Mada ya kuulizia walipo watu mashuhuri ndani na nje ya Tanzania

Mada ya kuulizia walipo watu mashuhuri ndani na nje ya Tanzania

Kindeena

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2017
Posts
11,462
Reaction score
21,124
Kuna wakati tunashindwa kujua walipo watu maarufu.

Pengine kwa sababu ya shughuli nyingi za Kitaifa tunashishwa kuwasikiliza kwenye vyombo vya habari pindi wanapokuwa wanazungumza.

Binafsi, kuna watu kama

John Mnyika: Huyu ni Katibu Mkuu wa CHADEMA. Zamani mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi 2015 hivi alikuwa mzungumzaji sana ila sasa hivi simsikii.

Wengine ni Dr Slaa, Raila Odinga, Bensoni Kigaila, nk

Wewe ni mtu gani humsikii?

Mtaje na bila shaka kuna watu wana taarifa zake.

NB: Mada haihusiani na uvumi; na wala kuvumisha uongo.
 
Justine Kalikawa miaka ya 90 mpaka 2000s Alikuwa mwimbaji mzuri sana wa Regge na zilipendwa sana..
Hasa ile "panapofuka moshi" na "wamachinga"
Hivi huyu jamaa yuko wapi
Justine Kalikawe mwanamuziki wa Reggae kutoka Kagera, nilisikia kwamba alifariki dunia muda tu! Kama kumbukumbu zangu ziko sawa!

Nyimbo nyingine mbali na "panapofuka Moshi, zima moto chini" "wamachinga"

Pia aliimba "Maisha sio Ndoto" , "ningekuwa na Mabawa" etc
 
Duh sikujua kama kafa aisee..
Nilikuwa napenda sana nyimbo zake huyu jmaa alikuwa ana regge nzuri na imepoa kiasu fulani hivi
 
Wako wapi victor mwambalasa, aloyce kimaro, lucas seleli na wale wenzao kwa pamoja waliitwa mitume kumi na mbili wa kupinga ufisadi enzi zile za siasa za kuvua gamba za chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom