Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
1,710
Reaction score
8,690
Wasaalam,

Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.

Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"

Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿

Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi LATRA ahsante kwa ushirikiano.

IMG-20250325-WA0083.jpg
 
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
 
Abiria pia tunachangia kwa kukalia kimya huu upuuzi wanaoufanya makondakta. Mi si mpandaji sana wa daladala ila mwezi uliopita nilipanda daladala ya makumbusho - mbezi kupitia goba mida ya jioni, kufika mwenge konda akawaambia wanafunzi wasubiri abiria wengine wapande kwanza... abiria walivyopanda konda akafunga mlango akawagomea kuingia gari ikaondoka, aisee nilimtukana yule konda na dereva wake hadi wakakosa cha kuongea..kilichonishangaza abiria wengine nao kimya hata hawasemi kitu kwa kile kitendo.. nilitamani nitukane bus zima. Daladala ilipofika tangibovu ndio wakajishtukia wakapakia wanafunzi maana kwa jinsi nilivyowamind walihisi sitowaacha salama naweza wachomesha.
 
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Acha zako wewe kwani wanafunzi wanasafiri muda wote? Yaani asubuhi au jioni tu washindwe kupakia wanafunzi hata watatu kisa hesabu ya boss ? Nyie ndio mnakaliaga kimya huu upuuzi
 
Mbona serikali haiamuru wanafunzi kula mgahawani Bure? Kwani watoto hawapati njaa shuleni
Kwanini serikali iwaonee daladala, serikali haijui hii ni biashara
Msimamo wangu: ili kuepuka usumbu wanafunzi walipe nauli kamili
 
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Taasisi za huduma hizi Zina viongozi wake, hizo changamoto zote waende huko LATRA wawasilishe wajadili. Ndiyo maana ya kutoa huduma kwa mujibu wa sheria iliyokusajili. Kumnyima mtoto mdogo huduma ni kuvunja Sheria uliyoitii ikusajili. Na ukivunja Sheria hatua zake ni kuwajibika kisheria. Hivyo, dawa ya kukwepa yote haya ni kurudi kwa msajili na kuzungumza. Mambo ndiyo huenda hivyo tafadhali na siyo vinginevyo.
 
Na ushauri wangu ni kuwa, nyie watoa huduma naamini mliisoma Sheria kuhusu usajili wa huduma zenu hivyo, mnao wajibu wa kwenda kwa msajili na kusema, tuna hoja na ushauri na mapendekezo. Mimi kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Makundi maalumu, huwa natumia muda kuelimisha jamii yote kadri hoja zinavyonifikia. Ahsante Sana kwa ushirikiano wako/wenu
 
Taasisi za huduma hizi Zina viongozi wake, hizo changamoto zote waende huko LATRA wawasilishe wajadili. Ndiyo maana ya kutoa huduma kwa mujibu wa sheria iliyokusajili. Kumnyima mtoto mdogo huduma ni kuvunja Sheria uliyoitii ikusajili. Na ukivunja Sheria hatua zake ni kuwajibika kisheria. Hivyo, dawa ya kukwepa yote haya ni kurudi kwa msajili na kuzungumza. Mambo ndiyo huenda hivyo tafadhali na siyo vinginevyo.
Serikali ni 1 kimsingi serikali iheshimu biashara ya daladala
Wanafunzi wapewe nauli kamili na wazazi wao au wasomee shule za karibu na nyumbani
Wazazi tujifunze kuwajibika Kwa watoto wetu
Mtoto ni wako unataka asafiri Bure,
 
Hawezi kupandishaa gari zima wanafunzi serikali ingeweka walau idadi ya wanafunzi Kila gari konda awapakie...
Konda anatafuta hesabu ya boss wakati wanafunzi anatakiwa awahi shule au awahi nyumban utaratibu uangalie pande zote mbili...
Sasa maoni haya mnatakiwa kuchukua hizo simu hapo mpigie mtoe. Huwezi kusajili huduma kwa mujibu wa sheria halafu uende uanze kutekeleza kinyume na sheria halafu ufikiri umetatua tatizo, utakuwa umejiongeza mwenyewe.
 
Wasaalam,

Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.

Tagu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"

Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿

Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi @latra_tz ahsante kwa ushirikiano.

Ubarikiwe mh Waziri,
Kiukweli makondakta wanawanyanyasa sana wanafunzi asubui na jioni, na cha kusikitisha zaidi abiria watu wazima wanakuwa kimiya wala hawawatetei watoto,yaan baadhi ya watanzania waoga sijui ni kitu gani ,mtu anaona mwenzie au mtoto ananyanyaswa na kondakta ye au wao wananyamaza kimiyaa....

na Latra iweke sheria kali dhidi ya hawa wahuni,tena iambatane na kifungo cha jela kabisa.
 
Hivi Mama, huko kwenye vikao vyenu hamkuwahi kujadili Serikali kununua mabus yakutosha mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya Wanafunzi tu na wazazi wawe wanachangia kiasi fulani labda monthly.

Hii kero ipo miaka nenda rudi toka enzi zile za Tambaza mpaka Leo hapo Dar bado kunashida ya usafiri wa Wanafunzi tu, inamaana mpaka Leo hatuna solution?

Mama shida nyingine kuubwa mashule ya vijijini huko unakuta watoto wako kwenye highway wanaomba lift kwenye malori na magari yanayopita matokeo yake watoto wa kike wanakuwa kwenye hatari kwa hawa wahuni wa malori, na wengine.
Huko mawilayani kutokana na mashule kuwa mbali bodaboda wamekuwa ndio waume sasa wa mabinti. (Hatari sana)

Hili suala la usafiri wa Wanafunzi msiishie tu Dar es salaam hata mikoani sasa mnahitaji kuumiza kichwa, kwangu mimi naona suluhu ni Serikali kuanza school buses kuanzia kwenye miji mpaka mawilayani na vijijini huko.
Kwenye hizi highways mabus ya Wanafunzi yawe yanazungukuka muda wa kuingia na muda wa kutoka.
Kila Mkoa kwenye highways zake unakuwa na mabus yake maana tuna miji mingi mabarabarani, wilayani pia kila kwenye population kubwa inawekwa bus..nk
Huu umbali wanaotembea hawa watoto naamini hata upeo wao unakuwa mdogo mashuleni huko.
 
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
We hauna mtoto bibie lazima uwatetee hao wahuni.
 
Wasaalam,

Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.

Tagu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"

Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿

Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi @latra_tz ahsante kwa ushirikiano.

Kwanini magari ya serikali , STM, STN, STL, DFPA, DFP, SU, PT, nk hayawachukui wanafunzi?
 
Serikali ni 1 kimsingi serikali iheshimu biashara ya daladala
Wanafunzi wapewe nauli kamili na wazazi wao au wasomee shule za karibu na nyumbani
Wazazi tujifunze kuwajibika Kwa watoto wetu
Mtoto ni wako unataka asafiri Bure,
Nadhani umeziona namba za LATRA hapo, ingekuwa vema ukapiga ukatoa maoni. Mimi naelimisha tu utaratibu kwa nafasi yangu kama Waziri wa jamii na jamii mmekuwa mkinitag mambo mbalimbali. Kuhusu dhamana ya kupokea na kufanyia kazi maoni haya, ni mwenye Sheria husika. Ili kwa pamoja muongee muone kifuatacho kama ni maboresho haya
 
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Nakazia.
 
Back
Top Bottom