DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
mi nadhani pia mtoa huzi kitaaluma zaidi pia ilibidi umsaidie huyo daktari kumueleza juu ya umuhimu wa physical examination haswa kwa wagonjwa wenye complain ya shida ya moyo na mapafu kwanza alafu ndio uje kuongea jf lakini pale umeshindwa kumsaidia unakuja kuongea hapa je tatizo ni nani sasa?
Taaluma hii ndio inaongoza kwa kuchukiana sana nina huzoefu wa mda mrefu kazini ila madaktari punguzeni chuki ninyi kwa ninyi alafu shirikianeni unapotengeneza negativity kwenye jamii impact yake ni kubwa so wewe ndio shida sana
Inawezekana ukawa sahihi kuwa nilikosea, lakini kitu ambacho hauko sahihi ni kwamba mimi nina chuki na MDs wenzangu, wala sina sababu ya kuwa hivyo. Kumbuka hapo nilikua katika state ya ugonjwa, na nilikua nawaza mambo mengi hasa ukizingatia kuwa mimi ni daktari pia, so nina idea ya nini kinaweza kuwa kinaendelea mwilini mwangu na kuwaza mengi what could go wrong na mambo mengi sana, plus I was very disappointed. So, inawezekana siku act rationally. Sina sababu yoyote ya kuwa na chuki na mtu ambae hata simfahamu. Uko sahihi kuwa nilipoteza opportunity ya kumuelimisha yule kijana, lakini ni kwa sababu ya mazingira ambayo nimeyaeleza, na wala si chuki.
 
Kwa mda ulioenda haukutakiwa kulaumu mtu almost ni asubuhi Kwa vituo vyetu mtoa huduma ni uyo tangu saa 9 mchana
Lakini kuficha identity pia sio swala zuri unajua kitu share ili kuboroesha huduma
Hawana shift?

Unataka kusema watu waliozidiwa usiku imekula kwao sababu madaktari mida hiyo hawana ufanisi?
 
Aliniambia binti yangu ambaye ni daktari, '' Baba usiende kwa madaktari vijana, hawa walisoma ili wapate vyeti sio kuelewa''. Na mimi nakubaliana nae kabisa. Bora nitibiwe na nurse mtu mzima kuliko kutibiwa na daktari kijana.
It's true!
Wakati mama angu anakaribia kustaafu;akiwa wodini na hao internship wa kutoka UDOM ,aisee si akakuta dada anachanganya dawa(Ile ya unga ya sindano) na maji ya uhai 😳...wakati zile Zina maji yake ya kuchanganyia....
Ndo mama anamuuliza,ndo mnavyofundishwa? Hana la kujibu ...
Ilibidi mama angu afanye mwenyewe Ili kumchoma sindano huyo mgonjwa!
Km huna Dr ,nesi unaemfahamu vzr kwakweli ni balaa
 
It's true!
Wakati mama angu anakaribia kustaafu;akiwa wodini na hao internship wa kutoka UDOM ,aisee si akakuta dada anachanganya dawa(Ile ya unga ya sindano) na maji ya uhai [emoji15]...wakati zile Zina maji yake ya kuchanganyia....
Ndo mama anamuuliza,ndo mnavyofundishwa? Hana la kujibu ...
Ilibidi mama angu afanye mwenyewe Ili kumchoma sindano huyo mgonjwa!
Km huna Dr ,nesi unaemfahamu vzr kwakweli ni balaa
Sasa kama hospital haina distiled water?
 
Siku hizi madaktari wanageralize ugonjwa from a certain sample of diagnosis...

Vipimo navyo fake..
 
Mkuu mimi kila miezi 6 nafanya physical checkup, sasa nikaenda hospital tofauti safari hii. Kupima wakasema mkojo mchafu nikauliza kwanini mkojo mchafu wakasema kunywa maji mengi. Na wakanipa madawa nikatumia yale madawa ya kawa yananizidi nguvu wiki 2 sijatoka ndani. Nikaanza kufanya ganzi mkono mara ganzi ya mguu sijui kiuno kimeganda. Nikaona acha nitoke nje ya nchi nimekwenda huko nimeambiwa nina protein nyingi kwenye mkojo, kwahio niangaliwe liver na kidney naam hilo ndio lilikuwa tatizo. Lakini huku nyumbani nimeambiwa mkojo mchafu tena ninywe maji tu[emoji1787][emoji1787]
Una mikojo michafu lakini tena bado unameza madonge yenye sumu!!!

Watu huwa mnajitakia kufaa!!
 
Pole Sana kaka,Kuna hospitali moja nilitaka kuwashitaki maana Ni hispitali ya kubwa tu mkoani walinipimia mwanangu wakasema ana madonda kumbe ni uongo,ikabidi nipoteze pesa nyingi kwa kuutafuta ukweli pengine ,nikagundua Hana nilichoka kabisa,Mungu tu atulinde.Nisingekuwa makini mwanangu angetumia dawa ambazo zingeleta shida badae licha ya kuwa alitumia kwa mda Ndo nikashituka.
 
Akili zote ziko kwenye kula kimasihara,yaani shida tupu kuanzia vipimo vya lab,namuuliza daktari kama kuna kipimo cha HCG hajawahi kusikia hata hiyo hormone,asa ningemwambia estradiol,kiufupi sikumlaumu sana maana kusahau kupo ila kwa jinsi anavyonisikiliza nikaona hapa hamna kitu,nikaghairisha matibabu.
Unakutana na nesi wa kiume kama rikiboy , lazima ukufe haraka sana.

Muda wote anawaza papuchi na kudinya.
 
hii ilinikuta aisee nilipimwa nikakutwa na malaria 4 kwenye dawa nikapewa zile za wajawazito kuzuia malaria badala ya kutibu malaria.... akaniambia baada ya week mbili nipate dose nyingineee..nikarudi home naona siku mbili sioni unafuu ...bahati nzuri nina mdogo wangu anasoma muhimbili pale akaja kunicheck eeenh kuona zile dawa akasema bro utakufaa twende faster hospital hizo dawa walizokupa siku hizi hazitumiki kabisa.... ndio ilikuwa pona yangu
Aiseee...

Tumetengeneza madaktari vilaza.
 
Pole Sana kaka,Kuna hospitali moja nilitaka kuwashitaki maana Ni hispitali ya kubwa tu mkoani walinipimia mwanangu wakasema ana madonda kumbe ni uongo,ikabidi nipoteze pesa nyingi kwa kuutafuta ukweli pengine ,nikagundua Hana nilichoka kabisa,Mungu tu atulinde.Nisingekuwa makini mwanangu angetumia dawa ambazo zingeleta shida badae licha ya kuwa alitumia kwa mda Ndo nikashituka.
Mwanangu juzi kapewa midonge ya vidonda vya tumbo.. nimeitupa hukooo...
 
Aliniambia binti yangu ambaye ni daktari, '' Baba usiende kwa madaktari vijana, hawa walisoma ili wapate vyeti sio kuelewa''. Na mimi nakubaliana nae kabisa. Bora nitibiwe na nurse mtu mzima kuliko kutibiwa na daktari kijana.
Nimekumbuka kuna bibi mmoja alienda clinic kwenye hospitali moja ya rufaa.
Huwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na matatizo ya viungo.
Siku hiyo alikutana na Daktari kijana.
Baada ya kumhudumia na kumwandikia dawa akamwambia; nanukuu: -
" Bibi siku nyingine ukijisikia vibaya usije tena hospitali! Nenda tu kwenye duka la dawa ununue dawa zako".
Hii kauli ilimkatisha sana tamaa huyu Bibi; anaona kama daktari ameshamwona kama kutokana na umri wake mkubwa asubiri tu hatma yake. Hana haja ya kwenda Tena hospitali!!
 
Pole sana, ni kweli watu wengi sana tunakunywa Dawa ambazo haziendani na ugonjwa husika, Mungu atusaidie tu maana ni hatari sana.
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Hawa ndo wale sekondari wanauliza kozi gani chuo ni rahisi kupata boom na ukimaliza unapata kazi fasta...... Kuna wengine wapo huko sio kwa kupenda hio kazi
 
Swala sio mganga hajigangi.

Swala ni kuwa unaweza jua tatizo kwa kuhisi tu maana tayari wewe ni daktari unajua kabisa kuwa hapa tatizo ni hili na lile na sio swala la kuona pulse rate au kutumia steto kusikiliza mapigo ya moyo na sauti.

Mi si daktari ila huwa naweza fanya diagnosis ya mwenyewe.

Kama matatizo ya moyo unayo maana yake utakuwa na dawa ndani.
Hizo dawa ulimnunulia wewe ukamuwekea ndani??

Rudia kusoma ulichoandika hapo mwisho mkuu.
 
Back
Top Bottom