Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Siku ya jana kuna madai toka kwa mkurugenzi mkuu wa TRC kuwa anayo majina ya watu wanaoihujumu treni ya SGR, madai haya ni mazito na TRC haina uwezo wa kuyashughurikia kwa sababu yanahusu jinai.
Kwenye madai hayo kuna taarifa ya kuwa wapo watu wanakata waya za umeme ambao ndiyo nishati ya hiyo treni hivho kusababisha ishindwe kutembea, uhalifu huu ni mkubwa kwani umeme huo unatoka kwenye gridi ya taifa hivyo kunaweza kusababisha uharibifu kwenye gridi hiyo.
Ninashauri waziri mkuu amtake mkurugenzi Kadogosa ampe ushahidi wa madai hayo ili avitake vyombo vya dola kama polisi na usalama wa taifa walishughurikie haraka kabla madhara makubwa hayajatokea.