Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Bima za binafsi nyingi ziko vizuri msiba uko NIC na Zanzibar Insurance, hao ni majanga na usumbufu uko kwenye kupata docs toka jeshi la polisi kitengo cha barabarani pale ndio kuna rushwa iliyoota mizizi ya mbuyu

Polisi Tanzania kwa mizengwe na rushwa wamezidi aisee.
 
Wakuu mwenye uelewa na VW Golf tafadhali. Nipo kwenye mchakato wa kujichanga ili Mungu akipenda nivute hiyo kitu. Ushauri wa ujumla tafadhali
 
Za mchana wadau. Nimependa subaru forester sijajua ipi nzuri katika ubora wa injini. Pia tofauti ya ubora kati ya yenye turbo na isiyokuwa nayo. naombeni msaada
 
Hebu mpigie mtaalamu kwa namba hii,gari zangu ndiye ananitolea akupe total figure .Si lazima akutolee yeye ila ni vizuri ukapata bei tofauti tofauti ukachagua wewe,KUMBUKA kuna wahuni wanaongeza bei na siku unaletewa gari tairi zote zimebadilishwa zimepachikwa za kariakoo.0713777255
 
Kwa uzoefu wangu hasa gari za kijapan kwanza life time ya timing belt ni km laki 1, na mara nyingi inapozidi hapo hiyo taa huanza kuwaka na kuzima japo magari ya siku hizi yenye sensors nyingi check engine yaweza kuwaka kutokana na fault nyingine pia lakini inayohusika na engine

mkuu mshana jr ,mi nilifikiri kuna taa mbili, Nyekundu ya CHECK ENGINE na KIJANI imeandikwa TIMING BELT!
 
mkuu mshana jr ,mi nilifikiri kuna taa mbili, Nyekundu ya CHECK ENGINE na KIJANI imeandikwa TIMING BELT!

Hizo labda ni gari za kisasa ambazo zinatofautisha yaweza kuwa sawa
 
Jamn gari yangu leo imenizingua kwa kutokuwaka na nikaamua kuita watu wakanisukuma ila ilpowaka dashboard haioneshi yani ile mishale ya joto exclator mafuta na speed hazioneshi chochote na mpk dakika hii gari imezima nimepaki sijafika nyumbani
 
Naomba kujulishwa kuhusu S na B kwenya maana Hii gari ni staff gear naelewa P, R, N, na D. Sasa when and where to apply S & B.
 
Jamn gari yangu leo imenizingua kwa kutokuwaka na nikaamua kuita watu wakanisukuma ila ilpowaka dashboard haioneshi yani ile mishale ya joto exclator mafuta na speed hazioneshi chochote na mpk dakika hii gari imezima nimepaki sijafika nyumbani

Wiring hiyo kaka usijaribu tena kuiwasha
 
Za mchana wadau. Nimependa subaru forester sijajua ipi nzuri katika ubora wa injini. Pia tofauti ya ubora kati ya yenye turbo na isiyokuwa nayo. naombeni msaada

Iko poa, strong na performance yake ya engine ni nzuri, inategemea unataka nini kwenye gari
 
Hii gari haina cha uwani, fundi anasema clutch plates zitakuwa zinatatizo thus reverse inazingua. Naomba uzoefu wenu wadau. Toyota Sienta.
 
Wakuu mwenye uelewa na VW Golf tafadhali. Nipo kwenye mchakato wa kujichanga ili Mungu akipenda nivute hiyo kitu. Ushauri wa ujumla tafadhali

Mkuu, unahitaji VW Golf ya mwaka gani na vipi specs zake.

Gari bomba sana hizi na vijana wanazipenda.
 
naomba kuuliza jamani. eti kuna uhusiano kuwasha AC na ulaji wa mafuta kwenye gari?

Upo kwakuwa compressor inatumia nguvu ya engine hivyo unapowasha AC mzunguko wa engine huongezeka LAKINI ulaji wake ni kidogo sana
 
Ni gari ngumu na very economy endelea na mchakato
media

Volkswagen Golf 1.6 TDi 105 BlueMotion SE 5dr

Mwaka - 2010

Mafuta - Diesel

Ina mlango wa nyuma au Hatchback

Gear yake -Manual

Maili ilizoendeshwa -61119

Rangi yake ni Metallic Met Red,

Mengine ina- Cloth Trim, A/C, 16 inch alloy wheels, ABS brakes with Traction Control, Central Locking, Cruise Control, Electric Mirrors, Electric Windows (Front & Rear), Power-Steering, Radio & CD-player, Rear Head-Rests, 5 Door Hatchback, Air Conditioning. 5 seats,
media

media

Angalia dashboard yake.

Kama unavyoona gari hii inakula mafuta kiasi kidogo sana yaani 1.6 engine yake.
 
naomba kuuliza jamani. eti kuna uhusiano kuwasha AC na ulaji wa mafuta kwenye gari?

AC inatumia gas na mafuta pia ni gas hivyo kama unakwenda safari ndefu na unatumia AC basi mafuta yataisha haraka sana.

AC ni nzuri kutumia kwenye safari za mjini tu yaani safari fupi na unaposimama sehemu basi unazima AC na unafungua madirisha pia.

Kwa mfano huwezi kutoka DSM kwenda kibaha ukiwa umewasha AC, itabidi ufungue madirisha kidogo ili kuingiza hewa.

Kumbuka unatakiwa uifanyie service AC kila mwaka kuiweka katika hali nzuri ya ufanisi.

Ila mwisho wa siku ni suala la kutuna mfuko kama fwedha ipi hamna tabu wewe unatumia AC toka dar mpaka Morogoro au Tanga au Moshi.
 
Back
Top Bottom