Msigwa amesema amemuona mwanzo hadi mwisho (Jana aliporudi nchini), kwahiyo ondoa shaka mtoa mada. Jemedali yupo hai na atapona tuendelee kumsihi Mungu.
Madaktari kumruhusu apelekwe Marekani kwa matibabu zaidi, hawawezi na wala hawataweza kuruhusu kutokana na sababu mbalimbali...nikizihisi baadhi;
1. Hawawezi kukubali kushindwa kwa urahisi hivyo
2. Wanalinda heshima ya hospitali yao, isijeikagundulika waonekane wameshindwa kutibu wagonjwa...bora mgonjwa limpate lolote akiwa hapo na si kukiri kushindwa
3. Wamepata fedha nyingi za dharula, kibiashara ni lazima uendelee kumshawishi mgonjwa aendelee kubaki kwako na ikiwezekana umtishe asipate mawazo ya kumhamisha mgonjwa wake
4. Endapo limetokea baya kwa mgonjwa na unapata kigugumizi kumjuza muuguzi wake, na ikaenda zaidi yule muuguzi wake anataka kumhamisha mgonjwa kumpeleka mbele zaidi...basi huweza kutumia busara zaidi za kumfanya asijaribu kufanya hivyo na kumuaminisha kwamba akijaribu kufanya hivyo anaweza akatengeneza madhara zaidi. Mda huohuo wakiwa wanaandaa mazingira psychologically ya kumjuza kuwa mgonjwa wake si riziki.....(nisieleweke vibaya kwa mgonjwa wetu)
5. Mgonjwa watu yu salama na Mungu anaendelea kumlinda, tuzidishe maombi kwa kila mmoja na imani yake. Mtoa mada usilete mada km hizi wakati km huu!!