Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Msaada plse wa hizi gari Nissan X-Trail na Ford Escape. Ipi kati ya hizi mojawapo ni nzuri mahsusi kwenye fuel consumption, spare parts na upatikanaji wa mafundi kwa services. Natanguliza shukrani wana-jf.

Zote zaweza kuwa nzuri lakini kwa masuala ya spare ni afadhali X-trail
 
Mimi nina gari aina ya carina Si, baadhi ya watu wamekuwa wakinichanganya kwamba O/D ikiwa imedisplay O/D OFF ndo iko ON na ikiwa haijadisplay ndo iko off hapa ndo wananichanganya kabisa, naomba msaada mkuu
 
Wajapan walikosea sana hapo
 
Mimi nina gari aina ya carina Si, baadhi ya watu wamekuwa wakinichanganya kwamba O/D ikiwa imedisplay O/D OFF ndo iko ON na ikiwa haijadisplay ndo iko off hapa ndo wananichanganya kabisa, naomba msaada mkuu

Unajichanganya mwenyewe mkuu. display inakwambia O/D OFF Wewe bado unataka ushauri wa mtu mwingine. Tatizo nini hapo?
 
Mkuu Mshana, embu nisaidie kitu kimoja. Nini dalili za kuchoka kwa ABS kwenye gx 110?
 
Achana na magari wewe lete hela tupige monde maeneo yetu. Au unataka kuuza Prado ile

Afu acha umbea Shark.....naona roho inakuuma sana nikiwa nae.
Anyway....nataka kuuza Prado lile, ninunue M-VX, mtakoma mkiniona MK au Tw.
 
Last edited by a moderator:
Naomba kufahamu tofauti iliyopo kati ya LandCruiser TX na VX, ipi nzuri kwa kuendesha hasa kama mimi ni mwanamke....
Pia ningefahamu bei, maana budget yangu ni 70Mil.

Landcruiser tx ni prado,nyingi ni cc 2700,ingawa kuna cc 3400 ,zote ni petrol,kuna zenye engine ya diesel ya kz pia,!landcruiser vx ni baba lao,cc 4700 petrol engine na 4200 diesel engine,chaguo ni lako
 
Wakuu mimi swala langu ni kuhusu rotary engines. Hasa kwenye gari aina ya mazda rx8 inatumia mfumo huu wa engine.. Ni engine isiyotumia pistons ila inatumia rotors.

Kwa mwenye uzoefu wa aina hii ya engines, spare zake upatikanaji wake ukoje, matatizo ya engines hizi ni yapi
 
Samahani kama swali liliwahi kuulizwa. ila nuliza kama ukibadili engine ya freelander na kuweka ya rav 4 (3s) gari itapiga mzigo vizuri?
 
Mkuu Mshana, embu nisaidie kitu kimoja. Nini dalili za kuchoka kwa ABS kwenye gx 110?

Kwanza lazima uelewe kuwa Gx 110 inaingia kwenye kundi la magari ya kisasa zaidi ambapo sensors ndio zinacontrol karibia kila kitu magari mengine mpaka upepo ukipungua inakujulisha
Sasa kwa suala lako la ABS halina tofauti kwakuwa kila wakati taa ya ABS kwenye dashboard itakuwa inawaka kukuashiria kuwa kuna shida
 
Wakuu mimi swala langu ni kuhusu rotary engines. Hasa kwenye gari aina ya mazda rx8 inatumia mfumo huu wa engine.. Ni engine isiyotumia pistons ila inatumia rotors.

Kwa mwenye uzoefu wa aina hii ya engines, spare zake upatikanaji wake ukoje, matatizo ya engines hizi ni yapi

Naamini ulimaanisha routers! Duka moja la spare za Mazda la siku nyingi sana liko opposite na Tabata dampo along Mandela road hapo utapata ushauri spare na mafundi
 
Samahani kama swali liliwahi kuulizwa. ila nuliza kama ukibadili engine ya freelander na kuweka ya rav 4 (3s) gari itapiga mzigo vizuri?

Hiyo inaitwa weird modification kwakuwa freelander ni gari za UK wakati Rav 4 ni za kijapani hivyo zina mifumo miwili tofauti sana lakini ukipata fundi mzuri kibongobongo haina shida kwakuwa kuna mavogue na mabenz mengi tu mitaani yamechakachuliwa na engine za Toyota na zinapiga mzigo vizuri tu!

Sanasana tofauti utanotice kwenye mngurumo
 
Naamini ulimaanisha routers! Duka moja la spare za Mazda la siku nyingi sana liko opposite na Tabata dampo along Mandela road hapo utapata ushauri spare na mafundi

Hapana mkuu ni rotors...hizi engines huwa hazitumii pistons.. Huwa zinatumia rotors za pembe tatu...engines hizi huitwa rotary engines au wenkel engines.

Kwa anaejua shida zake pamoja na uimara wake na upatikanaji wa spare tafadhali atujuze.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi lakini umejaribu kucheki hapo tabata dampo!?
 
Hapana. Bado sijaiagiza hii gari. Ila nimeiangalia kwenye mtandao nimetokea kuipenda. Ila kabla sijafanya uwamuzi nadhani itakuwa vyema kujua wadau wanazizungumziaje aina hii ya engines.
 
Aina hii ya engine sidhani kama tuna professional fundis hapa kwetu kama una gari ya ziada waweza agiza hiyo ili usikwame likitokea tatizo
 
Mkuu toa ufsfanuzi kwa manufaa ya wengi hii kitu inachanganya wengi sana kwani nnapo press O/D kwa maana ya kwamba in a display o/d off kwenye dushboard ndo apo speed inabadilika ikiashilia extra power sasa mini ukwel kuhusu display ya o/d off ufafanuz tafadhal tusije haribu Magari ambayo yanatugarimu matengenezo
 
Back
Top Bottom