DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Huyu atakua amesomea St. FRancis Ifakara
 
Mwanangu juzi kapewa midonge ya vidonda vya tumbo.. nimeitupa hukooo...
Nakushauri kaka endelea kumpima hispitali nzuri zaidi walau utapata ufumbuzi licha ya kuwa utapata garama kubwa,Mimi wa kwangu nilipata ufumbuzi yupo salama
 
Ni kweli baadhi yao ni 'bogus' ... hawaaminiki kabisa. Kuna vifo vingi vimesababishwa na uzembe wao.. Inasikitisha sana
 
Wanakuaga wakali hao ukiwaambia ukweli
 
Aisee ukilinganisha graduates wa miaka ya nyuma na hawa wa siku hizi utaona tofauti kubwa sana, kwa sasa elimu siyo hovyo tu kuanzia ngazi za kule chini bali imezidi ku reflect huku juu kwa wahitimu ambao ni hopeless kabisa. Tukiendelea kufanya siasa kwenye mambo ya msingi kama elimu tutarajie zaidi ya hili.​
 
Hii ndiyo hali ninayo sasa.
Mbavu zinabana na kuachia, kichwa, mwili na viungo vinauma uma tuu.. Muda wote mwili una uchovu.

Na hapa nimeshamaliza Dozi ya UTI na Typhoid zaidi ya Wiki sasa ila sijaona mabadiliko yoyote.

Huenda hii kitu ipo kweli mtaani huku..
Trust me unakunywa dawa ambazo huugui ugonjwa wake kama uko karibu na Dar sogea Medwell Kibaha hapo hawafeki kitu
 
Bila kuwekeza na kuweka vigezo vikubwa kwa udaktari lazima tutapoteza watu wengi kwa uzembe.

Leo mtu ana Division 4/0 anaenda India, China, Uturuki anarudi na Degree
 
Vyuo vya udaktari vya angalau uwe na D tatu vimekuwa vingi Sana....
Swala siyo D tatu, D tatu A-level enzi hizo haikuwa mchezo..........ila kwa sasa kuna kuporomoka kwa kiwango cha elimu inayotolewa tokea msingi hadi huku juu. Kinachangaliwa sasa ni statistics, walioandikishwa shule ni wangapi, waliomaliza ni wangapi......kujua kwamba hawa wahitimu wamepata nini kichwani siyo la msingi tena.​
 
Nilikua Bukoba na kundi la wageni. Tumeenda hospitali, mmoja alikua ana homa. Vipimo vikaonyesha hana shida. Cha ajabu daktari akamuandikia lundo la dawa. Yule mzungu alishangaa sana na kutukana matusi mengi ya kuonyesha kwamba watu weusi hatuna akili. Aliniuliza, hivi ndivyo mambo yanafanyika? Na, je Dar ni hivihivi? Sikuvunga nikamchana ukweli. Akasikitika sana.
Duh
 
Swala siyo D tatu, D tatu A-level enzi hizo haikuwa mchezo..........ila kwa sasa kuna kuporomoka kwa kiwango cha elimu inayotolewa tokea msingi hadi huku juu. Kinachangaliwa sasa ni statistics, walioandikishwa shule ni wangapi, waliomaliza ni wangapi......kujua kwamba hawa wahitimu wamepata nini kichwani siyo la msingi tena.​
Well said mkuu....serekali iangalie vizuri sera ya elimu na ifanye reform panapotakiwa
 
Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this?
Una bahati nzuri wewe ugonjwa uliisha, I mean ulipona kutokana na kilichotokea.

Sasa kuna wale ambao badala ya ugonjwa kuisha ghafla kama wewe, wao ugonjwa unaongezeka ghafla.

Mungu atusaidie sana.
 
Sa nyingine sio lazima afanye hayo anatumia na uzoefu ukimwelezea tu anajua hili litakua ni tatizo Fulani naongea kama Doctor Car apa
 
Duh! kuna mmoja alinishona kidole uzi sita hadi anamaliza sina hamu,sindano ya gazi inaingizwa hadi inatokea upande mwingine kama anashona nguo...

[emoji38][emoji38][emoji38]
Pole sana mkuu, na kama ilkua ni hospital ya serikali ndio mambo yao.
 
  • Thanks
Reactions: Sax
Back
Top Bottom