Mama tutalaumu sana hawa makonda na kuwashushia rungu, tunachopaswa kujua KUNA SHIDA KUBWA YA USAFIRI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NA SERIKALI INAPASWA KUFANYA KITU.
Population imekuwa kubwa kuliko uwezo wa haya mabus, ukiangalia mara nyingi vituoni ni vita Kwa abiria kupanda hayo mabus, mpaka vita inaisha bus tayari limejaa, huyo mwanafunzi unamuweka wapi sasa?.
Mama nenda pale Mbezi kituo cha Mwendokasi asubuhi na kivukoni jioni uone shughuli yake, halafu ufikirie namna huyu mwanafunzi wa shule ya msingi namna anaweza kufit.
Agizeni baadhi ya mabus kwenye hizi mwendo kasi kila route ziwe school bus tu kuendana na ratiba za shule, sisitizeni kwa wazazi kupeleka watoto shule zilizopo jirani na makazi yao..nk