Madai ya Polisi kuwabambikia kesi watuhumiwa yamejithibitisha katika kesi ya Kabendera

hatus
Sisi hatusemi kuwa Jiwe hana makosa............

Anayeagiza na anayetekeleza amri hiyo wote wana makosa na laana itawatafuna na wala haitawaonea huruma
 
Anayewatuma hamumpi lawama, analaumiwa ambaye katumwa, tuache ujinga . Huu unafiki hautusaidii. Marehemu Mtikila alishasema hao ni mbwa wa ccm.
 
Maskini Kabendera! Au ndio maana gazeti alilokuwa analiandikia la the economist lilimwandika jiwe vizuri kuwa ataendelea kutawala kwa kipindi kingine? Au nalo lilipewa maagizo ya kusifu kwa sharti la kuachiwa kijana wao? Nimejaribu kuwaza kwa sauti tu msinishambulie kwa akili zangu kiduchu!
 
Hahaha simsafishi yeyote hapa, kila hoja huwa ina majibu yake mimi nili comment kwa Pascal Mayalla, na sioni kwanini wote tuwe na mtizamo unaofanana kwenye kila kitu.

Binafsi nilijaribu kuangalia the otherside, hata kama rais ana husika nilidhani pia kulikuwa na uhusika wa marehemu Mengi kwenye hili somehow,I thought.
Sikumtetea yeyote na hata hilo nilisema sina ushahidi ni hisia zangu tu,bahati nzuri Pascal Mayalla aliishaandika kuhusu hili huko nyuma.
 
Misimamo ya magazeti ya mabeberu ni tofauti sana na hapa Bongo

Siamini kuwa gazeti kubwa kama The Economist, likubali "pressure" ya watawala wetu
 
utaratbu wa kijesh uko hv
"ukishapewa order na mkuu,ww ni kutekeleza" na sio kuanza kusema oooh hapa sjui weled sjui sio weled hakunaga hcho ktu. no time for negotiation
Sent using Jamii Forums mobile app
 
L
utaratbu wa kijesh uko hv
"ukishapewa order na mkuu,ww ni kutekeleza" na sio kuanza kusema oooh hapa sjui weled sjui sio weled hakunaga hcho ktu. no time for negotiation

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini katika safari ya kwenda kule kwenye mahakamani ya kimataifa ya The Hague kwa yule mwanamama Fatou Bensouda, hakutakuwa na "excuse" kuwa Mimi niliagizwa na Bosi wangu
 
Samahani, nini kilitokea kati yao!?
 
Mbinyo wa Pompeo hamna kitu.
Bila Pressure kutoka Nje Kabendera ataozea Jela

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Paskali...
Ni Uhaini Kutaka anayewatuma Polisi alaaniwe.
Mwenzako aliota akaishia kukaa Jela Miezi minne

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Samahani, nini kilitokea kati yao!?
Ni story ndefu, ila nadhani tumuombe Pascal Mayalla kama atapendezwa aandike kwa kirefu, mimi nilikuwa msomaji na ila nakumbuka hicho kisa kili mtibua sana marehemu Mengi, na hata serikali.
Matatizo ya kabendera na serikali yalianzia hapo, maana uhamiaji wali mtifua sana baadaye wakachoka naye wakamuacha. Na ndio maana lilipoanza tena uhamiaji walisingiziwa na wao wakajibu kwamba wao hawana sababu yakumteka na kuhoji uraia wa kabendera, ikagundulika kumbe walikuwa ni wasiojulikana ndio walikuwa naye, baadaye tukasikia kahujumu uchumi, na kutakatisha pesa, na ukwepaji kulipa kodi.
Nadhani hii ndio kurasa za mwisho wa kitabu, inabidi uanzie mwanzo kuelewa misukosuko ya kabendera, mimi nakumbuka alipotoa ushahidi against marehemu Mengi dhidi ya wazungu wale waingereza, jamaa alionekana siyo mzalendo, na hakuwa na shukrani, na walisema kalipwa na serikali ya uingereza wengine walisema wale wazungu walimlipa pesa nzuri.
Ila wapotoshaji tuka muhusisha Pascal Mayalla na matatizo ya kabendera, ila nahisi ni AMA kutokujua au kufakamia hoja bila kujua kiini na historia ya muhusika.
Muombe pascal Mayalla aandike vizuri, hili pia linaweza ku clear air kuhusu wale walokuwa wakisema yeye ndiye aliye mchomea kabendera kwa serikali na kwa wasiojulikana.
 
Paskali...
Ni Uhaini Kutaka anayewatuma Polisi alaaniwe.
Mwenzako aliota akaishia kukaa Jela Miezi minne
Sent from my SM-A207F using Tapatalk
Itakuwa ni uhaini only if anayewatuma unamjua, lakini kwa vile humjui, mimi nakuhakikishia kuwa ataalaaniwa na baada ya kifo, atafanywa kuni!.
NB. Please naomba msianze kupiga ramli chonganishi, kwa kuwadhania watu bure, umdhanie ndiye, siye, na usiye mdhania kabisa ndie!.


P
 
Mkuu, Nina uhakika kabisa unamjua anayewatuma.



Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Hata kwenye maandiko matatifu tabia ya polisi kukosa uaminifu imeandikwa
 
Hahaha sio karma tena kaka?!
 
It's true ni kweli hili la Kabendera na Mengi nalijua vizuri, kwa vile Mzee Mengi ameishatangulia mbele ya haki, naomba tumuache apumzike kwa amani, tukianza kufukua mambo humu, mtu aliyeheshimika na kuonekana kama malaika kwa wema wake, anaweza kugeuzwa shetani.

Ila Kabendera ni mkweli daima!, kwenye ushahidi ule alisema kweli tupu!. Ukiwa mkweli too much kwenye jamii iliyozoea uongo, utaonekana an enemy of the people!.

Hata mimi ni mtu mkweli kihivyo, and there is a price to pay!, kiukweli Kabendera alifuatwa na wasiojulikana, salama yake ni CCTV cameras nyumbani kwake!.

Tena hicho kilichomtokea aliwahi kulizungumza tukiwa naye kwenye mjadala wa huu organized by jamiiforums, mimi ndio nilikuwa moderator.

P
 
Mkuu, Nina uhakika kabisa unamjua anayewatuma.
Sent from my SM-A207F using Tapatalk
Simjui anayewatuma, ila kwa vile mimi ni mwandishi mwenye uwezo wa kufanya investigative journalism, ningeombwa kusaidia, ningesaidia na nimeishawahi kutangaza wazi humu jf, ila sijaombwa.



P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…