Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Polisi nchini Marekani wamemtia mbaroni abiria mmoja mkorofi aliyekuwa akifanya vurugu na kuwatupia takataka wasafiri wenzake ndani ya ndege ya shirika la Delta Air Lines.

Tukio hilo lilitokea Alhamisi jioni, Oktoba 8, 2026, kwenye ndege namba DL832 iliyokuwa ikisafiri kutoka Atlanta kuelekea Washington. Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ililazimika kupokewa na maafisa wa usalama mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kitaifa wa Ronald Reagan saa 1:13 usiku kwa saa za huko.

Vurugu hizo zilianza muda mfupi baada ya ndege hiyo kuanza safari yake ya dakika 90. Abiria huyo aliyekuwa ameketi kwenye kiti namba 2D alianza kurusha uchafu kwa watu waliokuwa karibu yake na kusababisha taharuki na usumbufu mkubwa ndani ya ndege.

Kutokana na hali hiyo, marubani walilazimika kuwasiliana na mamlaka za uwanja wa ndege mapema ili kuomba msaada wa polisi.

Ndege ilipotua salama na kuegeshwa kwenye lango lake, maafisa wa polisi na walinzi wa uwanja wa ndege walikuwa tayari wakimsubiri ambapo walimtoa mara moja kwenye ndege hiyo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Shirika la Delta Air Lines limesisitiza kuwa lina msimamo mkali wa kutovumilia kabisa tabia yoyote ya utovu wa nidhamu inayovuruga usalama na amani wakati wa safari za anga.
1791820760304.jpg
 
WASHINGTON D.C., Oktoba 9, 2026.
Bondia maarufu wa zamani, Mike Tyson, amezua gumzo baada ya kuonekana akiandamana na Rais wa Marekani, Donald Trump, katika safari iliyohusisha helikopta ya urais, Marine One, na ndege ya Air Force One.

Tyson alionekana akitembea na Trump katika bustani ya Ikulu ya Marekani kabla ya kupanda Marine One kuelekea kituo cha kijeshi cha Joint Base Andrews.
Baadaye, walipanda Air Force One kuelekea Syracuse, New York, kwa mkutano wa kisiasa.

Kabla ya safari hiyo, Trump alimtambulisha Tyson kwa waandishi wa habari huku akitania kwamba hatapigana naye siku hiyo, akieleza kuwa wamekuwa marafiki kwa muda mrefu.

Urafiki wao ulianza miaka ya 1980, wakati Trump alipohusika katika kuandaa mapambano ya ndondi ya Tyson huko Atlantic City.
1791822717270.jpg
 
Timu ya watafiti imewasili katika Kisiwa cha Nikumaroro, katika Bahari ya Pasifiki, kuchunguza kitu kisichotambulika kilichopo chini ya maji, ambacho kinahofiwa kuwa huenda ni mabaki ya ndege aliyokuwa akiitumia rubani maarufu wa Marekani, Amelia Earhart, aliyetoweka mwaka 1937.

Earhart na mwongozaji wake wa safari za anga, Fred Noonan, walipotea Julai 2, 1937, walipokuwa wakisafiri kwa ndege kuvuka Bahari ya Pasifiki. Hadi sasa, ndege yao aina ya Lockheed Electra haijapatikana kwa uthibitisho wa mwisho.

Kitu kinachochunguzwa, kinachojulikana kama Taraia Object, kinaonekana kuwa na umbo lisilotambulika chini ya maji karibu na ufukwe wa kisiwa hicho. Watafiti wanaamini huenda ikawa ndege hiyo, lakini bado hakuna uthibitisho wa kisayansi unaothibitisha dhana hiyo.

Uchunguzi huo pia umeibua tena nadharia inayohusisha kaa wakubwa wanaojulikana kama coconut crabs, ambao huishi katika kisiwa hicho. Mwaka 1940, mifupa ya binadamu iliyokamilika kwa sehemu iligunduliwa Nikumaroro, lakini baadaye mifupa hiyo ilipotea kabla ya utambulisho wake kuthibitishwa.

Taarifa za wakati huo zilisema kaa hao huenda walitawanya mifupa hiyo. Majaribio yaliyofanywa baadaye kwa kutumia mzoga wa nguruwe yalionyesha kuwa kaa wa aina hiyo na kaa wadogo wa nchi kavu waliweza kuondoa sehemu kubwa ya nyama ndani ya wiki mbili, huku baadhi ya mifupa ikipatikana umbali wa takribani mita 18 kutoka eneo la awali.

Nadharia moja inaeleza kuwa Earhart na Noonan huenda walitua kwa dharura katika kisiwa hicho, wakaishi kama watu waliokwama bila msaada na hatimaye kufariki. Kwa mujibu wa nadharia hiyo, kaa hao huenda walikula mabaki ya miili yao baada ya kufariki; hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa kaa hao ndio waliowaua.

Timu hiyo, inayohusisha Archaeological Legacy Institute na Chuo Kikuu cha Purdue, inalenga kuchunguza kitu hicho moja kwa moja ili kubaini kama kina uhusiano wowote na ndege iliyotoweka.
1791954674558.jpg
 
Morocco imewasilisha ombi rasmi kwa Marekani la kupata mafunzo kwa marubani wa Jeshi la Anga la Kifalme la Morocco kuhusu uendeshaji wa ndege za kivita aina ya F-35A, hatua inayodokeza uwezekano wa nchi hiyo kujiandaa kununua ndege hizo za kizazi cha tano.

Ombi hilo linafuatia juhudi za Morocco kuimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na Washington pamoja na kuboresha uwezo wa jeshi lake la anga. Nchi hiyo tayari inaendelea na mpango wa kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, ikiwemo ununuzi wa ndege za kivita aina ya F-16 Block 72 zilizotengenezwa na kampuni ya Lockheed Martin ya Marekani.

Inatarajiwa kuwa mafunzo kwa marubani wa Morocco yanaweza kufanyika katika Kituo cha Jeshi la Anga la Marekani cha Luke, kilichopo Arizona. Kwa kuwa F-35A ni ndege yenye kiti kimoja cha rubani, maandalizi yake yanahitaji mafunzo ya kina ya darasani na matumizi ya mitambo ya mazoezi ya kuiga mazingira halisi ya urubani (Flight Simulator) kabla ya marubani kuruhusiwa kuendesha ndege hizo.

Hatua hiyo inakuja wakati Morocco ikiendelea kuboresha uwezo wake wa kijeshi, huku ushindani wa kijeshi na Algeria ukiwa miongoni mwa mambo yanayoangaziwa katika tathmini ya mahitaji ya ulinzi ya nchi hiyo.

Algeria nayo imekuwa ikiimarisha uwezo wa jeshi lake la anga kwa kutumia mifumo ya kijeshi inayotengenezwa na Urusi.

Hata hivyo, ombi la mafunzo pekee halimaanishi kuwa mkataba wa ununuzi wa F-35A umekamilika.

Endapo Morocco itanunua ndege hizo, itakuwa hatua muhimu katika juhudi zake za kuongeza uwezo wa operesheni za kijeshi na kujiunga na kundi la mataifa yanayotumia teknolojia ya ndege za kivita za kizazi cha tano.
1791998288676.jpg
 
Mradi wa ndege kubwa ya abiria ya masafa marefu, ulioanzishwa na China na Urusi mwaka 2017, ulilenga kuleta ushindani kwa ndege za Boeing 787 na Airbus A330neo. Hata hivyo, tofauti za kibiashara, teknolojia na vikwazo vya kimataifa zilisababisha ushirikiano huo kuvunjika, huku kila nchi ikiendelea na mipango yake.

Mradi huo ulijulikana kama CR929 na ulisimamiwa na kampuni ya pamoja ya China-Russia Commercial Aircraft International Corporation (CRAIC), iliyoundwa na COMAC ya China na United Aircraft Corporation (UAC) ya Urusi.

Ndege hiyo ilipangwa kubeba takribani abiria 280 hadi 400 na kuwa na uwezo wa kuruka umbali wa karibu kilomita 12,000, hivyo kulenga soko la safari ndefu za kimataifa.

Kwa nini Urusi ilijitoa?

Tofauti kati ya China na Urusi zilihusu zaidi mgawanyo wa majukumu, umiliki wa teknolojia na uteuzi wa kampuni zitakazozalisha mifumo mbalimbali ya ndege hiyo.

Hali ilibadilika zaidi mwaka 2022 baada ya Urusi kuingia katika vita dhidi ya Ukraine na kukabiliwa na vikwazo vya Marekani na nchi za Ulaya. Vikwazo hivyo vilifanya upatikanaji wa teknolojia na vipuri vya anga kutoka nje kuwa mgumu.

Urusi ilitaka kuongeza matumizi ya teknolojia inayozalishwa nchini humo, wakati China ikiendelea kutafuta ushirikiano na wazalishaji mbalimbali wa kimataifa. Kutokana na tofauti hizo, ushiriki wa Urusi katika mradi ulipungua, na hatimaye China ikaendelea na ndege hiyo chini ya jina C929, bila herufi R iliyokuwa ikiwakilisha Urusi.

China inaendeleaje na C929?

Kampuni ya COMAC imeendelea na usanifu wa C929 kwa lengo la kuifanya iwe ndege ya masafa marefu inayoweza kushindana katika soko la kimataifa.

Mradi huo unahusisha maendeleo ya usanifu, majaribio ya kiufundi na maandalizi ya mifumo itakayohitajika kabla ya ndege kuanza kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kibiashara.

Hata hivyo, C929 bado haijaingia katika huduma za kibiashara, na tarehe rasmi ya kuanza safari zake haijathibitishwa.

Urusi imeelekeza nguvu wapi?

Baada ya kujitenga na mradi huo, Urusi imeendelea kuweka kipaumbele katika ndege zake za ndani, zikiwemo MC-21, Tu-214 na Il-96.

MC-21 inalenga soko la safari za masafa ya kati, huku Tu-214 ikiendelezwa kama sehemu ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa ndege za abiria nchini humo. Il-96 ni ndege kubwa ya masafa marefu inayotengenezwa na Urusi.

Kwa ujumla, kuvunjika kwa ushirikiano wa CR929 kumeifanya China kuendeleza C929 kivyake, huku Urusi ikijikita katika miradi inayotegemea zaidi teknolojia na uzalishaji wa ndani.
1791999151604.jpg
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetangaza kuondoa hatua za muda zilizowekwa kurahisisha huduma za usafiri wa anga nchini, kuanzia Novemba 1, 2026.

Hatua hizo zilianzishwa Juni 18, 2025, kwa lengo la kuendeleza muunganiko wa safari za anga na kupunguza usumbufu kwa abiria na wadau wa sekta hiyo.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuruhusu mashirika ya ndege ya kimataifa kupata haki za ziada za usafiri wa anga, pamoja na kutoa unafuu wa kiudhibiti kwa mashirika ya ndege ya Tanzania kupitia mikataba ya codeshare na vibali maalumu vya muda.

Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 15, 2026, TCAA imesema uamuzi huo umetokana na mabadiliko ya hali ya uendeshaji na kupungua kwa hitaji la kuendelea na utaratibu huo wa muda.

Kutokana na uamuzi huo, mashirika yote ya ndege yatakayoathirika yanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazotumika katika uendeshaji wa usafiri wa anga nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri K. Bakari, ambayep pia amesisitiza dhamira ya mamlaka hiyo ya kuhakikisha sekta ya usafiri wa anga inaendelea kwa usalama, ulinzi na utaratibu unaofaa.
1792058745421.jpg
 
Mnamo tarehe 17 Februari 2024, ndege ya Airbus A321 ya shirika la Lufthansa, namba ya safari LH1140, ilikuwa ikisafiri kutoka Frankfurt, Ujerumani, kuelekea Seville, Hispania, ikiwa na abiria 199 na wahudumu sita.

Ndege hiyo ikiwa katika usawa wa futi 35,000, nahodha alitoka kwenye chumba cha marubani kwenda kutumia choo. Sekunde 36 tu baadaye, rubani msaidizi alipata kifafa cha ghafla kutokana na tatizo la mfumo wa neva ambalo lilikuwa halijagunduliwa.

Katika hali hiyo, rubani msaidizi alibonyeza baadhi ya mifumo ya ndege bila kukusudia, na kusababisha ndege kuyumba kidogo. Hata hivyo, mfumo wa kujiendesha wa ndege (autopilot) uliendelea kufanya kazi na kurekebisha mabadiliko hayo.

Nahodha aliporudi baada ya takribani dakika nane, ambapo alikuta mlango wa chumba cha marubani haufunguki.
Alijaribu kutumia namba ya kawaida ya kuingilia mara kadhaa bila mafanikio, huku wahudumu wa ndani ya ndege wakijaribu kuwasiliana na rubani msaidizi bila kupata majibu.

Hatimaye, nahodha alitumia mfumo wa dharura kufungua mlango.
Kabla muda wa mfumo huo haujaisha, rubani msaidizi alipata fahamu kwa kiasi cha kutosha na kufungua mlango kutoka ndani.

Nahodha alirejesha udhibiti wa hali ya ndege na, baada ya kuona rubani msaidizi akiwa amepauka, akitokwa na jasho na kuonyesha dalili zisizo za kawaida, alitangaza dharura ya kiafya na kuelekeza ndege kwenda Madrid, Hispania, ambako ilitua salama.

Uchunguzi ulionyesha kuwa tatizo lililosababisha tukio hilo lisingeweza kugunduliwa kwa urahisi kupitia vipimo vya kawaida vya afya bila kuwepo kwa dalili za awali.

Kwa bahati nzuri, watu wote 205 waliokuwa ndani ya ndege hawakupata majeraha.
1792254857673.jpg
 
Helikopta ya upelelezi ya jeshi la Saudi Arabia aina ya Apache AH-6i imeanguka katika eneo la Najran, kusini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Yemen, na kusababisha vifo vya wafanyakazi wawili waliokuwa ndani yake.

Msemaji wa muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, Meja Jenerali Turki al-Maliki, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa rasmi aliyochapisha mnamo Jumapili, tarehe 18 Oktoba 2026.

Al-Maliki alieleza kuwa ndege hiyo ilianguka ikiwa kwenye eneo lililo chini ya mamlaka ya Wizara ya Walinzi wa Taifa wa Saudi Arabia kutokana na hitilafu za kiufundi.
Hata hivyo, taarifa hiyo inakinzana na madai ya waasi wa Houthi wa Yemen.

Siku moja kabla ya taarifa ya serikali, yaani siku ya Jumamosi, tarehe 17 Oktoba 2026, msemaji wa kijeshi wa Houthi, Yahya Saree, aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) kuwa wapiganaji wao walifanikiwa kuidungua helikopta hiyo.

Saree alidai kuwa walilenga ndege hiyo wakati ikitekeleza operesheni dhidi ya maeneo yao ya mpakani.

Meja Jenerali wa Saudi Arabia, al-Maliki alipinga vikali madai hayo ya waasi. Alijibu kwa kuchapisha picha za helikopta hizo zikiwa salama na kusisitiza kuwa madai ya Houthi si ya kweli na ndege hizo zitaendelea na kazi zake uwanjani hivi karibuni.

Eneo la Najran limekuwa mstari wa mbele kushuhudia mapigano ya mara kwa mara na mashambulizi ya makombora huku mvutano kati ya muungano wa Saudi Arabia na waasi wa Houthi ukizidi kuongezeka.
1792373266338.jpg
 
Helikopta ya upelelezi ya jeshi la Saudi Arabia aina ya Apache AH-6i imeanguka katika eneo la Najran, kusini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Yemen, na kusababisha vifo vya wafanyakazi wawili waliokuwa ndani yake.

Msemaji wa muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, Meja Jenerali Turki al-Maliki, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa rasmi aliyochapisha mnamo Jumapili, tarehe 18 Oktoba 2026.

Al-Maliki alieleza kuwa ndege hiyo ilianguka ikiwa kwenye eneo lililo chini ya mamlaka ya Wizara ya Walinzi wa Taifa wa Saudi Arabia kutokana na hitilafu za kiufundi.
Hata hivyo, taarifa hiyo inakinzana na madai ya waasi wa Houthi wa Yemen.

Siku moja kabla ya taarifa ya serikali, yaani siku ya Jumamosi, tarehe 17 Oktoba 2026, msemaji wa kijeshi wa Houthi, Yahya Saree, aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) kuwa wapiganaji wao walifanikiwa kuidungua helikopta hiyo.

Saree alidai kuwa walilenga ndege hiyo wakati ikitekeleza operesheni dhidi ya maeneo yao ya mpakani.

Meja Jenerali wa Saudi Arabia, al-Maliki alipinga vikali madai hayo ya waasi. Alijibu kwa kuchapisha picha za helikopta hizo zikiwa salama na kusisitiza kuwa madai ya Houthi si ya kweli na ndege hizo zitaendelea na kazi zake uwanjani hivi karibuni.

Eneo la Najran limekuwa mstari wa mbele kushuhudia mapigano ya mara kwa mara na mashambulizi ya makombora huku mvutano kati ya muungano wa Saudi Arabia na waasi wa Houthi ukizidi kuongezeka.View attachment 3693282
Hii ni mbaya kwa saudia
 
D.B. Cooper ni jina bandia alilopewa mwanamume aliyeteka nyara ndege ya abiria aina ya Boeing 727 nchini Marekani mnamo Novemba 24, 1971, na kufanya moja ya matukio ya kushangaza na fumbo kubwa zaidi ambalo halijawahi kutatuliwa katika historia ya anga.
Hapa kuna mkakati mzima wa kisa chake ulivyokuwa:

1. Kutekwa kwa Ndege

Siku ya tukio, mwanamume aliyejitambulisha kama Dan Cooper alinunua tiketi ya ndege ya shirika la Northwest Orient Airlines kutoka Portland kwenda Seattle. Baada ya ndege kuruka, alimpa muhudumu wa ndege kikaratasi kilichosema ana bomu kwenye mkoba wake. Alionyesha bomu hilo kwa sekunde chache na kutoa madai yake:
• Dola za Kimarekani $200,000 za sarafu za nchi hiyo (zote zikiwa kwenye noti za dola 20).
• Miamvuli minne (parachutes) — miwili mikuu na miwili ya akiba.
• Gari la mafuta liwe tayari kumwongezea mafuta ndege hiyo mara watakapotua Seattle.

2. Kupokea Kikombozi na Kuruka Tena

Ndege ilitua Seattle, ambapo abiria wote 36 waliachiliwa salama baada ya maafisa wa serikali kumpatia Cooper pesa na miamvuli aliyotaka. Aliamuru ndege hiyo iruke tena ikielekea Reno, Nevada, huku akitaka iruke kwa kasi ndogo na kwa urefu wa chini ya futi 10,000.

3. Kuruka kwa Parachuti na Kutoweka

Wakiwa angani kati ya Seattle na Reno, kwenye eneo lenye misitu minene na milima ya Kusini-Magharibi mwa jimbo la Washington, Cooper alifungua mlango wa nyuma wa ndege na kuruka usiku kucha kukiwa na dhoruba kali ya mvua.
Tangu usiku ule, Dan Cooper hajawahi kuonekana tena. Licha ya msako mkubwa uliohusisha jeshi, polisi, na idara ya ujasusi ya FBI, hakuna mwili wala miamvuli iliyopatikana mara moja.

4. Ushahidi Pekee Uliopatikana

Mnamo mwaka 1980, mvulana mmoja alipata mabunda ya noti za dola 20 zilizokuwa zimeoza zikiwa zimezikwa kwenye mchanga kando ya mto Columbia. Noti hizo zilikuwa na jumla ya $5,800, na nambari zake za siri (serial numbers) zililingana kabisa na zile zilizopewa D.B. Cooper. Hii ilithibitisha kuwa alitua au alipita eneo lile, lakini hakuna ushahidi mwingine wa mabaki ya mwili wake uliopatikana.

Hatima ya Upelelezi

Baada ya miaka 45 ya upelelezi mkubwa na kuchunguza maelfu ya washukiwa, shirika la FBI lilifunga rasmi upelelezi wa kesi hii mnamo mwaka 2016 bila kupata jibu la nani hasa alikuwa D.B. Cooper na kama alinusurika baada ya kuruka usiku ule wa baridi kali. Hadi leo, kisa hiki kinabaki kuwa fumbo kuu la uhalifu duniani.
 
1. Washukiwa Wakuu Wanaohisiwa Kuwa D.B. Cooper
Katika miaka 45 ya upelelezi, FBI ilichunguza washukiwa zaidi ya 1,000. Hawa hapa ndio wanaoongoza kwa kuhisiwa zaidi:
  • Richard McCoy Jr.: Huyu anatajwa kuwa mshukiwa mkuu mwenye nguvu zaidi. Miezi minne tu baada ya tukio la D.B. Cooper, McCoy aliteka ndege nyingine kwa mtindo ule ule na kuruka kwa parachuti akiwa na dola $500,000. Alikamatwa na kuhukumiwa miaka 45 jela lakini FBI walisema sura yake haikulingana kikamilifu na maelezo ya mashuhuda wa kesi ya Cooper.
  • Sheridan Peterson: Alikuwa mwanajeshi wa zamani wa kikosi cha anga na alifanya kazi kwenye kampuni ya Boeing. Alikuwa mtaalamu mkubwa wa kuruka na miamvuli. FBI walimchunguza sana lakini hawakupata ushahidi wa kutosha wa DNA kumtia hatiani.
  • Robert Rackstraw: Alikuwa rubani wa jeshi la nchi kavu wakati wa vita vya Vietnam na alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya kuishi mwituni na kuruka kwa miamvuli. Rackstraw alijulikana kwa akili nyingi na dharau kwa mamlaka, na hata alipohojiwa mara nyingi alitoa majibu ya mafumbo yaliyofanya watu waamini ni yeye. Alifariki mwaka 2019 bila kushtakiwa rasmi.
 
2. Nadharia: Je, Alinusurika au Alikufa?

Wataalamu wamegawanyika katika makundi mawili makubwa kuhusu hatima ya Cooper baada ya kuruka kutoka kwenye ndege:
• Nadharia ya Kifo (Mtazamo wa FBI): FBI wanaamini kuwa Cooper hakunusurika. Usiku ule ulikuwa na dhoruba kali ya mvua, baridi ilikuwa chini ya sifuri (freezing temperatures), na aliruka akiwa amevaa suti ya kawaida na viatu vya ngozi juu ya misitu minene yenye milima. Pia, alichagua miamvuli miwili ya zamani bila kujua kuwa mmoja ulikuwa wa mafunzo tu (uliokuwa umeshonwa usifunguke). Pesa zilizopatikana zikiwa zimeoza mtoni mnamo 1980 zinaunga mkono nadharia kuwa huenda alifia msituni na pesa zikasombwa na maji.
• Nadharia ya Kunusurika: Wanaounga mkono nadharia hii wanadai kuwa Cooper alikuwa mtaalamu wa hali ya juu ambaye alijua anachokifanya. Uchaguzi wa ndege (Boeing 727 ambayo ilikuwa na mlango wa nyuma unaofunguka angani) na maelekezo yake kwa rubani ya kuruka kwa kasi ndogo na urefu wa chini yanathibitisha alikuwa na mpango madhubuti. Wanaamini alitua salama, akazika sehemu ndogo ya pesa ili kupoteza maboya (zilizopatikana mtoni), na kutokomea na zilizobaki.
 
Back
Top Bottom