufuata ulipo DAR

Mkuu Lusungo ubarikiwe sana kwa msaada huu mkubwa, asante kiongozi
 
Waone hawa.... nimekopi hii thread kutoka jukwaa kazi;




Yesterday
sisi ni vijana watatu kutoka toyota tz
,tunatengeneza
engine aina zote hasa za V8.Yeyote mwenye
kuhitaj huduma yetu tuwasiliane no.0766981308
tunakufuata ulipo DAR

Nawapongeza wametumia fursa vizuri mno
 
UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?

Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !

Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katika barabara zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara – iwapo kila mmoja atazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao, isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.

Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati gani anakusimamisha uwapo barabarani.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kama atakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).

Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa. Ili kuepuka matatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:

Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo ya kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo kama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari:

Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani na kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang’anywa:

Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama:

Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatenda kosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe
:

Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakati unaendesha:
Ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi:

Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).

Kustahili kuwepo barabarani
:

Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwa ofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –usitoe rushwa na usipokee rushwa.

Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbuka kwamba ni mwongozo tu.

Kuna mtu aliniambia kwamba afisa wa polisi kwa mujibu wa sheria ni askari polisi mwenye cheo kuanzia koplo, ni sahihi hii?
 
Kuna mtu aliniambia kwamba afisa wa polisi kwa mujibu wa sheria ni askari polisi mwenye cheo kuanzia koplo, ni sahihi hii?

Nafikiri ni hivyo ila nijuavyo mimi ni kwamba si kila askari ana haki ya kusimamisha gari na kuanza kukagua kama ni ukaguzi wa kawaida au makosa ya barabarani
 
mi sikushauri ununue hyo maana bodi yake ni plastic kbisa ukimgusa mtu kidogo sana ni majanga mchina huyo ni heri nunua harrier iko vizur na haipishani bei sana na xtrail yani hii gar kwa kweli ni heri harrier ni nzur imetulia hata used inauzka.
Nashukuru mkuu kwa ushauri, vipi kuhusu harrier na freeland2 ipi iko njema zaidi
 
Nauliza km sheria inataka tulipe 20000 kama faini ya kosa moja kwanini tunatozwa 30000?
 
Back
Top Bottom