Chomsky
Member
- Jul 15, 2012
- 31
- 5
Ni muda mrefu Waislam wa Tz wanalalamika juu ya manyanyaso wanayofanyiwa na serikali yao. Hili limekuwa likijitokeza katika siasa, elimu afya na hata nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini.
Mwaka huu serikari inatarajia kuendesha zoezi la kuhesabu watu na makazi kwa wote watakaolala nchini usiku wa kuamkia tar 26. Zoezi litadumu kwa muda wa siku saba. Dodoso litahusisha jina la mtu, umri wake, jinsi, elimu nk. Nyumba za Ibada pia zitahesabiwa!
Ni uamuzi mzuri wa serikari yetu kwa lengo la ku-provide huduma kwa raia wake.
Sasa Waislam wanahoji kukosekana kwa kipengele cha Dini katika madodoso hayo ya sensa. Eti wana-JF wenzangu, kuna ubaya gani serikari kujua idadi ya watu na imani zao? Kwani hii si inaweza kusaidia katika kutoa huduma stahili kwa watu kulingana na imani zao? E.g Kugawa maeneo ya mazishi kulingana na idadi ya waumini fulani katika eneo fulani? (Kumbuka Waislamu, Wakristo nk huzikana kulingana na imani zao hivyo si rahisi ku-share eneo la makaburi).