Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Poleni kwa majukumu wakuu,naomba uzoefu wenu juu ya gari ya kutembelea aina ya Isuzu Wizard,bimaana ustahamilivu wake ktk barabara za vumbi,ulaji wa mafuta per km na upatikana na bei za vipuli.
Natanguliza shukrani kwenu.
 
Poleni kwa majukumu wakuu,naomba uzoefu wenu juu ya gari ya kutembelea aina ya Isuzu Wizard,bimaana ustahamilivu wake ktk barabara za vumbi,ulaji wa mafuta per km na upatikana na bei za vipuli.
Natanguliza shukrani kwenu.
bysange kwa uzoefu Wangu binafsi hizo gari zinawatesa wengi ndio maana zimeshindwa kabisa kukubalika hapa nchini
Kikubwa kinacholalamikiwa ni uimara vipuri na ulaji wa mafuta... sina uhakika na haya lakini ndivyo inayosemwa
 
Naomba kujua hii gari suzuki escudo old model ya 1490cc,naomba kujua ni kwanini watu wengi hawazipendi siku hizi?
 
Kwa Kua unahitaji gari ya kuitumia pamoja na Familia angalia Ile yenye room ndani, ambayo ni comfortable... Raum itakufaa zaidi. Lakini IST ni nzuri pia na haito kusumbua pindi ukiamua kuachana nayo.
Raum kwa yard za hapa nchini inaenda kwa bei gani!???
 
Habari zenu wana jamvi
Nina gari toyota Cami na imekuwa na matatizo yafuatayo.... meno ya rejetor yalipasuka baadhi wakati wa kusafishwa ikawa inatoa maji kidogo sana na kufanya gari kuchemka ila nikawa naongeza maji kwa muda wa 2 weeks hivi nikabadili rejetor ikawa haichemki tena.
Baada ya siku kadhaa ikaanza kutetemeka hasa nikiwa kwenye foleni garage nikaambiwa tubadili plugs nikabadili zote 4 ikatulia kwa siku 1 tu ikaanza kutetemeka tena na general performance ikashuka.
Ikabidi nikaiscan inshort nikaambiwa engine compression imeshuka katika cylinder 1 ilisoma 8 na zingine 3 ikasoma 10 bt alivyorudia ikapanda kidogo kwenda 9. Sasa kilichonimaliza nguvu hadi kukimbilia humu ni kuambiwa engine imekufa nijiandae kununua nyingine. Kwa pale sijui alifanya nn ila gari iliacha kutetemeka tena. Now ni wk imepita ila naona dalili za kuanza kutetemeka tena kwa mbali...
Please mwenye ushauri wa nini cha kufanya kabla sijazunguka sana ama wapi kuna watu wa uhakika kuniangalizia tatizo and if possible kumaliza ili tatizo mafundi wengi naona wanazingua coz service nilikuwa nafanya bila kupitisha km.
 
Msaada katika usomaji wa consumption ya mafuta katika Harrier cc 2400
 

Attachments

  • 1470412331821.jpg
    1470412331821.jpg
    29 KB · Views: 112
Mkuu mimi gari yangu ni RAUM toka juzi nikifunga milango ya kushoto kwenye dash board inaonyesha milango ipo wazi nimepeleka kwa mafundi kama watatu wameshindwa Sijui tatizo litakuwa nini
 
Habari wadau! Wapi nitapata hydrolic genuine aina ya nisssan cvt fluid ns-2. Msaada tafadhali nipo dar.
 
Kwa uzoefu wangu kama unasafiri safari ndefu ni vizur over drive kuwa On hii itakusaidia gari kukimbia zaidi kwani ikiwa Off halaf unasafir safari ndefu utaichosha injini kwani itakuwa inadai gear nyingne wakati gearbox haijapewa nafasi ya kubadili, pia hiyo itachangia gari kutumia mafuta mengi lakn ikiwa On itarahisisha gari kukimbia zaidi na kubadili. Kumbuka unashauriwa kabla ya kuo-overtake gari unatakiwa kuiweka Off ili kuipa gari nguvu zaidi.
Samahan mkuu naomba kujua OD inakuwa on kipind kipi? ni pale dashboard inapoonesha neno OD au ni pale dashboard inapokuwa haioneshi neno hilo. Msaada wakuu
 
Samahan mkuu naomba kujua OD inakuwa on kipind kipi? ni pale dashboard inapoonesha neno OD au ni pale dashboard inapokuwa haioneshi neno hilo. Msaada wakuu
Inapokuwa haionyeshi kitu
 
Wakuu taa ya alarm ya ABS ikiwaka inamaanisha nini kwenye Gari?
 
Back
Top Bottom