Kuenda kwa tumbo ni katika maana hiyo hiyo ya "figurative" (symbolic), unaposema fulani "atasota", kusota kwa maana ya moja kwa moja ni kutembelea makalio kwa kujiburuza ardhini lakini maana ya figurative ni kupata shida kimaisha nk, hivyo kusota ni sawa na kutembelea tumbo kwa nyoka kuhusiana na binadamu.
Maana nzima ya nyoka kutembelea tumbo katika muktadha wa Adam na Hawa ni huyo nyoka (mtu muovu) atapigika, atasota nk, katika maisha.
Watu wengi sana tunakosea sana kutafsiri baadhi ya maneno ya kiroho "literally" ni makosa kama hayo ndiyo yamepelekea kuamini KIMAKOSA kwamba Yesu alikufa akafufuka na akapaa KIMWILI mbinguni na yupo hai hadi hii leo huko juu, imani potofu kama hiyo hata Wayahudi walikuwa nayo kabla hata Yesu hajazaliwa, wao waliamini kwamba Nabii Eliya alipaa juu mbinguni na angeshuka kabla ya Masiha (Yesu) hajatokea, Yesu alipotokea wakamuuliza; je mbona Eliya hajashuka kutoka mbinguni??, Yesu akawajibu Yohana mbatizaji ndiye Eliya na mwenye masikio asikiye!!., hivyo sasa imani potofu ya watakatifu kupaa mbinguni kidhahiri ilianza kitambo sana ila tu watu wanashindwa kujua ni nini maana ya mtu kupaa mbinguni katika lugha ya kiroho, kupaa mbinguni maana yake ni kusalimika kwa uwezo wa mbinguni (uwezo wa Mungu) kutokana na shida, karaha, mateso nk, abayopata mtu, kama tujuavyo Yesu alipata Mateso makubwa chini ya mafarisayo nk, hivyo alinusurika na kuhamia nchi nyingine akiwa yeye na mama yake na Mariam Magdalene mkewe. Bi Mariam Mama Yesu alifariki wakiwa njiani na alizikwa chini ya foot of Mt Muree in Pakistan (Mary's mountains, named so after her)
Walihamia Kashmir na huko aliendelea kuhubiri injili kwa Wana wa Israeli waliopo huko na akazikwa huko na kaburi lake lipo huko Kashmir, Shrinagar, mtaa wa Khanyar, Watalii kibao huenda kuzuru hilo kaburi lililo maarufu sana huko Kashmir, Kwa habari pana ingia Youtube orGoogle Rozabal shrine.
Nimeamua kueleza kwa ufupi jambo hilo kuonyesha jinsi watu wanavyopotoka kwa kusoma na kuelewa maandiko ya kiroho "literally".
"Kushuka" (kuja) tena kwa Yesu duniani nako kuna maana yake Kiroho, sitaweza kueleza kwani ni habari ndefu sana.