Hayo ni ya mwanzo tu. Yapo mambo mengi ya kupigania. Kubwa ni uwanja sawa wa kufanya siasa. Hata iletwe katiba ya marekani, kama utawala utakuwa huru kuivunja ni kazi bure.
CAG analindwa na katiba hii hii lakini wamemfukuza kwa madai feki kuwa amemaliza kipindi chake.
Mikutano na maandamano ni haki ya kila mwananchi, lakini imezuiwa kinyume kabisa na katiba.
Lissu alipigwa risasi mchana kweupe, na bado yupo hospitali, lakini wakadai hawajui alipo, wakamvua ubunge.
Wagombea wote wa vyama vya upinzani wameenguliwa kwa madai kuwa wamekosea kujaza fomu, bila ushahidi wa makosa kuonyeshwa.
Vyombo vya habari vya uma vimegeuzwa vyombo vya kuifanyia CCM propaganda na kumsifia rais masaa 24 kinyume na katiba na taratibu za utawala bora.
Pesa zinachotwa kwa matrilioni tukiambiwa zimeenda kununua ndege bila kufuata taratibu za kisheria za manunuzi, na bila bunge kuishinisha bajeti husika.
Huu ni upuuzi mtupu.