Madaktari acheni kutuchanganya na hii kauli yenu tata ya Critical but Stable

Madaktari acheni kutuchanganya na hii kauli yenu tata ya Critical but Stable

Nadhani aliyekuhifadhi tumboni mwake kwa miezi Kenda / Tisa Yeye ndiyo anaweza akawa Punguani mkubwa wa kunizidi. Hivi katika uzi wangu nimetaja mahala popote jina la Tundu Lissu? Kwahiyo GENTAMYCINE sina uhuru wangu na haki yangu ya kuhoji Jambo la Kitaalam na kupata ufafanuzi wake? Kwani ni Wagonjwa wangapi humu Mahospitalini huwa tunaambiwa na Madaktari kuwa wapo Critical but Stable?

Utundu Lissu katika huu uzi wangu umekukaje? Umepimaje kama Mimi siuguzi huyo Mgonjwa wangu? Naona unanitafuta Mkuu hivyo endelea tu utakipata unachokitafuta kutoka Kwangu kwani unaonekana unajifanya Kunijua sana halafu unawashwawashwa na Mimi.

Na nilitaka ufafanuzi wa Kitaalam na Kiueledi kabisa kutoka kwa Madaktari humu JF na sikuhitaji maoni ya Wapumbavu wachache wa mfano wako ambao akili zenu zote na muda wote zimekaa tu Kiitikadi za Kisiasa. Nauguliwa je ni dhambi kuhoji juu ya jambo fulani ambalo linanitatiza?

Uvumilivu wangu Kwako unaanza kufikia Kikomo.
Bwana usigombane na watu ngoja nokusaidie "critical but stable " no kwamba hali si nzuri lakini imeimarika au hakuna mabadiliko hasi halibyake haiporomoki wala hapati nafuu significant yaani yupo yupo tu na hakuna jinsi ya kusaidia bali kujaribu ku maintain hali hiyo hoping itabadilika for the better!hapo no pale mnapofanya tiba zote halafu mnabakia kusubiri mwili ujitibu wenyewe !
Kwa kumlizia hofu yako ni sahihi upande mmoja hutokea kesi mgonjwa huna la kumfanya bali ni kusubiri tu aje juu au kufunga kitabu chake cha maisha!
Maombi jamani kwa mgonjwa Gentamycine
 
Sikutegeme kabsa watu watoe maoni kinyume na neno critical but stable, sasa nashangaa watu wanaleta maoni na hisia zao binafsi. .

Ustarabu ni kitu cha bure kabsa hasa unapokuwa unachangia hoja ya MTU ambaye pengine hata humfahamu

Umesoma vizuri? mhuni huyo!!
 
Critical but stable .. Probability yake yakufa nikubwa. Nakuishi kwake kutategemea Mungu + mwili wake unapokea vipi huduma anazopata.
 
...

Sasa Mkuu naomba nikuulize kidogo tu kwahiyo kwa haya maelezo yako ndiyo unataka kusema kwamba huyu Mgonjwa wangu hatofariki? Kwahiyo tuzidi kuwa na imani nae na ikiwezekana niendelee kuhimiza michango hapa kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki ili aendelee kutibiwa kwani tunapanga kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Bahari Barabara na kumtoa hapa Hospitali ya Muhitwo.

Nitashukuru ukinijibu Mkuu.

Maneno yanayotumiwa na hospitali kuwasiliana na jamii kuhusu hali ya mgonjwa, kama nilivyoeleza hapo awali hayana tafsiri/maana ya msingi kisayansi kwamba huwezi kuyatumia kutoa uamuzi wa kisayansi matokeo ya matibabu (kupona au kifo) anayoendelea nayo mgonjwa.

Kwamba michango ya matibabu ya mgonjwa yaendelee au la, maelezo yangu hapo juu yanajitosheleza. Mwenye moyo wa kuchangia ataendelea kufanya hivyo kama madaktari wanavyoendelea na matibu ya mgonjwa katika hali yake yoyote, wakati wote. Hapo ndipo huwa tunajiweka mikononi mwake Mwenyezi Mungu, aliye juu ya yote.
 
Sasa mbona hujatutafsiria kwa Kiswahili Mkuu? Mfano kama Mimi sijui Kiingereza kabisa na naamini nipo na wenzangu wengi tu hivyo ulichokiweka hapo hatujakielewa halafu na hata Kamusi zenyewe hatuna hapa. Wakati ukijiandaa kunijibu labda nikuache tu na swali Mkuu kwakuwa Wewe unajua Kiingereza hicho je kwa hayo maelezo unadhani huyu Mgonjwa wangu ataishi au tuanze kujiandaa kwa huzuni na maombolezo? Naomba maana ya Kiswahili sanifu kabisa cha maneno Critical but Stable.

Nitashukuru ukinijibu Mkuu.
Mkuu ndio maana nimeweka hivyo ili wenye utaalamu wa tiba na udaktari wafafanue zaidi kwa maana najua humu jukwaani wapo na wanaweza kuelezea zaidi kiundani kwa kiswahili.
 
Na kuna Daktari mmoja alinipa Siri kubwa ya wao kupenda kuitumia hii Kauli ya Critical but Stable kwamba huwa wanaitumia sana ili kuwaandaa Kisaikolojia wenye Mgonjwa wao ili hata baadae wakiwaambia ameshafariki basi wasiwe na mshtuko mkubwa
Mpwa Kwa Jina la MUNGU aliye hai LISSU ataishi tu
 
Sasa na elimu yako ya kudownload a.k.a kupima utaweza kung'amua maana ya critical but stable....


Nchi hii ina vilaza waliotukuka
 
Sijui ni kwanini Madaktari wanapenda sana kusema kuwa Mgonjwa fulani yupo Critical but Stable lakini baadae ukija kuchunguza zaidi utakuta tayari huyo Mgonjwa ameshaonyesha dalili zote za Kukata roho / Kufa na mara nyingi wale Wagonjwa wengi ambao huwa tunaambiwa na Madaktari wetu kuwa wapo Critical but Stable huwa wanafariki dunia ndani ya ama muda mchache au siku chache tu zijazo.

Na kuna Daktari mmoja alinipa Siri kubwa ya wao kupenda kuitumia hii Kauli ya Critical but Stable kwamba huwa wanaitumia sana ili kuwaandaa Kisaikolojia wenye Mgonjwa wao ili hata baadae wakiwaambia ameshafariki basi wasiwe na mshtuko mkubwa lakini ukweli ni kwamba Kitabibu duniani kote hakuna kitu cha fulani ni Critical but Stable ila ukweli ni kwamba tayari huyo Mgonjwa anakuwa ameshafikia hatua ya mwisho kabisa ya kukata roho.

Sasa kama kumbe Mgonjwa kuwa Critical but Stable ni sawasawa tu na tayari ameshakata roho / amekufa nyie Madaktari huwa mnaogopa nini kutuambia Sisi tunaouguza kuwa Mpendwa Mgonjwa wetu ameshafariki dunia? Je hamuoni kwamba kuendelea kutuambia hii Kauli yenu ya Mgonjwa yupo Critical but Stable wakati kumbe ameshafariki dunia tayari mnatupa mzigo mwingine tu wa gharama na huenda mngesema tu ukweli mapema basi tungeokoa Pesa?

Kwa mfano Mimi binafsi nina Mgonjwa wangu Hospitali moja hapa Jijini ambaye alishambuliwa vibaya mno na Majambazi huku akiwa ameumizwa vibaya sana mkononi, mguuni, tumboni, kichwani na hadi wakaathiri na ini lake huku akiwa anapumulia mashine, lakini tokea tumkimbize hapo Hospitali leo ni siku kama si ya 15 basi ya 16 yupo ICU na hata haturuhusiwi kuingia kumuona ila ni Madaktari tu pekee ndiyo hutoka nje na kutupa taarifa zake za neno lao kubwa Kwetu sisi Wauguliwaji ni kwamba Mgonjwa wetu yupo Critical but Stable.

Madaktari acheni kutuchanganya tafadhalini huyu Critical but Stable anatutesa sana Sisi tunaouguza Wagonjwa wetu. Nawaomba pia Madaktari mliotukuka na mliopo humu JamiiForums mnipe ufafanuzi wa hii Kauli kwani inatuchanganya sana na hadi kuwafanya Ndugu, Jamaa na Marafiki zetu wengi wasijue la kufanya na huku wengine wasite pia hata kutaka kutoa msaada wao wa michango na huduma zingine kwa huyu Mgonjwa wetu Mpendwa ambaye ni Ndugu yangu aliyejeruhiwa vibaya sana na Majambazi huko Tarime Mkoani Mara ( Musoma ) akiwa anatoka Kazini na anaingia Nyumbani Kwake.

Nawasilisha.
Kwa nini wewe mkuu unatamani kambiwa kuwa Mgonjwa anayeuguzwa Huko Nairobi ameshafariki... Utapata faida gani taarifa hiyo ukipewa? Na kwa nini unajiita Muandishi Mahiri ili hali uandishi wako unajulikana unamlenga nani? Kumbe israel ipo Duniani siku hizi tena kwa binadamu wanaojifanya kuwa ni wema... Basi kama hilo ndiyo Ombi lako basi Hongea na Acha tuendelee kumuuguza. Najua utatokwa na Povu ila kwa nini umnamuombea mwenzio Mauti...?I hate this kind of writting.....
 
mhhh kama sikuelewi kama unawish jambo baya litokee vile !haya !
Achana nae huyo mchawi hamna anachokijua zaidi ya uchawi na anataka lisu afe mgonjwa hata akiwa comma ,kwani mgonjwa akiwa comma ndio anakufa ?wangap wanapona?
 
We Sio mzima na adhma yako haitofanikiwa.
 
Samahani Mkuu haya maelezo yako unadhani yanashabihiana kabisa 100% na kile ambacho nimetaka kukijua au kupata ufafanuzi wa Kitaaluma na Kiuweledi kabisa kutoka kwa Madaktari wabobezi wa JamiiForums? Siku nyingine si vibaya sana kama ukificha Upopoma / Upumbavu japo kwa muda.

Kuugua kwa Tundu Lissu kusiwe Kikwazo kwa sisi wengine katika Kuhoji mambo ya Kitabibu na bahati mbaya sana unaweza kukuta hao hao ambao wanajifanya kumlilia au kuhuzunika na Kuuguliwa Kwake hawajatoa hata Senti moja ya mchango wao Kwake ila juhudi zao ni Kujitutumua tu humu JF.
Huu sio upopoma!!.
Ulichokieleza nadhani kingetokea madaktari wa Nairobi wangewaeleza raia, na hilo neno namna ulivyoliuliza ungeuliza pasipo kuweka maelezo ya ujuaji wako. Wangekuja kukujibu aidha tofauti na unavyoelewa basi ungewauliza zaidi, lakini wewe uombe ufafanuzi huku unaelezea habari za kifo...wala si vyema!!. Utakuwa hutaki kujua bali unaleta ujuaji wako na hapo ndpo ujinga wako ulipolalia
 
Safi sana Mkuu na nazidi kufurahi na Wewe na kuamini kuwa hata uwezo wako wa akili ni mkubwa mno kwani ili kuweza kumuelewa kabisa / vilivyo GENTAMYCINE na Wewe pia yakupasa uwe na akili nyingi na kubwa vinginevyo kila siku utakuwa unaniona Mimi mbaya kumbe Wewe akili zako ndizo mbaya.

Mkuu nakukubali sana na naunga mkono kwa 100% yote uliyoyaandika hapa. Kula likes zangu za kutosha.


Pamoja, mkuu, [HASHTAG]#GENTAMYCINE[/HASHTAG],

Lazima tuwaeleweshe vijana namna ya kuelewa kutofautisha mada na mukhitadha wa bandiko.
 
Back
Top Bottom