Kuna watu wanacomment kwa kubeza lakini hii ishu ya matumbo ikija kuwakamata moja ya thread watakayopitia kupata msaada ni hii hii.
Mtu akisema anakosa choo msikie hivo hivo aisee ni kitu kinatesa sana na kinakuharibu psychologically. Mnaweza kua mmekutana kama weekend hii kijiwe flani mnapata msosi mzuri sana lakini unaona mwenzako anakula hana raha, tena kidogo kidogo.
Ushauri wa kula mapapai, kunywa oil chafu, tumia bisacodyl, tunywa castrol oil, kunywa maji ya chumvi na sukari, kula vyakula vya fiber kwa wingo, ushauri wote utafuata lakini mwisho wa siku utarudi palepale hupati choo, wala hisia kwamba umebanwa haja haipo kabisa.
So tushauriane kwa upendo, kama unajua solution weka hapa watu wafuate na kama huna basi usicomment mzaha. Maana utaikumbuka thread hii siku za usoni