Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Do Pilots sleep during flight? [emoji3575]

The answer is yes!

Pilots are allowed to take a rotational rest for about 45 minutes or depending on the longevity of the journey whenever the workload is light. This obviously helps the two pilots to stay alert during the most crucial part of the flight.

It is not proper for the two pilots to fall asleep as it is a big risk.

However, on 15th August 2022, Two pilots flying a plane from Sudan to Ethiopia fell asleep when the aircraft was 37,000 feet above sea level, and missed their landing.
luck being on their sides, one of the pilots suddenly woke up and subsequently the succeeded in safely landing the aircraft without any injuries.

Bonus: [emoji16]

What happens when a plane run out of fuel in mid air?

An airliner can land if it runs out of fuel. The only difficulty will be finding an airport within its glide distance but if it doesn’t find one, it would need to land anywhere, as the airliner drops from the air diametrically. So it is not like it will fall off just because it has run out of fuel.

Oluwanishola Akeju
FB_IMG_1690776750119.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
#SUPATECH: Wakala wa maswala ya anga na hali ya hewa kutokea nchini Marekani, National Aeronautics and Space Administration (NASA) imepanga kuja na ndege ambayo itakuwa na uwezo wa kukusafirisha sehemu yoyote Duniani kwa muda wa masaa mawili tu.

Taarifa za mwisho kutoka NASA kwamba wamefanikiwa kutengeneza chombo cha anga ambacho kimepewa jina la X-59 chenye uwezo wa kwenda umbali wa km 1,500 kwa lisaa.

Chanzo: The times

#EastAfricaTv #SupaTech
FB_IMG_1690785371195.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya takriban miaka 38 angani, Flight Purser, Alice Waweru alihitimisha safari yake ya mwisho ya muda wake kama mhudumu kwa kumalizikia safari ya mwisho ya ndege kwenda JFK, New York.

Ili kumtukuza kwa utumishi wake wa mfano, alifanyiwa saluti ya maji ya mzinga ambayo ilimshangaza.
Alice, ambaye alijumuika na familia yake na marafiki, anashikilia sifa ya kuwa kiongozi wa Wahudumu kwenye safari yetu ya mwisho ya kihistoria ya uzinduzi wa ndege kuelekea New York.

Chanzo:
Kenyaairways
FB_IMG_1692179887830.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝗡𝗱𝗲𝗴𝗲 𝘆𝗮 𝗖𝗼𝗻𝗰𝗼𝗿𝗱 𝗶𝗹𝗶𝘄𝗮𝗵𝗶 𝗸𝘂𝘁𝘂𝗮 𝗞𝗲𝗻𝘆𝗮 𝗺𝗻𝗮𝗺𝗼 𝗺𝘄𝗮𝗸𝗮 𝟭𝟵𝟴𝟴 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝘀𝗲𝗵𝗲𝗺𝘂 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗷𝗮𝗿𝗶𝗯𝗶𝗼 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝘂𝗳𝘂𝗻𝗱𝗶.
FB_IMG_1692179713069.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Igor Sikorsky, mwanasayansi, mhandisi, rubani na mfanyabiashara, alikuwa mwanzilishi katika muundo wa ndege ambaye anajulikana zaidi kwa bunifu yake ya helikopta.
Baada ya miundo miwili ya helikopta kushindwa, Sikorsky alielekeza mawazo yake kwa ndege za kawaida.
Kufikia 1913 alikuwa ametengeneza Il’ya Muromets, ndege za abiria zenye injini nne ambazo ziligeuzwa kuwa za kulipua kwa ajili ya matumizi katika WWI. Mapinduzi ya Bolshevik yalimlazimisha Sikorsky na familia yake kuhamia Amerika mnamo 1919 ambapo alianzisha Shirika la Uhandisi la Sikorsky Aero huko New York.
Katika miaka 20 iliyofuata, kampuni ya Sikorsky ilijenga ndege za abiria na boti za kuruka, kutia ndani S-40 American Clipper ambayo ilitumiwa kufungua njia mpya za anga katika Pasifiki.

Katika miaka ya 1930 Sikorsky alielekeza mawazo yake tena kwa muundo wa helikopta na mnamo Septemba 14, 1939, Sikorsky mwenyewe aliruka na VS-300 ndege yake ya kwanza ya majaribio.
Igor Sikorsky, aliyeonekana hapa kwenye pua ya 1943 XR-5 yake, alifariki mnamo Oktoba 26, 1972.

Chanzo:
Flight magazine
FB_IMG_1693991569074.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana huwezi kutumia mfumo wa reverse kama break hizi ni part mbili tofauti kabisa kulingana na speed ya ndege hata kwa dawa reverse haiwezi kuingilia mfumo wa break kwenye mfumo wa gari tuuu ni shughuli
 
UNAFAHAMU NINI KUHUSU KIOO CHA HUD?

Sote tunaona mara kadhaa katika baadhi ya filamu zinazohusisha mashambulizi ya ndegevita angani hutumia miongozo ya kioo macho mbele kinachomsaidia rubani kumuweka kwenye 18 adui 'Locking Target ' kisha kulenga na silaha yake.
Huu ndiyo mwanzo wa kioo 'macho mbele' au 'kichwa juu' kitaalamu 'Heads Up Display' au #HUD.

HUD ni kioo wazi kinachoonesha pande mbili (transparent) ambacho humpa rubani misingi ya taarifa muhimu za ndege.
Hii inawezesha macho ya rubani kubaki yakiangalia nje ya ndege huku akipata taarifa za hali halisi na mwenendo wa ndege yake katika kioo cha HUD pasipo kuhamisha macho mara kwa mara kutazama chini.

Teknolojia ya HUD zilianza kutumika katika ndege-vita za vita vya pili vya dunia na kuendelea katika matumizi ya kijeshi miaka ya 1960.

Matumizi ya kwanza kiraia au kibiashara ilianza mnamo 1993 na leo ni kawaida kukuta katika ndege zote za kijeshi, abiria na binafsi.

#Boeing787 "#Dreamliner" ni miongoni mwa ndege za kwanza za abiria kusimikwa kioo cha HUD kama kifaa cha kawaida kutoka #RockwellCollins.

HUD za kawaida zinaweza kuonesha maumbo, ishara na alama halisi kuhusu mwenendo wa ndege kama mwendo, uelekeo, kimo cha angani, data za rada, mahala ilipo n.k
Vingine vinampa chaguzi rubani kuweka mambo muhimu tu anayohitaji kuyaona.

HUD katika ndege za kijeshi inaonesha taarifa nyingi za ziada za msingi kama shabaha ya shambulio, hali ya silaha n.k

Vioo vingi vya kisasa 'Enhanced Flight Vision System' au #EFVS vina uwezo wa kumuonesha rubani njia mbele hata kama kuna hali mbaya ya hewa inayozuia macho ya kawaida kuona.

Katika ndegevita HUD hujumuishwa pia katika kofia ya rubani 'Helmet Mounted Display' (#HMD).

#Aviationtoday
FB_IMG_1695536004128.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndege ya kwanza aina ya Boeing 737-9 MAX kwaajili ya AirTanzania inayoonesha usajili namba 5H-TCP ikiwa majaribio mruko B-2 katika uwanja wa Boeing mapema leo asubuhi.
Hii ni ndege ya kwanza kati ya mbili 737-9 MAX kwa Tanzania zilioagizwa moja kwa moja kutoka Boeing.
Jina la ndege ni "Olduvai Gorge".
Pichani ni kabla na baada ya kupakwa rangi.

Picha/chanzo:
BFI watch/Twitter
FB_IMG_1695794413683.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado inatupa tabu kiasi kufahamu tabiahewa ya umbo na upaaji wa ndege hii ambayo iliwahi kupendekezwa na kampuni ya #Lockheed
FB_IMG_1696082464765.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji630] Shirika la ndege la China Eastern Airlines leo limetia saini mkataba wa ununuzi wa kununua ndege 100 za C919 kutoka kwa mtengenezaji wa ndege wa China, COMAC.
Mpango huo wa ununuzi una thamani ya dola bilioni 10.
Uwasilishaji umepangwa kufanyika kwa awamu kuanzia 2024 hadi 2031.
Hili ndilo agizo kubwa zaidi la ndege ya C919 kufikia sasa na kufanya China Eastern Airlines kuwa mtumiaji mkuu zaidi duniani wa ndege za sasa za C919.

Shirika la ndege la Brunei, Gallop Air, linakuwa shirika la pili la kimataifa kutambulisha ndege aina ya COMAC C919 katika ndege zake.
Kufikia sasa, COMAC C919, ambayo imekuwa kwenye habari kuwa mshindani wa familia ya Airbus A320 na ndege ya familia ya Boeing B737.

[emoji328]
[emoji2398]Habari za Xinhua
FB_IMG_1696089915267.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KIFUPI KUHUSU NDEGE AINA YA BOEING 737 MAX

Ndege za Boeing aina ya 737 MAX ilitumbukia katika moja ya janga kubwa zaidi katika historia ya usafiri wa anga kufuatia ajali mbili mbaya zilizosababisha kusitishwa uendeshaji wake kwa muda.

Hali hiyo ilisababishwa na 'Software' (MCAS) yenye lengo la kudhibiti tabia mpya inayozalishwa na ndege katika upaaji kwasababu ya injini mpya kubwa, mara nyingine ilidhibiti tabia hiyo nje na maamuzi ya rubani.

Licha ya hiyo, 737 MAX ilirudi kuendelea kutoa huduma baada ya marekebisho na maboresho makubwa na kubaki kuwa moja ya ndege maarufu na salama zaidi duniani, kwa historia na mtandao mkubwa wa waendeshaji na wauzaji.
MAX inakuja moja kwa kushindana na mpinzani wake mkubwa 'Airbus' familia ya 320NEO' na pia Embraer toleo za EMR190s.

Boeing 737 MAX ni kizazi cha nne cha familia ya ndege zake za Boeing737 Bodi nyembamba (Narrow body)

MAX inajumuisha injini mpya na maboresho mengine ya teknolojia kulinganisha na vizazi vyake vingine vilivyopita kama:
Boeing 737-100/200 (kawaida)
Boeing 737-300/400/500 (Classic)
Boeing 737-600/700/800/900 (Next Generation "NG"

Boeing 737 MAX iliongeza ufanisi kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi, kuongezeka kwa idadi ya abiria, kupunguza matumizi ya mafuta na vichafuzi kwa asilimia 20 huku ikipunguza kelele kwa asilimia 50% na pungufu ya asilimia 14% gharama za matengenezo.
Boeing 737 MAX ni maarufu zaidi kwa muonekano wa ncha yenye V kwenye mabawa (winglets).

Toleo la Boeing 737 MAX ilianzishwa Desemba 2011 baada ya kupokea oda kutoka shirika la ndege Southwest.

Max ya kwanza yenye namba 42554 na usajili N8701Q ilifanya mruko wa uzinduzi mnamo Januari 29, 2016, kutoka Renton, Washington.

Matoleo ya MAX, upakiaji abiria viwango vya juu pasipo kuzingatia madaraja;
B737-7 hadi abiria 172
B737-8 hadi abiria 189
B737-9 hadi abiria 220
B737-10 hadi abiria 230

Mashirika yanaendesha ndege hii ni kama AerCap, Aviation Capital Group (ACG), Copa, Donghai, GE Capital Aviation Services, Lion Air, Malaysia, TUI Group, United Airlines, Xiamen Airlines, Ethiopian, Air Tanzania n.k

Shirika la ndege Air Tanzania linategemea kupokea ndege yake ya kwanza aina ya Boeing 737-9 MAX siku ya 03/Oktoba/2023 kwa mujibu wizara ya uchukuzi.

Makala fupi na:
#Airwaysmag
#Admin mkuu/Aviation Media Tanzania

[emoji328]
Kwa hisani ya mtandao
FB_IMG_1696325633058.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boeing Defense imetoa picha ya kwanza ya chombo chake cha chini ya bahari iitwayo #Orca "Extra-large unmanned undersea vehicle" au #XLUUV. kichoendeshwa na mtu ikiwa majaribio baharini.
Pentagon mnamo 2019 ilitoa oda kundi la kwanza ya Orcas nne, chombo chenye tani 80 kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani, na ya tano kuongezwa baadaye mwaka huo.

Kutumia 'drones' katika vita ni dhana ya kawaida kwa wengi katika dunia ya sasa.
Lakini kutumia drones chini ya maji ni mageuzi bado yanayoendelea kufanyiwa tafiti.
Manowari ya Orca ni hatua ya mwanzo katika uwanja huu wa mifumo ya chini ya maji isiyo na rubani inayowasilisha uwezo mpya wa kupigana chini ya bahari.
Orca itakuwa na uwezo wa kubeba silaha za mashambulizi na kujikinga.

Makala:
#Boeing
NavalNews
FB_IMG_1696412940468.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom