Mada ya wanyama

Kuna Aina flani ya breed wao hawatoki kutafuta nje hata kama utakuwa hujamfunga, na wakigundua Kama hujawafunga mnyama yeyote atakayekatiza mbele yake ye ni halali yake. Mfano ni American pit bull na Rottweiler
Mbwa ni rafiki wa kweli kwa binadamu.Hata usipokuwa na chakula ataendelea kuishi kwako ingawa chakula atajitafutia nje.Ila paka ni mtafuta fursa akikosa msosi ataondoka.
 
Nikikaona haka kamnyama hua najua kanaitwa King Julian.

NB. Hivu madagascar kuna Penguins???
Unajua huyo jamaa tuko naye jamii moja! Wote ni primates. Nafikiri hata akili zitakuwa za kama primates wengine, sokwe, Orangutans nk. Labda ndiyo maana kalipewa uking!😄😄.
 
Unajua huyo jamaa tuko naye jamii moja! Wote ni primates. Nafikiri hata akili zitakuwa za kama primates wengine, sokwe, Orangutans nk. Labda ndiyo maana kalipewa uking!😄😄.
Hahaaa Huu utani sana, hata kama tuko kundi moja ila hapana.
Nikikaona hapo naisikia kabisa sauti yake (Ya Sacha Baron Cohen)

"It's no Use Maurice, I'm the King without a kingdom. What the point of admiration"😆😆😆
 
Hapa mada inaweza hama kwenda kwingine. Tunaenjoy mada ya wanyama na tabia zao hapa,
 
Nimemkumbuka na Antlion( Chungu simba). Larva wa huyu bosi huwa anachimba kashimo ardhini na yeye anajifukia pale katikati ya shimo. Kuta za shimo zinakuwa ziko kwenye angle fulani. Kwenye zile kuta anajaza mchanga. Sasa sisimizi au siafu ikijichanganya na kudumbukia mpe inashindwa kutoka. Ule mchanga kwenye ukuta unakuwa unaporomoka kila akijaribu kutoka. Basi hapo jamaa anatoka na kumtafuna kisha anarudishia mchanga na kusubiri tena windo.
 
Huu uzi kwakweli umeahibisha ubongo wangu. Nimejua vitu vingi Sana.

Lakini pia kuna mdau nimejikuta nampenda bure, amekuja na interpretation ya biblia iliyotulia, sijawahi iona popote.

Yesu hakupaa mbinguni kumbe. Sijui kwanini watu wanapenda kupotosha.
 
Haha Mungu kampa kila kiumbe jinsi ya kupata chakula chake. Huku kwetu tunamwita fukufuku
 
Kuna samaki anaitwa electric eel, huku kwetu bongo tunamwita mkunga anapatikana katika mabwawa na mito mingi Africa na America ya kusini. Huyu samaki ana uwezo wa kuzalisha nguvu za umeme mpaka kufika Volts 600 kwaajili ya kuliua windo lake au kuwaweka adui zake mbali na yeye au kushambulia pale anapohisi kuna hatari.
Binafsi nishawavua sana hawa samaki nikiwa teenager katika makuzi ya kuvua vua samaki katika mabwawa lakini sikujua kama ana uwezo wa kukupiga shoti ambayo inaweza kukusababishia shock nakuwa drown hata katika kina kifupi cha maji. Kuna cases chache mpaka sasa za vifo vya binadamu vilivyosababishwa na huyu mjuba.
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    17 KB · Views: 41
[emoji298] 600?
 
Hili dude wabongo wanaliita chunusi,wanaamini kwenye maji kuna jini linalofyonza damu,kumbe ni huyo electric eel anakugonga shoti unakufa halafu tukikupata tunakukuta umepungukiwa damu sababu ya ile shoti,hapo wabongo ndio wanasema jini lilikunyonya damu[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…