Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mie nnaomba maelezo yahusuyo POWER TILLERS, nipo obsessed nayo kwa Sana Tu.
Nina ihitaji kwaajili ya kilimo cha mpunga huku Kyela.

Bei yake Na matumizi mf services nk.
Nawasilisha.

Mmh mi hizo bilabila
 
Nawezaje kuagiza gari kutoka nje bila hofu ya kutapeliwa na je nchanganuo wa ushuru ukoje gari ikishafika nchini wanabodi naomba mnijuze tafadhali

Jihadhari mno chances za kutapeliwa zipo pitia post zangu za nyuma
 
Si sahihi kabisa kifua na mapafu ya mtoto mdogo hayajakuwa na uwezo wa kuhimili baridi ya AC! Cha kufanya kama unasafiri naye kwanza hakikisha umemvisha jacket zito la kuzuia upepo kisha fungua vioo kidogo kuruhusu hewa kuingia

acheni kudanganya watu, ac haina madhara kwa mtoto, nenda aghakhan utakuta mtoto kalazwa na kwashiwa ac, kufungua vioo vya Gari ndo mbaya zaidi maana jiulize Kama gari linachafuka kwa moshi na vumbi je wewe?

upepo wa safirini ni mbaya kuliko hiyo ac, kwanza hata mtu mzima inakunyima comfort

ulaya na dubai kuna watoto toka anazaliwa mpaka utu uzima no full kipupwe tu, mf Dubai wakikusikia unasema ac ina madhara nahic utapigwa risasi hahahaha
 
acheni kudanganya watu, ac haina madhara kwa mtoto, nenda aghakhan utakuta mtoto kalazwa na kwashiwa ac, kufungua vioo vya Gari ndo mbaya zaidi maana jiulize Kama gari linachafuka kwa moshi na vumbi je wewe?

upepo wa safirini ni mbaya kuliko hiyo ac, kwanza hata mtu mzima inakunyima comfort

ulaya na dubai kuna watoto toka anazaliwa mpaka utu uzima no full kipupwe tu, mf Dubai wakikusikia unasema ac ina madhara nahic utapigwa risasi hahahaha

Nimezungumzia kwa uzoefu wangu sijadanganya mtu lakini bado nasimamia kusema Ac si nzuri ndugu yangu si kwa mtoto tu hata kwa mtu mzima! Kuhusu vioo nimesema unafungua kidogo
 
Pia asilimia kubwa hawajui kuwa matairi ya gari huwa yaisha muda toka kutengenezwa kwake, yanakaa muda usiozidi miaka mitano kutambua tairi limetengenezwa lini kuna namba zinakuwa nne pembeni ya tairi, mbili za mwanzo ni wiki iliyotengenezwa katika mwaka na mbili za mwisho ni mwaka mfano 2314 tairi imetengenezwa wiki ya 23 mwaka 2014 tuzingatie hili kuepuka kupata pancha au tairi kupasuka likiwa jipya
 
Naulizia toyota mark two hii mpya za sasa hivi yaani kisasa toleo jpya
 
Nitapata wapi mafundi wa ku overhaul engine ya mazda titan? ikiwa ni pamoja nakupata spare zake.
 
Wadau naomba mtu mwenye ujuzi wa marketing anisaidie hapa. Je unapoona bei ya gari FOB price ndo nini? Na je gari ya kawaida(cheap) ya kutembelea unaweza pata kwa dolla ngapi?
 
FOB price ina maana kwamba muuzaji mf: kutoka China atahusika na gari yako kutoka anapouza mpk port ya China. Baada ya hapo cost zote kuanzia kupakia, mpaka kuitoa bandarini (port of destination) zinakuwa za kwako na risk zote zitakazoipata hiyo gari zitakuwa juu ya mnunuzi.

Tofauti na ukikuta imeandikwa CIF price ambapo gari mpk inafika destination inakuwa chini ya seller na cost unazirudisha baada ya kuiona gari na kuikagua. Nadhani kidogo utakuwa umepata kaulewa apo
 
FOB price ina maana kwamba muuzaji mf: kutoka China atahusika na gari yako kutoka anapouza mpk port ya China. Baada ya hapo cost zote kuanzia kupakia, mpaka kuitoa bandarini (port of destination) zinakuwa za kwako na risk zote zitakazoipata hiyo gari zitakuwa juu ya mnunuzi. Tofauti na ukikuta imeandikwa CIF price ambapo gari mpk inafika destination inakuwa chini ya seller na cost unazirudisha baada ya kuiona gari na kuikagua. Nadhani kidogo utakuwa umepata kaulewa apo
Nashukuru mkuu nimekupata kabisa!!!
 
Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa

Kaka nimekuwa nikitumia Corolla Van kwa barabara za vumbi muda mrefu tu.Gari inahimili ingawa haina mvuto mzuri kwa muonekano wake ila kwa barabara mbovu gari haitaabiki.

Ni gari nzuri tu kwa mtu wa kipato cha chini maana spare parts zinapatikana tena kwa bei chee..ulaji wa mafuta mzuri ni 14 km/ litre.

Engine zipo 5A, 4E, 5E mpaka 2E ya Cabulator .Performance zake zinakaribiana tu. Wataalamu zaidi watapita kusema.
 
Wanajamii naomba msaada wenu nahitaji kununua gari na nimeipenda sana Toyota Corolla Fielder. Bararbara ninayotumia kila siku ni ya vumbi kama km 6 na pia huwa naenda vijijini ambako miundo mbinu ni tatizo.

Naomba kujuzwa kwa mazingira kama hayo mnyama huyo ni sahihi kuwa naye au si mahala pake maana huwa natumia corolla van na haina shida ila nimependa sana muonekano wa Fielder. Wanajamvi msaada wenu jamani.
 
Wanajamii naomba msaada wenu nahitaji kununua gari na nimeipenda sana Toyota Corolla Fielder. Bararbara ninayotumia kila siku ni ya vumbi kama km 6 na pia huwa naenda vijijini ambako miundo mbinu ni tatizo.Naomba kujuzwa kwa mazingira kama hayo mnyama huyo ni sahihi kuwa naye au si mahala pake maana huwa natumia corolla van na haina shida ila nimependa sana muonekano wa Fielder. Wanajamvi msaada wenu jamani.

Fielder ni gari ngumu na kwakuwa tayari unatumia corrola van basi fielder itakufaa sana kwa kila kitu
 
Na ni vipi kuhusu suzuki vitara kwenye njia ya vumbi?
 
Na ni vipi kuhusu suzuki vitara kwenye njia ya vumbi?

Suzuki haiwezi kuhimiri taabu za mara kama brand za corolla hasa kwa mtu wa kipato cha chini unayetumia barabara za vumbi mara kwa mara.Suzuki vitara kuna jamaa yangu namuona anayo inamtesa sana.

Nafikiri kutizama vitara kwa barabara za vumbi Toyota mark 2 GR itakuwa ni imara zaidi ila nita opt kwa Fielder kulingana na ushauri wa mkuu Mshana.
 
Back
Top Bottom