Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Nina gari gx 100,tatizo ni fupi sana. Nikipita ktk tuta barabarani au rough roads chesis huwa inagonga sana. Je kuna uwezekano wa kuiongeza na je hukuna side effects yoyote kwa kufanya hivyo.?!
 
Badili tyres tu uweke kubwa kiasi ambazo hazitazidi vipimo husika lakini, usijaribu kunyanyua kwa namna yoyote ile kwa kuweka Spencer utaharibu mwonekano wa gari na kupoteza balance ukiwa 80+speed
 
Recomended tyre specification ni 165/65R15. Sasa nitumie ipi mkuu mshana jr.?!

Nafikiri hizo ni zile za sports rims, waweza chukua inayofuatia na si zaidi ya hapo, la sivyo ulaji wa mafuta utaongezeka
 
asanteni kwa ushauri wa kubadilisha engine but haina implications kwenye systems nyingine za gari? kodi (TRA) na polisi? maana lengo la kununua bighorn si kuja tena kununua na Engine ili kubadilisha natamani nikinunua kitu kiwe COMPLETE, si mara mlango wa RAV 4, Engine ya PRADO, siti za PASSO, RIM za PAJERO hilo si lengo la mimi kununua gari jamani
 
Nimetokea kuzipenda hizi gari. Naomba msaada wenu kwa anaezijua ipi ni bora zaidi kwa nyanja zote.
 
Nina tatizo kidogo,nikiendesha gari mguu mmoja wa nyuma kushoto unapiga kelele sana kwenye rough road then kuna kipind inasikika harufu kama ya tair inaungua,tatizo litakuwa nini?
 
Kuchoka kwa bushes, springs, shockups pia inawezekana breakpads zimekufa kabisa halafu hilo sio tatizo dogo chilonge ukiendesha 80+ halafu ushike break ndio utaona ukubwa wa tatizo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Bighorn ni kimeo sana kwenye masuala ya sensors,
Mbili si kweli kwamba ukiwa safarini na bighorn hakuna gari ya kukupita !! baba kuna gari zinafungua kuliko hata hiyo V8 unayoiogopa.
Pia Bighorn ina tatizo la kutotulia barabarani hasa ukishafika 120+.
Bila kusahau hii gari ni ngumu kuuzika sio kidogo.
 
Kuchoka kwa bushes, springs, shockups pia inawezekana breakpads zimekufa kabisa halafu hilo sio tatizo dogo chilonge ukiendesha 80+ halafu ushike break ndio utaona ukubwa wa tatizo

Mkuu Mshana nina gari honda crv nataka kuiweka spancer ipande juu kidogo je juna tatizo??kwasasa inatumia lita moja km.11 nimetoka juzi moshi to dom,ni RD1 ya 1996, ntashukru kupata ufafanuzi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mshana nina gari honda crv nataka kuiweka spancer ipande juu kidogo je juna tatizo??kwasasa inatumia lita moja km.11 nimetoka juzi moshi to dom,ni RD1 ya 1996, ntashukru kupata ufafanuzi.

Hapana kabisa hiyo ni modification itakayokuletea matatizo mengi sikushauri kabisa
 
Wadau hivi karibuni nimenunua ISUZU BIG HORN SUV ya mwaka 1998 imetembea 280,000 kms daah sasa nimeanza kutembelea inakula mafuta kama JINI MAHABA ya 1 ltr = 3kms yaani pamoja na kufungua vioo na kuweka FREE mara kibao imekuwa hatari. Najutaa kununua huu mgari na hela ya mkopo jamaa wa NMB ndo wameanza kukata mwezi huu
.Usifanye kosa kama langu mdau

Duh nimecheka ingawa sio mazuri
 
Nina gari gx 100,tatizo ni fupi sana. Nikipita ktk tuta barabarani au rough roads chesis huwa inagonga sana. Je kuna uwezekano wa kuiongeza na je hukuna side effects yoyote kwa kufanya hivyo.?!

Next timw nunua gari according to ur routes mkuu, kuinua gari haishauriwi kabisa na usijaribu kwanza inapoteza shoo, pili unaforce G (centre of gravity) kuwa juu.
 
Mkuu nimetoka tanga to dsm na kirudi na passo ila tairi moja ya nyuma ni kale ka spar je kunamadhara yakukatumia?pia hiki kigari kinakimbia sijawahi kuona japo kana piston 3 yaani sijapitwa na gari yeyote mpaka nafika mpaka watu wanauliza nimefunga engine yanini?na kwenye mafuta nilijua kabovu hakali kabisa from dar to tanga lita 16 na mpaka sasa hivi natembelea bado wese lipo
 
Hahaha mkuu passo haijapitwa na gari yoyote njian labda ulikua unakutana na suzuki samurai n.k lakini hapo siwezi kuamini kabisaa
 
Next timw nunua gari according to ur routes mkuu, kuinua gari haishauriwi kabisa na usijaribu kwanza inapoteza shoo, pili unaforce G (centre of gravity) kuwa juu.

Ahsante mkuu. Sasa hivi moja ya vigezo nitakavyokuwa naviangalia ni urefu wa gari toka chini. Mana mwanzo wkt wa kulinunua nilipewa ushauri eti litanyanyuliwa..
 
Back
Top Bottom