Madaktari wa kiume wasijihusishe na uchunguzi wa sehemu za Siri za wanawake, sera itungwe upya daktari wa kike ahudumie wanawake!

Madaktari wa kiume wasijihusishe na uchunguzi wa sehemu za Siri za wanawake, sera itungwe upya daktari wa kike ahudumie wanawake!

Mtu akiumwa atibiwe tu kwa kufuata utaratibu muhimu ni kupona. Tatizo mleta mada una mawazo ya kishenzi ndo maana unapendekeza upuuzi.
 
Nilioomaliza chuo nilipatwa na changamoto ya kiafya ikanibidi nilazwe hosii, jirani yangu alikuwa ni baba kabisa Kwa makamu yake na miaka yangu anqeza kunizaa.
Yule baba alikuwa na changamoto katika njia ya mkojo yani mkojo ulikuwa hautoki njia ilikuwa imeziba.

Kaka nurse mmoja asee akaanza kuishika mashine ya yule baba na nurse Kwa umri wake ni mtoto wa yule baba nilipatwa na aibu mimi pamoja na kuwa nilikuwa hoi lakin ile hali ilinihuzunisha sana.

Nurse alikuwa anaishika mara aipigepige mara aipikichepikiche yani ilikuwa ni balaa.

Kuna vile vipazia alikuwa kavitandaza kuziba watu wasione lakin kwa angle nilikuwa nimelazwa mimi kulikuwa hakuna kipingamizi niliona kila kilichoendlea
Urethra stricture
 
Kama ilivyo polisi wanapoenda kumkamata mhalifu wa kike askari anayehusika na ukamataji ni askari wa kike, hata magereza ya kike huwa inahudumiwa na askari wanawake.

Upande wa afya mambo ni tofauti, vijana wa kisasa waliojipata kuwa madaktari na wauguzi wanafanya michezo ya kishetani kwa mama zetu ,dada zetu na wake zetu !hata ugonjwa usio wa kuchunguza sehemu za siri daktari anamuamuru mgonjwa avue nguo alale kitandani amuingize vidole ati anaangalia kama Ute uko safi!

Sera ibadike kama Kuna uchunguzi ufanywe mbele ya mume wake au mmoja wa ndugu na si mgonjwa peke yake, ama daktari wa kike ahudumie wagonjwa wa kike ikiwa amehitajika kuchunguzwa sehemu za Siri. Wake zetu asilimia tisini wakivukiwa nguo huko kwenye vyumba vya madaktari hawatoki salama kabisa!

Na kwa Hali ilivyo sasa madaktari wengi ni wagonjwa na wanaleta athari kubwa kijamii waziri wa afya jitahidi kuondoa kero hii,
Pole sana kwa changamoto hiyo.

Wafanyakazi wote wa afya (madaktari, manesi nk) hufanya kazi zao kwa kuzingatia kanuni, miongozo, sheria na viapo vyao vya kitaaluma wanapowahudumia wagonjwa.

Kila daktari kabla ya kupewa shahada ya udaktari kwanza hula kiapo (Hippocratic Oath). Vivyo hivyo kwa manesi na wengine.

Pia zipo kanuni zinazoongoza utendaji wa kidaktari (principles of medical ethics) ambazo ni:

-Autonomy –kuheshimu na kujali uhuru/haki za mgonjwa (respect for the patient's right to self-determination.)

-Beneficence – kuhakikisha kwamba kila unachofanya kama daktari kina athari nzuri/chanya kwa mgonjwa (the duty to 'do good')

-Non-Maleficence – kuhakikisha kwamba kama daktari haufanyi kitu chochote chenye athari mbaya/hasi kwa mgonjwa (the duty to 'not do bad')

-Justice –kuwatibu na kuwachukulia watu/wagonjwa wote kwa usawa (to treat all people equally and equitably).

👉Kwa hiyo kwa kuangalia kanuni hapo juu mgonjwa ana haki ya kukataa (bila kulazimishwa) kufanyiwa uchunguzi wowote, kipimo chochote au kukataa matibabu ya aina fulani hasa baada ya kuelezwa/kuelimishwa kuhusu umuhimu wa uchunguzi huo, kipimo hicho au matibabu hayo

👉Pia sheria/miongozo ya utendaji wa kazi za kidaktari huwataka madaktari kuwa na mfanyakazi mwingine wa afya wa jinsia ya mgonjwa pale anapomfanyia uchunguzi wowote mgonjwa ambaye si wa jinsia yake ndani ya chumba chake.

Mfano kama daktari wa Kiume anamfanyia uchunguzi mgonjwa wa Kike basi sheria/taratibu zinataka kwenye chumba chake au wakati wa uchunguzi huo awepo daktari au nesi wa Kike. Vivyo hivyo kwa daktari wa Kike kwa mgonjwa wa Kiume.

Kama taratibu hizo zinakiukwa basi huenda kukawa na vitu ambavyo huchangia hayo kutokea.
 
Bila shaka hii mada inawalenga hawa madaktari wetu wa •com ambao unaweza kusema wameingia kwenye hiyo fani kwa kufuata tu mkumbo, huku maadili ya kazi yakiwa ni 0.
 
Na kwa Ta

Kwa hapa Tanzania sasa hivi Madaktari vihiyo ni wengi mno tena kwa sasa wamerudi kwa kasi, wapo kila hospitali. Wengi wakishapekua sehemu za siri za wake zetu wanaenda vijiweni kusimulia jinsi nyeti za wake zetu zilivyo na wanapenda kuvaa chupi za aina gani huku kijiwe kikichangamka kwa vicheko. Utashangaa mwisho wa siku mtaa wako umejaa vijana ama watu wasio na kazi wanapita kuzingira nyumba yako ili mradi tu naye apate kumuona mkeo.
Kwenye kile kiapo cha udaktari (Hippocratic Oath) kuna kuapa kutunza siri za mgonjwa.

Kwa hiyo kama kuna daktari anachukua taarifa za afya ya mgonjwa na kuzipeleka kijiweni basi anastahili kuchukuliwa hatua za kisheria kupitia baraza la madaktari.
 
Madaktari wenyewe kuna maeneo hawatoshi unadhani hilo litawezekana nchi nzima?.Option niwewe kuajiri daktari wako kwasababu dunia yaleo hakuna kipya.Kama niswala lakukosekana maadili na uadilifu ata hao wanawake nao wanamichezo michafu wao kwa wao siku hizi.cha msingi weledi,sheria na kanuni za kazi zizingatiwe.
Kweli kuna changamoto hiyo ya upungufu wa madaktari na manesi nk.
 
Kama ilivyo polisi wanapoenda kumkamata mhalifu wa kike askari anayehusika na ukamataji ni askari wa kike, hata magereza ya kike huwa inahudumiwa na askari wanawake.

Upande wa afya mambo ni tofauti, vijana wa kisasa waliojipata kuwa madaktari na wauguzi wanafanya michezo ya kishetani kwa mama zetu ,dada zetu na wake zetu !hata ugonjwa usio wa kuchunguza sehemu za siri daktari anamuamuru mgonjwa avue nguo alale kitandani amuingize vidole ati anaangalia kama Ute uko safi!

Sera ibadike kama Kuna uchunguzi ufanywe mbele ya mume wake au mmoja wa ndugu na si mgonjwa peke yake, ama daktari wa kike ahudumie wagonjwa wa kike ikiwa amehitajika kuchunguzwa sehemu za Siri. Wake zetu asilimia tisini wakivukiwa nguo huko kwenye vyumba vya madaktari hawatoki salama kabisa!

Na kwa Hali ilivyo sasa madaktari wengi ni wagonjwa na wanaleta athari kubwa kijamii waziri wa afya jitahidi kuondoa kero hii,
Acha kupotosha watu,90% unaijua wewe au umeandika kujifurahisha?,kwa hiyo naye wote wanaochunguzwa hufurahia kutotoka salama sio?
 
Kama ilivyo polisi wanapoenda kumkamata mhalifu wa kike askari anayehusika na ukamataji ni askari wa kike, hata magereza ya kike huwa inahudumiwa na askari wanawake.

Upande wa afya mambo ni tofauti, vijana wa kisasa waliojipata kuwa madaktari na wauguzi wanafanya michezo ya kishetani kwa mama zetu ,dada zetu na wake zetu !hata ugonjwa usio wa kuchunguza sehemu za siri daktari anamuamuru mgonjwa avue nguo alale kitandani amuingize vidole ati anaangalia kama Ute uko safi!

Sera ibadike kama Kuna uchunguzi ufanywe mbele ya mume wake au mmoja wa ndugu na si mgonjwa peke yake, ama daktari wa kike ahudumie wagonjwa wa kike ikiwa amehitajika kuchunguzwa sehemu za Siri. Wake zetu asilimia tisini wakivukiwa nguo huko kwenye vyumba vya madaktari hawatoki salama kabisa!

Na kwa Hali ilivyo sasa madaktari wengi ni wagonjwa na wanaleta athari kubwa kijamii waziri wa afya jitahidi kuondoa kero hii,
Shida hao madaktari wa kike hawatoshelezi nchini kiasi cha kubadili sera, 5 years sio mchezo na wengi wa wanafunzi wakike hukimbia masomo ya sayansi kwa kudai ni magumu.
 
Na kwa Ta

Kwa hapa Tanzania sasa hivi Madaktari vihiyo ni wengi mno tena kwa sasa wamerudi kwa kasi, wapo kila hospitali. Wengi wakishapekua sehemu za siri za wake zetu wanaenda vijiweni kusimulia jinsi nyeti za wake zetu zilivyo na wanapenda kuvaa chupi za aina gani huku kijiwe kikichangamka kwa vicheko. Utashangaa mwisho wa siku mtaa wako umejaa vijana ama watu wasio na kazi wanapita kuzingira nyumba yako ili mradi tu naye apate kumuona mkeo.
Hizi tuhuma unaweza kuthibitisha?
 
Akishasema achia miguu....nayo inainuka.
Mungu awapiganie kwa kweli kazi yao ni ngumu sana
🤦🤦🤦To yeyeeee!! To yeyeeee!! To yeyeeee!!!
Daaah!! Katika ubora wako 🙆🙆🙆
 
Huduma ya afya ni heavily regulated na management yake ni (very technical).

Kuisimamia either umesoma shahada ya heath and social care management au daktari ambae umefika hapo through succession planning umepewa skills za kutosha za management.

Kati ya mtu aliesoma shahada ya ‘health and social care management’ na daktari aliekuzwa kwa succession planning na kupewa management skills. Daktari ni always superior.

Sasa kwa mtu ambae anaelewa maswala ya afya na nadharia ya ‘medical ethics’, nadharia ambayo wataalamu wote wa afya lazima wailewe na WHO pia wanai-promote; mgonjwa lazima apewe option kwenye kuangaliwa private parts.

That is through ‘medical ethics’ and patient choice (Medical Ethics: Autonomy – The Medic Portal.). kwenye maswala la kuchunguzana private parts, if not in emergency; mgonjwa lazima apewe option yupo comfortable kuchunguzwa na doctor yeyote au anataka gender yake.

Ni hivi wengi wenu humu mnampamba Dr. Dorothy Gwajima kwa mkumbo tu (yes she is special).

Lakini sisi wengine tulitaka arudishwe afya kutokana na ku-evaluate skills zake alizokuwa akionyesha alipokuwa akifanya troubleshooting wakati akiwa naibu katibu mkuu TAMISEMI, kama unaelewa management ya afya ilikuwa wazi kapitia succession planning ya management na performance yake ilikuwa nzuri ndio maana akapanda kutoka work floor hadi wizarani na kushika nafasi zote hadi kufika wizarani (ni mtaalamu, kweli kweli).

Watanzania mnamtaka Ummy Mwalimu afya na sasa mmepewa Jenista Mhagama. Muulize Mhagama concept moja tu ya medical ethics, let’s pick ‘beneficence’ akiweza kukuelezea, njoo unitukane. Mpe siku kadhaa tena akasome Google.

Nchi ya mzaha sana, ni rahisi kumlalamikia mtaalamu mambo ya kitaalamu akaona; kuliko poyoyo ambae hajui lolote.
 
Ushauri mzuri but ni ngumu kuu apply kwasababu 2
1. Idadi ya madaktari tulio nayo hadi sasa (bila kujali jinsia ) haitoshi, hawa waliopo tu tuna wa overwork. Daktari mmoja unakuta anafanya kazi hospitali zaidi ya 3 kwa siku
2. Kitu usicho kijua ni hiki, wanawake by nature is either hawapendani au hawaaminiani, wanawake wakiwa wana hudumiwa na wanaume wanajionaga wapo salama zaidi kuliko wakiwa mikononi mwa wanawake wenzao
NB: Kitu cha ajabu sana kwenye hi dunia, mtu anae TIBU watu hadi wapone, anafundishwa kwa gharama kubwa sana, yeye au wazazi wake zinawatoka pesa nyingi sana LAKINI mtu anaefundishwa kuua na kujeruhi watu, yeye anafundishwa BURE na chakula anapewa bure kabisa and hence, idadi ya wauaji na wwtesaji ni wengi zaidi kuliko wanao tengeneza afya zetu. Interesting
 
Kwenye sekta ya afya hakuna kitu kinachoitwa uchi , pale unahudumiwa upate matibabu njia ndo hyo tu hakuna nyengine pia madktari wengi ni wa kiume
 
hizi mbwembwe mnazoleta hapa jukwaani ni kwavile hamjawahi kuumwa na ukaenda hospital afu ukakutana na huyo dokta bingwa anaetakiwa kukusaidia ni jinsia ya kiume ndipo utaacha ujinga mnaoongea hapa

kikubwa ni kufuata taratibu zilizowekwa
 
Back
Top Bottom