Mada ya wanyama

Ni kweli, nyoka tunapishana nao tu mara nyingi bila kujua na wala hawatufanyi kitu kwa kuwa tunapopishana nao bila kujua wao wanapata taarifa kwamba hatujamuona ila ukijua tu wanapata taarifa kwamba umeshajua au ukimkanyaga wanapata taarifa kwamba umemuona hivyo huchukua tahadhari kwa kukung'ata.
 
Hivi hawa ndege wanaliwa? Mana nyama yake c itakuwa kama umechinja ng'ombe.
 
 
Mkuu;
1.Kinyonga:
Kinyonga ni mnyama mwenye Upendo wa hali ya juu. Anapofikia hatua ya kuzaa, hupanda juu ya mti mrefu sana na hujiachia/hujidondosha na akifika chini hupasuka/husambaratika ili watoto watoke. Anakufa kwa ajili ya watoto kuishi. Anajifanyia caesarian section Binafsi
2. Mbwa koko:
Mbwa mwenye watoto hubangaiza na akirejea /akirudi pale kwenye kundi la watoto huwatapikia chakula alichookoteza na maisha yanasonga. Usipolielewa hilo utakereka na kuona kinyaa sana kwa Tabia hii.
3.Binadamu:
Binadamu hapendi kuambiwa UKWELI kwamba yeye ni mmojawapo wa WANYAMA tena mnyama hatari zaidi Duniani. Bora Ukutane na kundi la Simba kuliko kukutana na Binadamu mmoja hususan adui yako!
 
Binadamu hapendi kuambiwa UKWELI kwamba yeye ni mmojawapo wa WANYAMA tena mnyama hatari zaidi Duniani. Bora Ukutane na kundi la Simba kuliko kukutana na Binadamu mmoja hususan adui yako
 
Binadamu hapendi kuambiwa UKWELI kwamba yeye ni mmojawapo wa WANYAMA tena mnyama hatari zaidi Duniani. Bora Ukutane na kundi la Simba kuliko kukutana na Binadamu mmoja hususan adui yako[emoji1545]
 
Dah! Huwezi amini ndy nimejua leo basi hawa samaki kigoma wako wengi
 
Tasmanian Devil,
Miongoni mwa wanyama wakorofi sana, usidanganyike na kisura chake kicute ukakutana nacho mtaani uende kukipetipeti. Wanaishi kibabe na hawana hofu na hupigana hata na mbwa wakubwa bila kujali size yao.

Ubabe unaanza tangu siku wanapozaliwa. Jike anaweza kuzaa vitoto 20-30 au zaidi ila ana chuchu nne tu hivyo vitoto vinapozaliwa tu vinaanza kushindana na kupigania chuchu vinyonye. Kwa hali hii asilimia kubwa ya vitoto vinakufa vinapozaliwa tu na vingine havitaishi kufika ukubwani.

Ukubwani nako ni ubabe. Jike atapandwa na dume mbabe tu hivyo madume watapigana na kushindana kupata mke. mshindi atapata nafasi ya kuongeza kizazi chake and the cycle continues.
 
Bull Shark

Papa mkorofi na aggressive kuliko wote. Inasemekana huyu ndo shark hatari kuliko hata Great White Shark ambaye wengi wanamchukulia kama mfalme wa bahari. Probability ya kung'atwa na bull shark ni kubwa kuliko kung'atwa na Great White. Hawa wanaishi karibia maeneo yote,

Bull shark anaweza kuishi baharini na pia kwenye mito na maziwa (saltwater na freshwater kote anatamba) tofauti na shark wengine.

Kama shark wengine wengi wanaozaa watoto na sio wale wanaotaga mayai, embryo wa shark wakiwa tumboni huwa hawana source ya chakula kingine hivyo wanakulana wenyewe kwa wenyewe mpaka wachache tu ndo wanabaki wakati wa kuzaliwa. Mara nyingine wanakulana mpaka wanabaki wawili tu au hata mmoja tu ndo anafanikiwa kuzaliwa.

Hawalelewi na wazazi. Anapozaliwa tu anaanza kujitegemea (tena anabidi asepe fasta tu akizaliwa maana kama mama yake ana njaa anaweza kumgeuza chakula 😁😁).

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…