Bima za binafsi nyingi ziko vizuri msiba uko NIC na Zanzibar Insurance, hao ni majanga na usumbufu uko kwenye kupata docs toka jeshi la polisi kitengo cha barabarani pale ndio kuna rushwa iliyoota mizizi ya mbuyu
Haina shida ni kuwa makini tu na matumizi, epuka kuoverload mizigo na abiria, rough ziepuke au nenda mwendo wa kinyonga, epuka madereva wengi
Agiza tu kaka hizo hazina shida landrover mbovu ni freelander hata comfortability ni zero
Kwa uzoefu wangu hasa gari za kijapan kwanza life time ya timing belt ni km laki 1, na mara nyingi inapozidi hapo hiyo taa huanza kuwaka na kuzima japo magari ya siku hizi yenye sensors nyingi check engine yaweza kuwaka kutokana na fault nyingine pia lakini inayohusika na engine
Jamn gari yangu leo imenizingua kwa kutokuwaka na nikaamua kuita watu wakanisukuma ila ilpowaka dashboard haioneshi yani ile mishale ya joto exclator mafuta na speed hazioneshi chochote na mpk dakika hii gari imezima nimepaki sijafika nyumbani
Za mchana wadau. Nimependa subaru forester sijajua ipi nzuri katika ubora wa injini. Pia tofauti ya ubora kati ya yenye turbo na isiyokuwa nayo. naombeni msaada
Wakuu mwenye uelewa na VW Golf tafadhali. Nipo kwenye mchakato wa kujichanga ili Mungu akipenda nivute hiyo kitu. Ushauri wa ujumla tafadhali
Ni gari ngumu na very economy endelea na mchakato
naomba kuuliza jamani. eti kuna uhusiano kuwasha AC na ulaji wa mafuta kwenye gari?