Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

  • Ndugu mshana jr nataka tukujua kama una gari/uliwahi kumiliki gari!
  • Nataka pia kufahamu tabia zako mtaani kwenu pindi uliponunua gari (Ruka swali hili kama hujawahi kumiliki)
  • Ni kwanini vijana wakiume(ke) waliozaliwa tukiwa kwenye mfumo wa vyama vingi wanawaza tu kumiliki magari wamalizapo shahada/diploma ama kupata ajira ya kwanza?
  • Ni kwanini jamii inadhani mtu anayemiliki gari(of which hata 5 K unanunua) ana maisha bora bila kimjini mjini ukiwa na 20 K huwezi kujenga labda uwe umepewa uwanja wa kujengea na baba/babu?
Horseshoe Arch kwanza nikwambie tu kwamba mimi ni mgonjwa wa magari, ninapenda magari na nimemaliki/ namiliki magari

Sina tabia za fujo mtaani na naheshimu mno usalama wengine na sheria pia kwa umri wangu huu siwezi kuwa limbukeni wa magari, mimi ni mfuatiliaji na mtunzaji pia

Kuhusu kumiliki gari badala ya kujenga nina maoni tofauti! Nyumba ya kupanga ya shilingi laki 3 kwa mwezi ni nyumba nzuri tu lakini hebu niambie je unaweza kukodi gari kwa laki tatu kwa mwezi?

Siku hizi gari ni ofisi gari ni usafiri wa kutengeneza michongo 'ya halali' na nk
 
Last edited by a moderator:
Boniface Nyange +254206977200
Joseph Kyalo +254721542679
Miriam Munywoki +254721490879 /+25420650555
Samuel mwema +254721795685
Hizo hapo ndugu akamwalikilo
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu kwenye ukurasa huu! Natafuta starter ya Benz ML 270 CDI Engine Diesel,

Nimekutumia no nyingi na hii pia chukua +254722734881
Hawa wanadeal na used na mpya, zile nyingine ni brand new
 
Wakuu kwema..??? Naona wadau wengi wanaomba jukwaa la magari, sasa wakati tunasubiri hilo jukwaa ngoja tuanze na uzi huu.

Kwa kuanzia naomba wale ndugu zangu wa Legacy,impreza,wrx,B4,forester,Pleo etc wajitokeze tubadirishane uzoefu na kuongeza undugu wetu, najua tayari tunateam zetu ila siyo mbaya pia tukiunda team nyingine hapa kwakua sisi sote tuna share teknolojia moja.

Kwa mfano ningependa kuzungumzia kuhusu spea, ni wazi kwamba spea zetu zinauzwa ghari sana lakini changamoto kubwa zaidi ni upatikanaji wa spea zenyewe, kwa mfano majuma mawili yaliyopita nilichochora(kupotea njia) kidogo, gari liliharibika kiasi. Nililazimika kubadirisha ile kitu wanaita wishbone, mziki ukaja kutafuta bumper, nilizunguka mji mzima kuanzia kariakoo mpaka kwa Zizu pale ila ikawa bila bila ikabidi ifanyike modification tu. Ila na uhakika kua kupitia jukwaa la magari ingekua rahisi sana kupata spea hizo.

Kwahiyo binafsi naunga mkono wazo la jukwaa letu, litatufaa sana. Najua mods pia wanaona hilo na huenda mipango na vikao vimeanza kufanywa kwaajili ya hii kitu.

Karibuni kwa mawazo yenu, sijafunguka vizuri sana nipo ktk foleni wakuu..0-60

Mnyenz PAScho Preta Invisible
 
Last edited by a moderator:
Kuna jamaa wana uzi wao wanaongelea SUV, Lakini nililazimika kuuvamia ule uzi katika kipengele cha speed, jamaa wamesifia sana magari yao ila nikawapa changamoto kati ya Subaru WRX 260KMP na hiyo VX V8 Kwenye lami iliyotulia safari fupi nani atakuwa wa kwanza?

Ila naona hawakunijibu vizuri kuridhisha nafsi yangu, sasa nafurahi sana kwa kuniita, ngoja na mimi niwavute huko waliko waje na vi sababu vyao vya kitaalam.
 
Hebu muite muheshimiwa Maxince Melo

Ohooo! Unaona utani wako? Umetishia kumuita amekuja kweli, mi simo, mwambie sasa kwamba tunalitaka jukwaa, maana Mwanaume haombi haki yake, ye anaichukua tu(natania) ila mimi simo.
Cc😡Maxence Melo.
 
Ohooo! Unaona utani wako? Umetishia kumuita amekuja kweli, mi simo, mwambie sasa kwamba tunalitaka jukwaa, maana Mwanaume haombi haki yake, ye anaichukua tu(natania) ila mimi simo.
Cc😡Maxence Melo.
RRONDO, Bulldog, Ukwaju
 
Last edited by a moderator:
Wakuu kwema..??? Naona wadau wengi wanaomba jukwaa la magari, sasa wakati tunasubiri hilo jukwaa ngoja tuanze na uzi huu.

Kwa kuanzia naomba wale ndugu zangu wa Legacy,impreza,wrx,B4,forester,Pleo etc wajitokeze tubadirishane uzoefu na kuongeza undugu wetu, najua tayari tunateam zetu ila siyo mbaya pia tukiunda team nyingine hapa kwakua sisi sote tuna share teknolojia moja.

Kwa mfano ningependa kuzungumzia kuhusu spea, ni wazi kwamba spea zetu zinauzwa ghari sana lakini changamoto kubwa zaidi ni upatikanaji wa spea zenyewe, kwa mfano majuma mawili yaliyopita nilichochora(kupotea njia) kidogo, gari liliharibika kiasi. Nililazimika kubadirisha ile kitu wanaita wishbone, mziki ukaja kutafuta bumper, nilizunguka mji mzima kuanzia kariakoo mpaka kwa Zizu pale ila ikawa bila bila ikabidi ifanyike modification tu. Ila na uhakika kua kupitia jukwaa la magari ingekua rahisi sana kupata spea hizo.

Kwahiyo binafsi naunga mkono wazo la jukwaa letu, litatufaa sana. Najua mods pia wanaona hilo na huenda mipango na vikao vimeanza kufanywa kwaajili ya hii kitu.

Karibuni kwa mawazo yenu, sijafunguka vizuri sana nipo ktk foleni wakuu..0-60

Mnyenz PAScho Preta Invisible

Ni kweli mkuu, spea za subaru ziko juu. Nadhani ni kwasababu feki hazijaingia sokoni.

Spea zinapatikana hapo Msimbazi karibu na bank ya DTB kwa Nyange.

Kwa forester, badilisha timing-belt kabla haijafika 100,000 km, tumia oil 15w40(multigrade oil) au Quartz 5000 ya Total, oil filter ya gearbox badilisha kila baada ya 100,000 km. Usitumie spea isiyokuwa ya subaru....usiwaamini sana wanaokuambia zinaingiliana na aina nyingine...za kuambiwa unachanganya na za kwako.
 
Ni kweli mkuu, spea za subaru ziko juu. Nadhani ni kwasababu feki hazijaingia sokoni.

Spea zinapatikana hapo Msimbazi karibu na bank ya DTB kwa Nyange.

Kwa forester, badilisha timing-belt kabla haijafika 100km, tumia oil 15w40(multigrade oil) au Quartz 5000 ya Total, oil filter ya gearbox badilisha baada ya 100km. Usitumie spea isiyokuwa ya subaru....usiwaamini sana wanaokuambia zinaingiliana na aina nyingine...za kuambiwa unachanganya na za kwako.

Hapo kwenye kubadili oil filter ya gearbox baada ya km 100 ni sahihi au ni typing error!?
 
Kwa forester, badilisha timing-belt kabla haijafika 100km, tumia oil 15w40(multigrade oil) au Quartz 5000 ya Total, oil filter ya gearbox badilisha baada ya 100km. Usitumie spea isiyokuwa ya subaru....usiwaamini sana wanaokuambia zinaingiliana na aina nyingine...za kuambiwa unachanganya na za kwako.
mshana jr hata mm naona kuna walakini katika hizo Mileage kwani nikitoka hapa Dodoma kuja Dar lazima niwe na Timming belt 8 ili niweze kurudi Dodoma 900km na kuifungua hiyo injini kwenye hizo cover sio mchezo bado Oil ya gear box
Oil ya injini km 5,000/= ni sahihi kabisa injini za kijapani zipo sawa labda katika gear-box ambazo za Auto ni kila unapobadili injini oil mara ya pili na yenyewe
Kawaida ya hizi injuni za Kijapan

Timming belt ni 100,000km
Gear box manual 100,000km
 
Last edited by a moderator:
Samahani wakuu, hivi ni sahihi kutembea na gari umewasha AC huku umempakia mtoto mchanga ili asipigwe na upepo wa nje? kama si sahihi nini kifanyike pale mtu anaposafiri na mtoto mchanga?
 
Samahani wakuu, hivi ni sahihi kutembea na gari umewasha AC huku umempakia mtoto mchanga ili asipigwe na upepo wa nje? kama si sahihi nini kifanyike pale mtu anaposafiri na mtoto mchanga?

Si sahihi kabisa kifua na mapafu ya mtoto mdogo hayajakuwa na uwezo wa kuhimili baridi ya AC! Cha kufanya kama unasafiri naye kwanza hakikisha umemvisha jacket zito la kuzuia upepo kisha fungua vioo kidogo kuruhusu hewa kuingia
 
Shukrani sana mkuu
 
Mie nnaomba maelezo yahusuyo POWER TILLERS, nipo obsessed nayo kwa Sana Tu.
Nina ihitaji kwaajili ya kilimo cha mpunga huku Kyela.

Bei yake Na matumizi mf services nk.
Nawasilisha.
 
Big up kwako mshana jr kwa kuanzisha thread hii nzuri. Nitqmleta mke wangu aje asomee driving hapa???

Nawezaje kuagiza gari kutoka nje bila hofu ya kutapeliwa na je nchanganuo wa ushuru ukoje gari ikishafika nchini wanabodi naomba mnijuze tafadhali
 
Back
Top Bottom