Uelewa mdogo na unyonge wa wananchi ndicho chanzo cha viongozi walio madarakani kutupuuza wananchi. Katiba mpya wananchi tuliiona kwamba ni jukumu la viongozi wa vyama tukisahau kuwa kuna wananchi wengi ambao si wafuasi wa vyama vya siasa ambao nao pia wanaihitaji katiba mpya. Nchi zote duniani zinatakiwa ziongozwe kwa matakwa ya wananchi na wananchi wasiporidhika wana haki ya kuwaondoa madarakani viongozi wao. Tanzania jukumu la kupata katiba mpya tumewaachia viongozi wa vyama! Hili ni kosa kubwa, ni sisi wananchi kwa umoja wetu ndiyo tuitake serikali itupe katiba mpya.