Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
- Thread starter
-
- #21
Uko sahihi kabisa, na hawasemi kwa kuwa wengi unakuta hata hawafahamu Sheria nadhani. Sasa tutakuwa tunatoa elimu ya utaratibu Ili wananchi wote wawajibike kutoa taarifa kwa wakati mahali sahihi Ili basi wahusika wote wakutane eneo sahihi wajadili kwa maendeleo na ustawi wa jamii zetu. Konda wa Leo na mmiliki wa gari Leo kesho wajukuu zake watapanda ya wengine.... Hivyo, tushirikiane kuelewa taratibu kwa pamojaAbiria pia tunachangia kwa kukalia kimya huu upuuzi wanaoufanya makondakta. Mi si mpandaji sana wa daladala ila mwezi uliopita nilipanda daladala ya makumbusho - mbezi kupitia goba mida ya jioni, kufika mwenge konda akawaambia wanafunzi wasubiri abiria wengine wapande kwanza... abiria walivyopanda konda akafunga mlango akawagomea kuingia gari ikaondoka, aisee nilimtukana yule konda na dereva wake hadi wakakosa cha kuongea..kilichonishangaza abiria wengine nao kimya hata hawasemi kitu kwa kile kitendo.. nilitamani nitukane bus zima. Daladala ilipofika tangibovu ndio wakajishtukia wakapakia wanafunzi maana kwa jinsi nilivyowamind walihisi sitowaacha salama naweza wachomesha.
Uhalisia wa mtaani hauko hivoNa ushauri wangu ni kuwa, nyie watoa huduma naamini mliisoma Sheria kuhusu usajili wa huduma zenu hivyo, mnao wajibu wa kwenda kwa msajili na kusema, tuna hoja na ushauri na mapendekezo. Mimi kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Makundi maalumu, huwa natumia muda kuelimisha jamii yote kadri hoja zinavyonifikia. Ahsante Sana kwa ushirikiano wako/wenu
Serikali kwanini msitoe ruzuku kwa hizi daladala ili wawabebe hao watoto pasipo kupata hasara.Na ushauri wangu ni kuwa, nyie watoa huduma naamini mliisoma Sheria kuhusu usajili wa huduma zenu hivyo, mnao wajibu wa kwenda kwa msajili na kusema, tuna hoja na ushauri na mapendekezo. Mimi kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Makundi maalumu, huwa natumia muda kuelimisha jamii yote kadri hoja zinavyonifikia. Ahsante Sana kwa ushirikiano wako/wenu
Sasa hayo maoni si ndiyo Sasa arudi kwa msajili? Asiporudi akaanza tu kuvunja Sheria unadhani akishtakiwa Sheria itamwacha? Hebu na wewe tafakariUhalisia wa mtaani hauko hivo
Boss anakubali hayo masharti lakini kondakta anapewa gari na huo mzigo wa kulipia halafu umpe wanafunzi walipe 200 yeye ataishije
Umehitimisha vema, kwamba sasa nao watoe maoni hayo maana hapa ni taarifa na elimu imekujaLabda matozo yasingekuwa lukuki kwenye mafuta n.k., hawa makonda / madereva na wenye magari wabangaizaji wasingehangaika sana kukusanya kila shilingi ili waweze kukamilisha marejesho ya riba na mikopo kabla ya wao pia kurudi kijiweni kwa kufirisika....
Like I always say ni mengi sana yanakwenda kombo na suluhisho ni majumuisho ya sekta kadhaa ili kupata sustainability ya uhakika...
Uwachomeshe gari yako? Nunua gari afu uwe unapakia wanafunzi, wee vipi? Una wapangia watu mali zao watumie vipi? LolAbiria pia tunachangia kwa kukalia kimya huu upuuzi wanaoufanya makondakta. Mi si mpandaji sana wa daladala ila mwezi uliopita nilipanda daladala ya makumbusho - mbezi kupitia goba mida ya jioni, kufika mwenge konda akawaambia wanafunzi wasubiri abiria wengine wapande kwanza... abiria walivyopanda konda akafunga mlango akawagomea kuingia gari ikaondoka, aisee nilimtukana yule konda na dereva wake hadi wakakosa cha kuongea..kilichonishangaza abiria wengine nao kimya hata hawasemi kitu kwa kile kitendo.. nilitamani nitukane bus zima. Daladala ilipofika tangibovu ndio wakajishtukia wakapakia wanafunzi maana kwa jinsi nilivyowamind walihisi sitowaacha salama naweza wachomesha.
We kinda pakia wanafunzi acha habari zako za kuleta janja janja mkono wa sheria ni mrefu utakunasa tuSerikali ni 1 kimsingi serikali iheshimu biashara ya daladala
Wanafunzi wapewe nauli kamili na wazazi wao au wasomee shule za karibu na nyumbani
Wazazi tujifunze kuwajibika Kwa watoto wetu
Mtoto ni wako unataka asafiri Bure,
We itakua mke wa konda sio bure Cha ajabu mmeo ananing'inia mlangonihuko mdomo ukinula kama choo na hajanunua yakeUwachomeshe gari yako? Nunua gari afu uwe unapakia wanafunzi, wee vipi? Una wapangia watu mali zao watumie vipi? Lol
Labda ungeenda kwa aliyeuliza swali umuulize kwa nini mimi kaamua kuniTag Leo jioni ..... Maana mimi nimepokea nikajibu kadri ninavyofahamu na kama ambavyo huwa napokea hoja zote wakiniTag na kama ninajua najibu. Ahsante Sana kwa ushirikiano wako.Haya Mambo tangia napata ufahamu wa Akili nilikuwa nayaona tokea miaka 20 iliyo pita. Tena naona sikuizi yamepungua. Je mulikosa suruhu miaka yote iyo. Au serikali haina macho au kwa sababu uchaguzi unakaribia.
Acha habari zako magari ya wanafunzi tanzania nzima pesa yake unaijua unataka wananchi tuendelee kukamuliwa mpaka damuKwanin serikali isinunue mabasi special kwa ajili ya wanafunzi?
Yanawekewa utaratiby tu wa muda wa kiwakusanya na kuwapeleka. Pia mda wa kuwachukua.
Serikali inatenga fungu la kuyahudumia magar hayo maana hayatakua na jam kubwa. Yanapita asubuh na jioni.
Kwanza itachangia mahudhurio kuongezeka mashuleni.
Hela ipo, kodi zetu zipo.
Hujambo? Nikuambie jambo ? Maboresho yanapokuwa yanaendelea kwenye eneo lolote , huwa hayafuti Sheria iliyopo kazini hadi hapo Sheria husika itakapofutwa au kubadilishwa. Sasa ni muhimu sana pamoja na maoni tuwe tunakumbuka kutimiza wajibu wa sheria ambayo Iko wakati huo. Ahsante SanaMama tutalaumu sana hawa makonda na kuwashushia rungu, tunachopaswa kujua KUNA SHIDA KUBWA YA USAFIRI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NA SERIKALI INAPASWA KUFANYA KITU.
Population imekuwa kubwa kuliko uwezo wa haya mabus, ukiangalia mara nyingi vituoni ni vita Kwa abiria kupanda hayo mabus, mpaka vita inaisha bus tayari limejaa, huyo mwanafunzi unamuweka wapi sasa?.
Mama nenda pale Mbezi kituo cha Mwendokasi asubuhi na kivukoni jioni uone shughuli yake, halafu ufikirie namna huyu mwanafunzi wa shule ya msingi namna anaweza kufit.
Agizeni baadhi ya mabus kwenye hizi mwendo kasi kila route ziwe school bus tu kuendana na ratiba za shule, sisitizeni kwa wazazi kupeleka watoto shule zilizopo jirani na makazi yao..nk