Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

C-17 Globamaster III kutoka Qatar ikiwa Kilimanjaro.
FB_IMG_1708710126440.jpg
 
C-17 Globamaster III kutoka Qatar ikiwa Kilimanjaro.
FB_IMG_1708710126440.jpg
 
The Hybrid Air Vehicles Airlander 10, initially known as the HAV 304, is a hybrid airship crafted by the British company Hybrid Air Vehicles (HAV). This unique aircraft features a helium airship structure along with supplementary wing and tail components. It utilizes a combination of aerostatic and aerodynamic lift principles for flight and is driven by four ducted propellers powered by diesel engines.
FB_IMG_1708811720325.jpg
 
"MAWAZO YA ADMIN"

Ifike kipindi kusadikika kuwe na taasisi yenye nguvu itayoshughulikia utafiti na uundaji wa vyombo vya usafiri wa anga, Reli, Baharini na Barabarani.

Lazima tujiondoe kundi la watu wa kungoja na kupoteza vipaji na Taaluma zinaoishia kwenye makaratasi.
Taasisi iwe inashirikisha wataalamu mbalimbali wa kujitolea kutoka kwenye sekta husika, iwe serikalini au binafsi, ndani na nje ya nchi.

Binafsi, nategemea kuandika na kusajili Taasisi binafsi 'NGO' itakayohusika na masuala hayo.
Sitojali kama itaendelezwa au la.

Nitaibatiza kwa jina la,
"Bonde la Tanzanite"

Admin.

Picha:
Gabriel Ngeritu/X
FB_IMG_1708813931570.jpg
 
Siku kama ya leo katika usafiri wa anga, Antonov An-22, iliyoundwa na Antonov Design Bureau ilikuwa ndiyo ndege kubwa zaidi wakati huo, ilifanya safari yake ya kwanza mnamo Februari 27, 1965.

Ikiwa kama ndege kubwa zaidi duniani inayotumia Mapangaboi 'turboprop' ilijivunia uwezo wa ajabu wa kupakia shehena na utendajikazi ikiendeshwa na injini nne za Kuznetsov NK-12.

Safari hii ya ndege ya kwanza iliashiria mwanzo wa kazi yake mashuhuri katika usafiri wa kijeshi, misaada ya kibinadamu, na usafirishaji wa mizigo mizito.

Admin.

[emoji991]
Pinterest
FB_IMG_1709035342088.jpg
 
𝗪𝗮𝗲𝗻𝗱𝗲𝘀𝗵𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗕𝗼𝗲𝗶𝗻𝗴 787 𝗗𝗿𝗲𝗮𝗺𝗹𝗶𝗻𝗲𝗿 𝗯𝗮𝗿𝗮𝗻𝗶 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗸𝗮 2024.

1. Ethiopian Airlines linaendesha ndege Ishirini na Tisa za Boeing 787 Dreamliners. (19 B787-8s & 10 B787-9s)

2. Kenya Airways inaendesha ndege Tisa za Boeing 787-8 Dreamliners.

3. Royal Air Maroc inaendesha Ndege Tisa za B787 (5 B787-8s & 4 B787-9s.)

4. Egyptair inaendesha ndege Saba za Boeing 787-9 Dreamliners.

5. Air Tanzania inaendesha ndege Mbili za Boeing 787-8 Dreamliners.

AvMedTz
FB_IMG_1709216725262.jpg
 
Nadhani kwa Rubani kupinda bawa la ndege kiasi hiki, ni kama kujaribu kushusha ile mikono ya kwenye kony@gi [emoji1]
FB_IMG_1709277242321.jpg
 
JE, NDEGE INARUDI NYUMA?

Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).

Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.

Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo

1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust

2>'Brake' za matairi na

3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.

Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.

Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.

Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug

1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'

2>Kuepuka ulaji mafuta

3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.

4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.

5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.

#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053
Sijaona sehemu inayoonsha kuwa ndege inaweza kurudi nyuma zaidi ya kuonesha mzunguruko wa injini ndio hubadilika.
 
Katika filamu ya The Usual Suspect, Inaonekana Boeing 747 (injini nne) ikitua.
Wakati inaonyeshwa kwa nyuma, ikaonekana Boeing 767 (Injini Mbili) ikutua.
FB_IMG_1709458917113.jpg
 
The Hybrid Air Vehicles Airlander 10, initially known as the HAV 304, is a hybrid airship crafted by the British company Hybrid Air Vehicles (HAV). This unique aircraft features a helium airship structure along with supplementary wing and tail components. It utilizes a combination of aerostatic and aerodynamic lift principles for flight and is driven by four ducted propellers powered by diesel engines.View attachment 2915365
By diesel engine!!
 
'Order' za wateja kutoka Boeing Field.
FB_IMG_1709544186483.jpg
 
Chuma imechochora, nadhani mtu aliyeguswa zaidi na hili tukio unaweza kumtambua kirahisi sana pichani.
FB_IMG_1709592839275.jpg
 
Kuna ndege nyingi chini ya maji kuliko nyambizi angani
5fcdf97a40070f3aef4c1c9279286de1.jpg
 
Ndege zagongana Kenya

Takriban watu wawili wamepoteza maisha baada ya ndege mbili kugongana katika Hifadhi ya Kitaifa ya Nairobi.

Takriban wengine 44 walitoka bila majeraha katika tukio hilo leo asubuhi.
Tukio hilo lilihusisha ndege aina ya Dash 8 yenye Usajili namba 5Y-SLK mali ya Safari Link iliyokuwa ikielekea Diani ikiwa na abiria 44 na pamoja na ndege ya Cessna.

Chanzo:
FB_IMG_1709636838989.jpg
FB_IMG_1709636834919.jpg
 
Ndege zagongana Kenya

Takriban watu wawili wamepoteza maisha baada ya ndege mbili kugongana katika Hifadhi ya Kitaifa ya Nairobi.

Takriban wengine 44 walitoka bila majeraha katika tukio hilo leo asubuhi.
Tukio hilo lilihusisha ndege aina ya Dash 8 yenye Usajili namba 5Y-SLK mali ya Safari Link iliyokuwa ikielekea Diani ikiwa na abiria 44 na pamoja na ndege ya Cessna.

Chanzo:
View attachment 2925188View attachment 2925189
 
Back
Top Bottom