Madai ya Katiba Mpya: inawezekana CHADEMA wana baraka za Rais ila kwa siri kubwa

Madai ya Katiba Mpya: inawezekana CHADEMA wana baraka za Rais ila kwa siri kubwa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Jicho la tatu linaniambia kuwa huenda Mama ana agenda ya Katiba Mpya ila anajua wenzake hawaitaki, hivyo kaamua kuwatumia CHADEMA kwa siri kubwa kuamsha madai ya Katiba Mpya.

CHADEMA wanaweza kuendelea na hii agenda bila vikwazo huku MATAGA wakiwa hawelewi halafu mwisho wa siku Mama anawaunga mkono CHADEMA.

Ingawa CHADEMA wanaonekana kumshambulia Mama, inawezekana ni mkakati tu wa kisiasa na ni siri ya viongozi wachache na wa wa juu wa CHADEMA.

Sitashangaa pia yakaibuka makundi mengine kuunga mkono hoja ya Katiba Mpya.

Katiba Mpya hata Wazanzibar wanaitaka kwani itasaidia kuondoa au kupunguza kero za Muungano.

Mama ni silent killer.
 
Du!tutasikia mengi
Wabunge Covid 19 baraka za nani kwa siri ya hali ya juu.
 
Wewe umeona mbali unajua hata suaka la bandari ya Bagamoyo kwanza alilipenyeza kwa Spika Ndugai Ndio mkaona Ndugai anamshambulia Hayati Magufuli kuwa alipotoshwa wakati Magufuli mwenyewe huwa ni mfuatiliaje wa kusoma kila kitu.

Lakini pia akapenyeza agenda kwa mwenyekiti wa TPSF kuwa private sector inaishauri Serikali iendelee na mradi wa Bagamoyo na yule mama wa TPSF akaiweka kwenye agenda..Baadaye Rais Samia akajibu serikali imeanza jitihada za kuzungumza na muwekezaji wa bandari na kwa masharti waliokiwa wameomba ya umiliki ya miaka 99 na kulipwa kama watatengeza hasara.

Lakini hata hili la covid akawadanganya ametengenza kamati ya covid imushauri wakati yeye mwenyewe aliishaamua kuleta chanjo.

Jiulize kamati ya kukaa wiki ikaja na mapendekezo yote kama ya WHO. So nakubaliana na hili la katiba kunasri kati ya mama na wachache chadema
 
Wewe umeona mbali unajua hata suaka la bandari ya Bagamoyo kwanza alilipenyeza kwa Spika Ndugai Ndio mkaona Ndugai anamshambulia Hayati Magufuli kuwa alipotoshwa wakati Magufuli mwenyewe huwa ni mfuatiliaje wa kusoma kila kitu...
Wabongo sio watu wa kusoma alama za nyakati. Mama ni mjanja sana.

Lissu akirudi, labda ndio watu wataanza kuelewa/kuunganisha dots.
 
Yapaswa mchakato uende fasta. Katiba mpya yafaa izuie kuibuka uchato. Maana ni vipi akiibuka mchato mwingine kisha akosekane wa kumpeleka kwa haraka kule kwa wengi?
 
Jicho la tatu linaniambia kuwa huenda Mama ana agenda ya Katiba Mpya ila anajua wenzake hawaitaki, hivyo kaamua kuwatumia CHADEMA kwa siri kubwa kuamsha madai ya Katiba Mpya...
Kama ni SIRI siungekausha tu Brother.
Uoni kama unamchongea Mh. Mbowe kwa kutoa SIRI kwako na wewe kuitoa hadharani?
 
Poa ikiwa hivyo lakini huyo mama na kauli zake sina imani naye kabisa. Kama analiunga mkono hilo la katiba mpya ya rasimu ya Warioba sioni kwanini afanye kificho.

Jicho la tatu linaniambia kuwa huenda Mama ana agenda ya Katiba Mpya ila anajua wenzake hawaitaki, hivyo kaamua kuwatumia CHADEMA kwa siri kubwa kuamsha madai ya Katiba Mpya...
 
Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania, asema Prof. Issa Shivji
 
Ukisikia mtu anafikiri nje ya boksi ndiyo huku.

Mleta mada kwa uelewa wako huu kwa vyovyote vile utakuwa siyo mwanachama, mshabiki wala mkereketwa w CCM.
 
Poa ikiwa hivyo lakini huyo mama na kauli zake sina imani naye kabisa. Kama analiunga mkono hilo la katiba mpya ya rasimu ya Warioba sioni kwanini afanye kificho.
Wenzake kwenye chama hawataki kusikia kabisa hii habari hivyo ni lazima atumie makundi yaliyo nje ya chama chake.

Narudia, huu ni mtazamo wangu kwa jinsi navyomsoma Mama.
 
Haina mashiko Mwafrika anajiangalia yeye na familia yake,unataka kusema Samia anawapenda sana wa Zanzibar aaah wapi!!!
 
Aliye sababisha kuwepo na mhamuko wa Katiba ni matendo ya Magufuli.
 
Ukisikia mazungumzo baada ya habari ndio haya. Haya tuendelee kupeana matumaini hewa hapa jukwaani.
 
Kama ni FITA basi iwe ni FITA TU!

Wenzake kwenye chama hawataki kusikia kabisa hii habari hivyo ni lazima atumie makundi yaliyo nje ya chama chake.

Narudia, huu ni mtazamo wangu kwa jinsi navyomsoma Mama.
 
Back
Top Bottom