Madai ya Polisi kuwabambikia kesi watuhumiwa yamejithibitisha katika kesi ya Kabendera

Suluhisho, tuwe na sheria inayowapa dhamana watuhumiwa wote isipokuwa wa mauaji. Na kisha tuwe na sheria inayowapa ukomo wa miezi 4 Polisi kufanya upelelezi. Miezi hiyo ikipita, hawajakamilisha upelelezi, kesi ifutwe. Inaweza kufunguliwa tena siku wakiwa na ushahidi.

Hizi sheria za sasa, ukiwa na Waendesha mashtaka wenye roho za kishetani kama ilivyo sasa, nchi nzima itafanywa kuwa ya kishetani. Nchi inayoonea watu. Nchi inayofurahia mateso ya watu badala ya furaha ya watu. Nchi inayowafanya watu waishi bila amani mioyoni mwao.

Sisi wakristo tunaamini Kristo alileta amani, ndiyo maana hata alipofufuka na kuwatokea mitume wake, neno lake la kwanza lilikuwa, 'AMANI IWE KWENU'. Kwa hiyo Mungu anataka tuwe na amani. Ukiona mtu anataka msiwe na amani, ujue huyo ni ibilisi katika umbo la binadamu. Hawa waendesha mashtaka ni ibilisi. Watu wa Mungu hawastahili kushikamana na ibilisi. Laana iwe juu yao na vizazi vyao. Hii kazi naona imelaanika nchini mwetu.

Lakini ukweli ni kuwa, waendesha mashtaka ni mikono tu ya utekelezaji, anayehusika hasa ndiye anayetaka kuikata mikono yake. Mh. Rais Magufuli tunakuomba usimamie haki kwa dhamira na moyo, na wala usitawaliwe na ulaghai.
 
Kiuhalisia hawa jamaa na mkuu wao pumzi imeanza kukata. Chezea Marekani wewe!
 
Pascal Mayalla, Tunaweza kusema mengi. Yawezekana kweli makala za Mayala zilifunua macho ya watawala, lakini itakuwa ukosefu wa utii kwa nafsi yangu, kwa namna yoyote ile kufikiria kuwa Mayala alizileta makala zile ili Kabendera akamatwe.

Na sijui kama kuna mtu anayesema hivyo kwa dhamira ya moyo wake. Huenda wengine wakishachukizwa na mawazo fulani ya Mayala, wanaona njia ya kumkomoa kisaikolojia ni kumhusisha na mateso ya Kabendera. Jambo ambalo siyo jema.

Mayala, kwa kuwa hukuwa na dhamira hiyo, tembea kwa amani.

Mzee Mwinyi alipokuwa anaongelea uwezekano wa kufanya makosa katika kutekeleza sera ya ubinafsishaji, aliwahi kunena, "Hata kama utafanya kosa, kama dhamira yako ilikuwa njema, Mwenyezi Mungu hulitakasisha kosa hilo. Lakini kama ulikuwa na dhamira mbaya, hata kama ulilolifanya likaja kuonekana ni jambo jema, Mwenyezi Mungu hulitia unajisi".
 
Usiombe uwekwe ndani Kwa kuonewa utaumia Sana , Nilishawahi kuwekwa GEREZANI Kwa muda wa miezi minne bila kosa lolote, nilipata ujasiri wa kipekee
Pole sana ndugu yetu. Uonevu ule ukupe ujasiri wakati wote kuwatendea haki watu wote, nawe utabarikiwa maradufu. Kumbuka, hata katika ubaya, kuna mema humea.
 
Mystery,

Mimi naona ni afadhali iwe hivi ili atoke huko, japo hawa policcm hujui kama walisha fanya yao juu ya kaflug, na hawana nia tena ya kuendelea kushikilia hasije akawafia gerezani.
 
Waendesha Mashtaka hawajaomba kutoendelea kesi kwakuwa hawana Maslahi nayo, bali, ni kwa kuzingatia sheria inayoruhusu washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kufanya mazunguzo ya kukubaliana kulipa.

Kabendera ameomba kulipa na waendesha mashtaka wameomba kwakuwa mazungumzo Kati ya Kabendera na DPP yanaenda vizuri. Muwe mnaelewa, muache kupotosha!
 
Mystery, Umeandika vizuri lkn bwana mkubwa yy ndio chabzo kikubwa anae sababisha ilikuaje awambie watuhumiwa warejeshe pesa wasemehewe kesi ya kuhujumi uchumi yani hata mahakama haijathibitisha kama hawa ni watuhumiwa jengine waliloona kama hapa wameshashtukiziwa na mabeberu.

Ni kuhusu ishu ya Makonda kuzuiwa marekani na waziri wa mambo ya nje ya marekani kasema ushahidi anao kuhusu ishu anazofanya makonda na kabendera kila akienda mahakamani mabalozi wa nchi za njee wanawasili wakajua kama hiyi ishu imeshtukiziwa sasa bwanamkubwa anajitoa yy kama yy ili awangushie wenzake msala lkn marekani kila kitu wanajua wanao husika na kesi hizo za kubambikizwa watu wasiyo na hatia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bams,
Mtu asikamatwe kama ushahidi haujakamilika.Hili ndilo linalotakiwa
Ni kweli kabisa Mkuu Bams

Utashangaa hao mapolisi wanampeleka mtuhumiwa mahakamani, halafu kila kesi ikitajwa kwa muda wa miezi 6 mfululizo, wanadai kuwa ushahidi haujakamilika!
 
mBINYO wa mabeberu unazaa matunda
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusianze kutabiri mambo kabla hayajawiva.
Hiyo plea bargaining inaweza kutushtua kwa jamaa kukiri na kuwataja wahusika wengine ambao hawapo mahakamani kwa sasa.
 
Magufuli hawezi kujikosha kwenye hili ni mmoja wa nguzo kuu za kubambikia watu kesi , ameshiriki kuamuru watu wabambikwe kesi ikiwemo kesi ya uzushi ya viongozi wa Chadema
 
Tusianze kutabiri mambo kabla hayajawiva.
Hiyo plea bargaining inaweza kutushtua kwa jamaa kukiri na kuwataja wahusika wengine ambao hawapo mahakamani kwa sasa.
Uongo utakusaidia nini wewe , Kapuku Kabendera anaweza kutakatisha nini ikiwa mama yake kafa kwa umasikini ?
 
Uongo utakusaidia nini wewe , Kapuku Kabendera anaweza kutakatisha nini ikiwa mama yake kafa kwa umasikini ?
Hivi sasa tunanyima uhuru kuwa na mawazo tofauti kwenye jambo lolote???? Au ndiyo mila mnayoijenga kuwa tuwe 'asante mzee kimawazo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…