DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Swala sio mganga hajigangi.

Swala ni kuwa unaweza jua tatizo kwa kuhisi tu maana tayari wewe ni daktari unajua kabisa kuwa hapa tatizo ni hili na lile na sio swala la kuona pulse rate au kutumia steto kusikiliza mapigo ya moyo na sauti.

Mi si daktari ila huwa naweza fanya diagnosis ya mwenyewe.

Kama matatizo ya moyo unayo maana yake utakuwa na dawa ndani.
Sasa utajifanyia diagnosis ugenini?
 
Akili zote ziko kwenye kula kimasihara,yaani shida tupu kuanzia vipimo vya lab,namuuliza daktari kama kuna kipimo cha HCG hajawahi kusikia hata hiyo hormone,asa ningemwambia estradiol,kiufupi sikumlaumu sana maana kusahau kupo ila kwa jinsi anavyonisikiliza nikaona hapa hamna kitu,nikaghairisha matibabu.
 
Zamani kazi hizo zilikuwa za wito,sasa hivi tunasoma tupate ajira,ila kuna vijana wako vizuri bado,daktari wangu ni she(specialist)lakini yuko vizuri sana na kuna mahali pia nilikutana na kijana naye pia anajua na anaipenda kazi yake,asilimia kubwa vijana ni wa hovyo
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Unamuonea tu daktar wa watu ila vitendea kazi ulijiridhisha kuwa vipo ? Health center zina uhaba wa vifaa , so shukuru hata alipo doubt BP kama diagnosis yake , mwisho wa siku ww kama daktar inabidi ujue wap kwa kwenda kulingana na case yako maana naamin lzm kichwan unakuwa ddx zako , kwenda health cente alitakiwa afanye hvyo commoner
 
Mkojo ulikuwa dark brown, hii hospital ipo sehemu ya wenye nazo[emoji383]. Sitaji jina kwa sababu za privacy.
Hadi hapo inakuwa ni uongo, privacy ya kitu gani kwamba wewe pekee ndo mgonjwa hospital nzima?
 
Kuhisi sawa.
Ila hadi kufikia hatua ya kujitibu mwenyewe, hapana. Sijawahi kuwa na tatizo la moyo kabla.
Nilishahisi shida ni moyo, ila nilitaka mtu mwingine ani examine na kufikia conclusion na kunishauri cha kufanya. Huwa hakuna kitu sipendi kama kujitibu mwenyewe, unless labda kama sina option kabisa. Tena ugonjwa wa kuhusu moyo, siwezi hata kujaribu kujitibu.
Hamaanish kujitibu , ila ww km dr lzm uwe na ddx zako ambazo zitakuguide uende wap kupata huduma nzuri
 
Kuna dogo yuko Mloganzila yeye ukimweleza tatizo kazi yake ni ku-google ndo anakupa majibu
Ndo maana nimesema kuwa mtoa mada alitakiwa ajue tatizo lake kabla hajaenda hospital.
Siku hizi ukiweka dalili zote unaletewa majibu, dawa etc
 
Aliniambia binti yangu ambaye ni daktari, '' Baba usiende kwa madaktari vijana, hawa walisoma ili wapate vyeti sio kuelewa''. Na mimi nakubaliana nae kabisa. Bora nitibiwe na nurse mtu mzima kuliko kutibiwa na daktari kijana.
Usikariri sasa kuna kada madaktar wapya ndo bora kulingana na mitaala mipya
 
Unamuonea tu daktar wa watu ila vitendea kazi ulijiridhisha kuwa vipo ? Health center zina uhaba wa vifaa , so shukuru hata alipo doubt BP kama diagnosis yake , mwisho wa siku ww kama daktar inabidi ujue wap kwa kwenda kulingana na case yako maana naamin lzm kichwan unakuwa ddx zako , kwenda health cente alitakiwa afanye hvyo commoner
Vifaa pekee alivyohitaji ni mikono yake, stethoscope pamoja na Manual BP machine, ambavyo vyote vilikwepo mezani kwake niliviona.
Ilikua ni saa tisa za usiku mind you, ilikua logical kwenda the nearest facility. Nimesisitiza si kwamba nilitegemea matibabu ya kibingwa usiku ule pale health center, ila nilihitaji mtu tu wa kusikiliza kifua changu, mapigo yangu ya moyo na pulse yangu na aweze kuniambia kwamba, brother hapa you need to go for specialist care, au bro, this is minor, haina issue. Na any MD with a stethoscope and a manual BP machine should have been able to do so.
 
Tatizo ambalo halipewi uzito au halisemwi especially kwenye kada ya Afya ni hili hapa wengine watasema.

Tuna watoa huduma ambao wamekata tamaa sana na wako stressed sana.. jamii/familia ndugu wanahisi mtu kuwa Dr anapata pesa nyingi sana hata jamii ime-set standard flani kwa mtu akisema yeye ni Dr basi wanajua/wanategemea awe mambo safi financially.

Bahati mbaya kabisa hata wenyewe(Drs, Ns, Phm etc) kipindi wanasoma since grass root waliamini wakifika level hizo .. mambo yao yatakuwa super ... miaka 20imepotelea darasani with high expectation .... Akija kitaa anakutana na mshahara kiduchu ... bellow 1M ... anakutana na tegemezi ya nguvu.
matokeo yake anaenda kazini kutimiza muda wake tuu arudi mtaani akanywe bia.

Hili eneo linahitaji kusoma kila siku ili uendelee kutoa huduma iliyo bora ... changamoto iliyopo nani asome kila siku na majukumu mengine yanamngoja ,.. kwanza anatakiwa atafute pesa nje na eneo lake la kazi ...

Matokeo yake Graph ya uelewa wa conditions huzidi kushuka unabakiwa na shule ya kuegesha mixer uzoefu....

NB. Ni kweli kuna baadhi ya mazingira unaona kabisa hapa huyu jamaa hii condition haijui na anakomaa bila kumpeleka mgonjwa sehemu nyingine akapate msaada....

BTW huku JF/mitandaoni hakuna pongezi kwa Drs, Nurses, Pharmacist na watoa huduma in general .. huku zinakuja lawama tuu .. are u expecting your son & daughters to be alien?

Had more than 500ops in my hand ... kama kuna apreciation ni hawazidi 10.
Any way mimi napenda attitude ya vijana wanaokuja kwenye Game ... hela, hela, shule kidogo ha ha haaa..
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani pia.
 
Mwanzo alishindwa kulala lkn baada ya tukio akapona kabisa. Sasa sijui ni ugonjwa gani mkali hivyo na ukipona bila dawa

Njooni kwetu madokta wa mitishamba hatuna mbambamba
Nimesema kuwa nilitoka hospitali hapo health center saa 11 alfajiri, hadi nafika home ni around kumi na mbili kasoro, hakukua na suala la kulala tena hapo.
 
Back
Top Bottom