๐๐, ๐จ๐ก๐๐๐๐๐๐ ๐จ ๐๐๐ก๐ฆ๐ ๐๐๐๐๐๐ข๐ฃ๐ง๐ ๐๐ก๐๐ฉ๐ฌ๐ข๐ฃ๐๐?
{Ufafanuzi mwepesi}
#Helicopter ni ndege inayotumia bawa inayozunguka juu {panga} kutengeneza '#lift' ili iweze kupaa.
Kumbuka ndege ya kawaida inategemea kusukumwa na injini kwenda mbele ili hewa ya kutosha ipite chini kuweza kunyanyuka 'lift' na kupaa "take off"
Kwa Helikopta hali ni tofauti kidogo, kwani panga ndiyo zinakimbia/kuzunguka (rotation) ili kuzalisha 'lift'.
Lakini pia ina panga ndogo nyuma {mkiani} ili kuzuia body {#fuselage} kuzunguka pamoja na panga kubwa inapopaa (torque effect)
'Helicopter' kiasili ni ndege isiyotaka kupaa kwasababu viungo vyake lazima vifanye kazi kwa kupingana ili iweze kwenda sawa.
Hiyo ndiyo sababu 'Helicopter' inahitaji hesabu ya ziada kupaisha.
Rubani wa Helikopta muda wote hufanya kazi ya kuipa milinganyo tofauti "balance" kati ya panga kubwa na ndogo itakayomwezesha kupaa alivyokusudia.
#UPAAJI
{Endapo kila kitu shwari}
Rubani huwasha mzunguko wa injini #rpm hadi ifike kiwango kinachohitajika kwa kutumia '#throttle' {inafanana na mkono wa #acceleretor ya pikipiki}
Baada ya hapo huvuta juu '#collective' {inafanana na mkono wa #handbrake}
Kazi ya 'collective' ni kubadili 'angle' ya mapanga ya juu {rotor blades tilt} ili yawe na umbile linaloweza kukandamiza hewa chini na kupaa {mfano wa panga za feni zilivyokunjwa ili kuweza kusukuma upepo}.
Wakati wa kunyanyuka ina tabia ya kiwiliwili kutaka kuzunga na panga kubwa {#torque effect} hivyo rubani huzuia hali hiyo kwa kukanyaga pedeli ya kulia au kushoto kuiweka sawa, kutegemea kiwiliwili kinazunguka upande gani.
Pedeli hizi zina'control panga ndogo mkiani kama ilivyo kwenye ndege ya kawaida pedeli zinavyo'control' kielekezi (#rudder) mkiani ili kukata kona.
Ikifika kimo anachohitaji kwenda juu hutumia "#cyclic" ambayo ni 'control stick' iliyopo katikati ya miguu ya rubani na kazi yake kuinamisha panga kubwa kulia, kushoto, mbele au nyuma ili helikopta ielekee upande ambao panga litainamia.
Kama ni kwenda mbele atasukuma mbele taratibu "cyclic" ambayo itasababisha mzunguko wa panga la juu {#main_rotor_disk} kuinama kidogo mbele na kusababisha helikopta kufuata kuelekea huo.
Hii ni kwasababu panga kubwa litaanza kukandamiza hewa kwenda chini na nyuma na kusababisha helikopta kunyanyuka juu na kwenda mbele (lift & Thrust)
Rubani pia anaweza kuongeza nguvu ya injini kidogo kwenye 'throttle' yake au kuvuta "collective" ili kuongeza kasi ya panga kuzalisha nguvu hizo kutegemea na haraka au uzito wa Helkopta wakati huo akikanyaga kwa umakini pedeli kusahihisha uelekeo.
Zipo Helikopta ambazo hazina panga ndogo nyuma, bali ina panga mbili kubwa zilizo katika nguzo moja (rotor must) ambazo zinazunguka kinyume ili kuondoa tatizo la kiwiliwili kuzunguka na panga wanaita 'Coaxial rotor' au 'Counter rotating Blades' mfano Kamov #Ka52.
Pia kuna Helkopta nyengine yenye panga zote kubwa mbele na nyuma zinazozunguka kinyume mfano #Chinook CH-47.
Helkopta ni mashine ya kufanya kazi nyingi ambazo ndege ya kawaida haiwezi kufanya.
Na hii kutokana na uwezo wa wa kuganda sehemu moja hewani (hovering), kugeuka papo kwa papo, kwenda ubavu ubavu kama kaa (ngadu) au kurudi 'kinyume nyume'.
Helikopta inatumika katika kazi nyingi kama zimamoto na uokoaji (fire&rescue) katika sehemu ngumu kufikika na chombo kingine,
Jeshini kama kubeba mizigo (Cargo Helicopter #CH), kushambulia (Attack Helicopter #AH), na Shughuli nyengine za ziada (Utility Helicopter UH) na hata shughuli za kijasusi.
Kwa upande wa shughuli za kiraia Helikopta inatumika kama kubeba wagonjwa (Air Ambulance), Kubeba abiria au watu mashughuli (Passenger & VIP helicopters), kubeba mizigo na vifaa vya ujenzi mfano Crane 'Helicopters' na kadhalika.
Kutokana na ugumu wa kupaisha Helikopta wanaanga wanatumia usemi ufuatao;
"kupaisha ndege ya kawaida ni kama kuendesha baiskeli ya tairi mbili na kupaisha Helkopta ni kama kuendesha baiskeli ya tairi moja.
#Admin