Madaktari hasa wa Tanzania rudini maabara tena kuhusu ugonjwa wa U.T.I

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,451
Hapana, hapana, hapana.

Huu ugonjwa limekua ni tatizo kubwa mno, tena mno... Yaani kama ungekua unatolewa takwimu si ajabu asilimia 99% ya wanawake wote wanaugua ugonjwa huu.

Taarifa za madaktari zinasema kisababishi kikuu ni uchafu kwa wakina mama katika sehemu zao za siri ambazo mara nyingi hutokana na kutojisafisha vizuri na kutumia vyoo vichafu.

Jamani hapana sitaki kuamini Tanzania tuna wanawake wachafu kiasi hiki maana tatizo hili limekithiri mno. Alaf WHY NOW? kwamba hapo mwanzo hatukuwahi kuwa wachafu?

Hapana madaktari rudini maabara mtuambie labda kuna chanzo kingine tofauti na hiki maana kama ni suala la uchafu this is too much. Hapana rudini maabara mtuambie labda kuna kingine tofauti na hiki mnachotuambia sasa, huu ugonjwa umezikithiri, hata mwanamke ajitahid vipi kuwa msafi bado ataupata tu.

Hapana rudini maabara mkauangalie tena ugonjwa huu
 
Fani ya udaktari ni fani adhimu sana, ni sawa na mambo ya utawala bora na mambo ya haki za binaadamu kwenye siasa za kidemocrasia.

Namna Siasa za kidemocrasia zinavyoendeshwa nchini ndio hivyo hivyo na sayansi ya kidaktari inavyoendeshwa.
vyote mauza mauza
 
Labda tafiti zifanyike kwa kina. Sekta ya afya nako kuna sintofahamu nyingi sana. Unakumbuka zamani kila ukipima ni malaria au homa ya mtumbo(Typhoid) tu. Sasa tumehama tupo U.T.I , kwakweli hata vidume siku hizi ni full U.T.I.
 
Ndugu yangu ni karibu Mara tatu tofauti..akijiskia vibaya akienda hosputal akirud anatuambia vipimo vinasema ana UTI na Typhoid...
Nae anaamini..anaambiwa typhoid yako ni ile ya juu na ipo kwenye damu ndo maana tofauti na wengine..
Kila akienda kupima majibu ni hayo tu.
 
Sekta ya afya ni kama sekta zingine, inavijisekta vingi sana vinavyotegeana kama.
1. Viwanda vya madawa.
2. Viwanda vya vifaa tiba.
3. Taasisi za utafiti wa Madawa.
4. Taasisi za utafiti wa vifaa tiba.
5. Hospitals
6. Madaktari
7. Maduka ya madawa.
8. vyuo vya udaktari.
9. Bima ya Afya
10. n.k

na wako dis organized kwelikweli. what do you expect?
 
Hapana, hapana, hapana.

Huu ugonjwa limekua ni tatizo kubwa mno, tena mno... Yaani kama ungekua unatolewa takwimu si ajabu asilimia 99% ya wanawake wote wanaugua ugonjwa huu.

Taarifa za madaktari zinasema kisababishi kikuu ni uchafu kwa wakina mama katika sehemu zao za siri ambazo mara nyingi hutokana na kutojisafisha vizuri na kutumia vyoo vichafu.

Jamani hapana sitaki kuamini Tanzania tuna wanawake wachafu kiasi hiki maana tatizo hili limekithiri mno. Alaf WHY NOW? kwamba hapo mwanzo hatukuwahi kuwa wachafu?

Hapana madaktari rudini maabara mtuambie labda kuna chanzo kingine tofauti na hiki maana kama ni suala la uchafu this is too much. Hapana rudini maabara mtuambie labda kuna kingine tofauti na hiki mnachotuambia sasa, huu ugonjwa umezikithiri, hata mwanamke ajitahid vipi kuwa msafi bado ataupata tu.

Hapana rudini maabara mkauangalie tena ugonjwa huu
Tanzania kuna listi ya magonjwa ambayo hospital nyingi (hasa ndogo za binafsi) hazijui kupima au hubambikia watu kwa makusudi ili kuuza huduma na dawa! Usipokuwa makini utakunywa dawa kila siku.
1. Malaria
2. Typhoid
3. UTI
4. Helicobacter pylori. (hii tabia imenza siku hizi)
Vingenevyo kwa wale wenye cases genuine na wanakunywa dawa bila kupona basi kuna uwezekano mkubwa kuwa dawa nyingi kwenye nchi yetu hazina viwango au ni fake.
 
Anhaaa heshimu fani zetu huo ndo ukwl
Hapana mkuu naomba mrudi maabara maana siku hizi hata hamuhangaiki kila mgonjwa akija mna simply tu UTI anpewa dawa baada ya wiki akiugua akirud tena utaskia ni UTI
 
Labda tafiti zifanyike kwa kina. Sekta ya afya nako kuna sintofahamu nyingi sana. Unakumbuka zamani kila ukipima ni malaria au homa ya mtumbo(Typhoid) tu. Sasa tumehama tupo U.T.I , kwakweli hata vidume siku hizi ni full U.T.I.
Kweli aisee
 
Antibiotics zenyewe zimekuwa sugu hili ni janga la dunia nzima turudi kwenye majani na mizizi tu
 
Tanzania kuna listi ya magonjwa ambayo hospital nyingi (hasa ndogo za binafsi) hazijui kupima au hubambikia watu kwa makusudi ili kuuza huduma na dawa! Usipokuwa makini utakunywa dawa kila siku.
1. Malaria
2. Typhoid
3. UTI
4. Helicobacter pylori. (hii tabia imenza siku hizi)
Vingenevyo kwa wale wenye cases genuine na wanakunywa dawa bila kupona basi kuna uwezekano mkubwa kuwa dawa nyingi kwenye nchi yetu hazina viwango au ni fake.
Serikali ingepiga marufuku hospitali kufanya kazi za kupima na kutibu.
Inasemekana kipimo kilichopendekezwa kupima maralia na wizara ya afya, na labda kutokana na methodology ya kipimo husika inahitajika zaidi ya masa 24 kiweze kusema kwa usahihi kama mtu na maralia au la.

lakini huwa inachukua wastani wa dak 20-30 kupata majibu, ukiwa na haraka sana hata 5minutes unapewa maralia yako.
 
Kuna kitu unataka kusema

Kuwa huru
Sekta ya afya ni kama sekta zingine, inavijisekta vingi sana vinavyotegeana kama.
1. Viwanda vya madawa.
2. Viwanda vya vifaa tiba.
3. Taasisi za utafiti wa Madawa.
4. Taasisi za utafiti wa vifaa tiba.
5. Hospitals
6. Madaktari
7. Maduka ya madawa.
8. vyuo vya udaktari.
9. Bima ya Afya
10. n.k

na wako dis organized kwelikweli. what do you expect?
 
Serikali ingepiga marufuku hospitali kufanya kazi za kupima na kutibu.
Inasemekana kipimo kilichopendekezwa kupima maralia na wizara ya afya, na labda kutokana na methodology ya kipimo husika inahitajika zaidi ya masa 24 kiweze kusema kwa usahihi kama mtu na maralia au la.

lakini huwa inachukua wastani wa dak 20-30 kupata majibu, ukiwa na haraka sana hata 5minutes unapewa maralia yako.
Ni kweli. Malaria sehemu nyingi hawajui kupima vizuri au labda nahisi vidudu vya malaria ''vimejibadilisha'' kiasi cha kuhitaji vipimo vya aina nyingine. Kwa upande wa typhoid ndiyo kabisaa, cases nyingi wanaso-conclude kuwa watu wana typhoid huwa siyo kweli. Na siku hizi ndiyo umeingia huo mtindo wa UTI na Helico Pylori bacteria.
 
Nawaza tu.

Baada ya kuambiwa una U. T. I. ulitumia dawa?

Baada ya kutumia dawa ulipona?

Ikiwa hukukubaliana na vipimo;

Hukutumia dawa?

Na baada ya hapo ulipona?
 
Shida ni pale unapopewa dawa ambayo inatibu UTI na maralia inatibu pia.
unazifaamu zile dawa zina paracetamal ndani yake?
 
Inahitajika Elimu hasa juu ya huu ugonjwa. UTI inakuzwa sana
 
Back
Top Bottom