Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hii Gari nzuri Sana iko poa kuanzia ndani ina seat 7 hvyo Kwa nafasi ya ndani ni nzuri na kubwa inatulia barabarani Kwa sababu ni nzito na ni Pana kwenye swala la ajali labda mechanical failure na uzembe tu Ila iko poa Sana Kwa ubaya mi nazani labda ni kwasababu wameinyima spare tyre tu japo wameiwekea kit ambayo ni full ikisumbua wameiwekea compressor ya kujazia tyre upepo ambayo utachomeka ndani ya Gari na tyre itajaa wameweka na dawa ya kuziba sehem iliyo pasuka au kutoboka kwenye hyo tyre Mimi ni mwaka wa pili na nusu sasa sijawahi ipeleka Kwa fundi labda kubadilisha oil ni Gari ngumu kama unataka kununua nunua chap maana zinapanda Sana bei Kwa sasa na zimeingia Kwa wingi sasa hivi
Mzee sorry naomba unijuze uzuri naubaya wa hii gari maana nahitaji kuichukua
 
Wakuu mambo vipi, hivi kuna spray yeyote naweza pata kwa ajili ya gari nyeusi au silver kutokana na mikwaruzo midogo midogo pembeni,
 
UFAHAMU KWA WENYE MAGARI;
Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne (4) tu toka yatengenezwe (sio toka uyafunge kwenye gari yako).
Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (2603) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.
Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. kwa mfano 2603 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au 2699 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.
KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.
Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi kama ifuatavyo
CODE SPIDI
F=============80
G=============90
J==============100
K==============110
L==============120
M==============130
N==============140
P==============150
Q==============160
R==============170
S==============180
T==============190
H==============200
Huandikwa hivi
280/R/70/13/150/S

View attachment 317580
280/R/70/13/150/S mbona hizi alama hujazitolea ufafanuzi mana hapo naona kuna herufi mbili R na S ipi inaonyesha speed
 
Nina gari Toyota Townace Van cc 1980 ikiwa na gia AUTOMATIC. Ni la mwaka 2005.
Sasa ina tatizo la kubadilisha gia.
Ukianza safari, inachelewa kubadili kuingiza gia namba mbili na gia zinazofuata.
Je inawezekana kurekebishwa?
Iwapo haiwezekani, nifanyeje?
 
Kiongozi

Mimi sio mjuzi sana wa magari ila kutokubadilisha gia husababishwa na vitu kadhaa; Moja wapo ni ile oil nyekundu maarufu kama gia box oil. angalia kama ipo levo sawa (kama sio sawa ongeza), na kama umeibadilisha hivi karibuni.
Hizi oil za kawaida za gia box hushauriwa ukibadilisha engine oil mara ya tatu umwage na oil ya gear box.
Kama oil ipo sawa na Orginal na haijakaa muda mrefu; tafuta fundi mzuri wa Gear box, inatengenezeka vizuri tu suala ni kupata fundi mzuri sio hawa wa kubahatisha watakudanganya eti gia box haitengenezeki kitu ambacho sio kweli (hawana ujuzi)
Lakini pia Kama umebadili timing chain ndio tatizo lika anza, anzia hapo...
 
Transmission issues hizi bwana sisi ndo huwa chanzo

Kwanza check transmission fluid yako ipo level sahihi? Kama ipo chini basi ongeza uangalie je kuna mabadiliko?

Na je huwa una badili transmission fluid (hydraulic fluid ya giabox) kila baada ya muda gani na je hii fluid uliyonayo muda ina muda gani tangu umefanya service? Kama ni muda mrefu umepita bila kuchange na imeanza kubarika rangi kua brown badala ya red, basi weka hydraulic fluid nyingine(recommend by your manufacturer na sio universal fluids)

Je watumia hydraulic fluid (transmission fluid) original (iliyo pendekezwa na mtengeneza gari?) Au ndo mambo yakutumia lubex au oil za Castrol mara total?
 
Asante sana.
Oil iko kipimo sahihi na bado ni mpya.
Tangu nimebadili haijazidi km.100.
Nitazingatia ushauri wako.
 
Transmission issues hizi bwana sisi ndo huwa chanzo

Kwanza check transmission fluid yako ipo level sahihi? Kama ipo chini basi ongeza uangalie je kuna mabadiliko?

Na je huwa una badili transmission fluid (hydraulic fluid ya giabox) kila baada ya muda gani na je hii fluid uliyonayo muda ina muda gani tangu umefanya service? Kama ni muda mrefu umepita bila kuchange na imeanza kubarika rangi kua brown badala ya red, basi weka hydraulic fluid nyingine(recommend by your manufacturer na sio universal fluids)

Je watumia hydraulic fluid (transmission fluid) original (iliyo pendekezwa na mtengeneza gari?) Au ndo mambo yakutumia lubex au oil za Castrol mara total?
Oil iko kipimo sahihi.
Nimekuwa nikibadili kila baada ya km.9,000 na haizidi 12,000.
Nimekuwa natumia iliyoshauriwa.
 
Swali Kwa wazoefu barabarani. Ikiwa ndio naingia barabarani Kwa mara ya kwanza. Na sipendi niguswe au niguse gari Ingine...ni nini cha kuzingatia.
 
TAHADHARI KWA WANAONUNUA MAGARI: Kabla ya kununua gari ulilochagua, iwe show room au kwa mtu mwengine yeyote hakikisha kabla ya kufanya malipo chukua nambari ya chassis ya gari hilo na uwasiliane na ofisi ya Interpol iliyopo ghorofa ya saba Jengo la Makao Makuu ya Polisi mtaa wa Ghana mkabala na jengo la Posts ili waangalie kwenye system ya Interpol iwapo gari hilo halijawahi kusajiliwa kuwa ni la wizi miongoni mwa nchi zaidi wanachama wa Interpol duniani. Bila kupata uhakika kutoka interpol kuna hatari ukanunua gari la wizi na ukajikuta unaliacha mikononi mwa polisi pindi ukikamatwa nalo wakati wa operesheni za interpol za kukamata magari ya wizi miongoni mwa nchi wanachama zinazofanyika kila Mwaka.
Je madalali wanaulizaga au wanajua kuwa mteja ataenda? Maana watakuwa madalali wakukamatisha magari ya wizi..

Ila imekaa vzr sana.
 
Faida na Hasara za kuwa na Gari yenye engine ya 1KR cc 900 na 1NR 1320cc Vitz New Model.

Habari za mida Ndugu zangu wa Jf.!
Naomba ushauri kutoka kwenu wazoefu wa Magari hasa kwa hizi gari ndogo Toyota Vitz New Model.
Naomba kujuzwa maana huwa naziona tu zikiandikwa Vitz jewela, Vitz U, Vitz Smile, Vitz Ciel, Vitz F, Je hizi tofaut yake ni nin na ipi sasa ni nzuri kwa matumiz ya kawaida mizunguko ya mjin na Faida na matatzo yake makubwa ni yepi..?
Asanteni Ndugu zangu.
 
TAHADHARI KWA WANAONUNUA MAGARI: Kabla ya kununua gari ulilochagua, iwe show room au kwa mtu mwengine yeyote hakikisha kabla ya kufanya malipo chukua nambari ya chassis ya gari hilo na uwasiliane na ofisi ya Interpol iliyopo ghorofa ya saba Jengo la Makao Makuu ya Polisi mtaa wa Ghana mkabala na jengo la Posts ili waangalie kwenye system ya Interpol iwapo gari hilo halijawahi kusajiliwa kuwa ni la wizi miongoni mwa nchi zaidi wanachama wa Interpol duniani. Bila kupata uhakika kutoka interpol kuna hatari ukanunua gari la wizi na ukajikuta unaliacha mikononi mwa polisi pindi ukikamatwa nalo wakati wa operesheni za interpol za kukamata magari ya wizi miongoni mwa nchi wanachama zinazofanyika kila Mwaka.
Hii ofisi IPO bado jengo tajwa??
 
Ntaka ninunue gari mkononi nitajuaje kama halijafunguliwa gearbox. Ni mambo yepi muhimu nizingatie. Nashukuru
Kwakifupi kwanza lazima ujiridhishe kuwa inatembea km ngapi kwa lt 1
Ulaji wa mafuta inategemea na vitu vingi ikiwemo hiyo ya 4wd.kama gari imetemgenezwa ni full time 4wd huna njia yakufanya usidanganyike kugusa gear box maana utaenda kununua mpya
Kuhusu guarantee kwa used car hakuna kumbuka magari haya yamekwisha tumika sio mapya
 
Mshana Jr,asante kwa thread hii.Swali langu ni je ntajuaje kuwa gari inakula Oili kuliko kawaida yake? Ishara za gari kula oil ni zipi? Asante.
 
Mshana Jr,asante kwa thread hii.Swali langu ni je ntajuaje kuwa gari inakula Oili kuliko kawaida yake? Ishara za gari kula oil ni zipi? Asante.
Gari haitakiwi kula oil kabisa, ni service to service unamwaga inawekwa nyingine. Ikipungua basi kuna shida labda leakage au piston rings zimechoka.
Hakikisha fundi unayempa kufanya service asiweke oil kupita mark ya maximum, kwa hili mafundi wetu hawako makini kabisa na ndio moja ya chanzo cha leakages za oil na ikiwezekana isiguse hiyo mark ya max.
Vilevile kwa coolant ya rejeta, gear oil haitakiwi kupungua hata tone.
 
UMUHIMU WA KUTUMIA GIA KUBWA MAENEO YENYE MITEREMKO MIKALI NA KONA

Faida za GIA kubwa unapoteremka mlima mkali ni kuwa zinafanya gari iwe nzito,sio uzito wa tonnage bali uzito wa kutembea au ku move.

GIA kubwa inasaidia gari kuwa katika slow motion hii ina maana unaweza hata kutumia exhaust brakes tu badala ya foot brake. Lakini faida nyingine ya kutumia GIA kubwa wakati wa kuteremka mlima ni kuwa gari inapokuwa kwenye gia kubwa hufua au kuzalisha upepo mwingi sana kwani mzunguko wa injini unakuwa mkubwa ukilinganisha na inapokuwa kwenye gia ndogo.

Sote tunajua kuwa upepo unahusika sana kwenye matumizi ya breki,iwe exhaust brake au foot brake upepo ni muhimu sana. Lakini pia upepo husaidia uingizaji wa GIA ki rahisi.

Sasa basi nina wasiwasi kinachotokea huko Mbeya na hata mahali pengine kuwa dereva anajaribu kushuka mlima kwa kutegemea sana foot brake huku gari ikiwa kwenye gia ndogo na matokeo yake akigusa gusa BREKI upepo unapungua kwenye mitungi na kwa vile gari au injini inakuwa nyepesi basi inakuwa haifui upepo wa kutosha.

Kumbuka upepo huo ndiyo unasaidi ubadilishaji wa GIA kirahisi na ni upepo huo huo ndiyo unatumika kwenye BREKI, matokeo yake unashindwa ku change down kwa wakati ili gari ipunguze kasi. Unashindwa kupata BREKI vizuri. Mwisho wa siku gari inakuwa free na kudongoloka kisha kusababisha ajali.

Nina imani kabisa kuwa kama utaweza kuweka GIA kubwa na sahihi mwanzo wa mlima unaweza kumaliza mlima bila kugusa foot brakes na hata ukigusa basi kwa kiasi kidogo.

Tumia GIA kubwa kama kisaidizi kikubwa cha breki pindi unaposhuka au kutetemka mlima. Lakini pia jitahidi kuendesha mwendo ambao angalau unaweza kulimudu gari lako in case of anything. Tusiendeshe kwa hisia au utashi bali tuendeshe kwa vigezo kadri iwezekanavyo.

Punguza vituo tembea mwendo mzuri na mdogo ufike salama kuliko kukimbia kimbia ukidhani ndo utawahi kufika,hapana
JITAMBUE BADILIKA na hii ndo #Roadlife.

Thomas B Mwamfupe ...
RSA Tanzania.......
 
Mkuu Msaada wako sijataka kukuendea PM.

Gari ya mkononi kutoka Kwa Dalal na Kwa sabab ni watu nsiojiana nao. Kununua usafiri nini Cha kuzingatia kuepuka adha yoyote mbaya badae. Asante Sana
 
Back
Top Bottom