Madaktari hasa wa Tanzania rudini maabara tena kuhusu ugonjwa wa U.T.I

Nilikunywa dawa hadi nikasusa tena maana sio poa, ulikuja kupona kwa miti shAmba
 

Siku ukiumwa serious ndio utajua kama ni mauza uza ama vipi...
 
Shida watanzania hawamalizi antibiotics sasa bacteria wanakuwa sugu ndo maana hamponi
 
Pole sana mpendwa,,nadhani kuna kitu watanzania wengi hawaelewi..ni kwamba majibu ya U.T.I unayopata baada ya dk 10 au 20 ukapewa na dawa ni kama tu unacheza kamali..unaweza ukapona au usipone..ila njian nzuri na bora ni kufanya kipimo cha kuotesha.kipimo hiki huchukua masaa 48-72. Hata hivyo changamoto kubwa inakuja kwenye swala la miundobinu na gharama .ni hospitali chache zinazoweza kufanya hicho kipimo cha kuotesha...nakuhakikishia kama U.T.i yako ni ya kujirudia rudia basi bila kufanya hicho kipimo utakunywa dawa sana tu
 
Mmh Hicho ni kipimo gan cha maralia kinachotumia masaa yote hayo.???
 
Acha kulinganisha afya na upuuzi Wa wanasiasa
 
Kama maprofesa wenyewe ndiyo hawa walioko kwenye siasa wako hivyo (eg Kabudi) bila shaka na madaktari wako hivyo. ( Kumbuka ile ya Moi Kichwa Vs mguuu). Tanzania tujitathmini sana. Kusema kweli hatuna kitu sasa hivi. Kuanzia kwenye michezo nk. Siasa yenyewe ndo kabisaa. Kama mtu ana PHd na hajui Kiingereza unategemea nini. Tunajisifu eti hatushindwi vita, hiyo ni hoja ya ovyo hovyo. Jaribu kuingia vitani sasa hivi tuone..
 
mara nyingi wanabambika vipimo,unakuta mtu anacheti fake,unatarajia atakupima kwa uhakika kweli?
 
hata mm nashangaa mkuu,au kuna siri tusoijua na hatupaswi kuijua sisi tunaoitwa wananchi wa kawaida kuhusiana na sera ya malaria haikubariki inapelekea kuhamisha magoli,kwamba tuonekane malaria Tanzania ni 0 ili kumfurahisha beberu (WHO)??maana sku hizi ni kawaida sana kukutwa huna malaria ila una UTI,nawaza tuu
 
Kuna haja ya kunywa mizizi yetu tuu kama huko zamani, hii U.T.I ni janga kiukweli
 
Tataizo ni madawa wanayotoa
Nchi zilizoendelea huwezi kuandikiwa antibiotics kabisa
Lakini kwetu watu wanatumia kama njugu na madhara yake ndio haya.
Haiwezekani kila mmoja ana UTI na majibu yanatoka kwa dakika kadhaa tu, hii haiingii akilini kabisa

Naungana na mleta hoja ya kuwa wataalamu warudi maabara kwa utafiti
 
Huambukizwa na mdudu anaitwa E coli anapatikana katika haja kubwa na huwa tuna jisafisha kutoka nyuma kuja mbele kwahyo kama Kuna vbakteria katika haja kubwa inakuwa rahisi sana kupata maabukiz.

Na pia si kwa wanawake hata watoto wadogo na pampas zenu hzo mtoto anakaaa na kinyes muda mrefu bila kusafishwa

U.T.I ina mlolongo mrefu sana na ndio maana ipo katika kundi la STDs
 
UFIRAJI ndio chanzo cha U.T.I sugu maana unakuta mtu anaandikiwa antibiotics kali lakini jioni ikifika anafurama kitandani analiwa TIGO na PAPUCHI zamu kwa zamu!

Madhara ya kuchokonoa mavi na kuyahamishia mbele mara kwa mara yanasababisha ugonjwa kukomaa kwa mwanamke na mwanaume!
 
Rudi darasani kajifunze kiswahili, Alaf (aluminium Africa)! Halafu ingependeza zaidi.
 
Labda tafiti zifanyike kwa kina. Sekta ya afya nako kuna sintofahamu nyingi sana. Unakumbuka zamani kila ukipima ni malaria au homa ya mtumbo(Typhoid) tu. Sasa tumehama tupo U.T.I , kwakweli hata vidume siku hizi ni full U.T.I.
Ukiona mwanaume ana UTI jua kuna moja kati ya haya

1.Kapata kwa demu wake kupitia uke
2.Anafanya mapenzi kinyume na maumbile maana bakteria mkuu anaye sababisha yupo hayo maeneo hayo


Turudi kwa mtoa mada
UTI ni kweli tatizo ni uchafu ila usielewe vibaya kuwa kuoga kila wakati,wanawake wanapata sana UTI kwa sababu hizi hapa
1.Kunawa kutoka nyuma(kinyeo) kwenda mbele(ukeni) hasa baada ya kukata kimba hivyo unakua una wabeba wale wadudu kutoka walipotakiwa kuwa na kuwapeleka pasipotakiwa.
2.Kutokumaliza dozi hasa kwa wale ambao walishawahi kuumwa
3.Kupata kutoka kwa mwenza wake kama na yeye ana maambukizi
4.matumizi ya pedi kwa muda mrefu bila kubadilisha mara kwa mara.
5.Matumizi ya sabuni kali ambazo zina pelekea kuua Normal flora wa uke na kuruhusu mdudu huyo kuingia kirahisi

Cha kufanya
1.safisha maeneo yako ya siri kutoka mbele kwenda nyuma
2.usitumie sabuni kali
3.ukiipata tumia dawa hadi umalize na usifanye ngono mpaka upone pia mwambie na mwenzi wako apime kama kapata atumie dawa
4.badili pedi mara kwa mara
 
Mkuu huwa mnalishwa matango pori,na hili mbona hata naibu waziri wizara ya afya faustine ndugulile ambaye kitaaluma pia ni daktari alitolea ufafanuzi,alisema watu wanadanganywa kuhusu huo ugonjwa wa U.T.I. huo ugonjwa huwezi kuthibitisha km mgonjwa ana U.T.I kwa dikika 30 baada ya kupima. Majibu ya U.T.I yanachukua masaa 48 mpaka masaa 72. Hospital za kibinafsi ndiyo matapeli wakubwa,lengo lao huwa ni kuuza dawa. Ndiyo maana siku hizi wamefanya km mtindo,eti kila mtu ana U.T.I!! tena siyo wanawake tu,hata wanaume na watoto. Na watanzania wengi ni mbumbumbu...
 
Wewe ndo hujui mkuu,,,typhoid ndo haiwezekani lakini U.T.I dk 5 zinatosha kuthibitisha kupitia Microscop au deep stick

Ngoja nikupe shule kwanini Typhoid haipimwi kwa nusu saa
 
Kingine cha kushangaza ni kwamba hata watoto wadogo wavulana kwa wasichana nao wanaugua UTI. Kisababishi cha tatizo hili kwa watoto hakieleweki vizuri. Fikiria mtoto wa miezi sita anapimwa na kukutwa na UTI. Jambo hili mara nyingine huleta kutokuelewana ndani ya nyumba na hasa mtoto akiwa wa kike!
 
Baba uti ipo kwenye std's hiyo ni mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…