DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tuweke utaratibu wa kupima miili yetu, FBP, ECHO, STOOL, URINE ANALYSIS
Angalau kila baada ya miezi 3-6

Tupunguze unywaji na ulaji wa hovyo.

Tulale kwa muda sahihi

Tuwekeze katika maombi
Mkuu mimi kila miezi 6 nafanya physical checkup, sasa nikaenda hospital tofauti safari hii. Kupima wakasema mkojo mchafu nikauliza kwanini mkojo mchafu wakasema kunywa maji mengi. Na wakanipa madawa nikatumia yale madawa ya kawa yananizidi nguvu wiki 2 sijatoka ndani. Nikaanza kufanya ganzi mkono mara ganzi ya mguu sijui kiuno kimeganda. Nikaona acha nitoke nje ya nchi nimekwenda huko nimeambiwa nina protein nyingi kwenye mkojo, kwahio niangaliwe liver na kidney naam hilo ndio lilikuwa tatizo. Lakini huku nyumbani nimeambiwa mkojo mchafu tena ninywe maji tu🤣🤣
 
Mkuu mimi kila miezi 6 nafanya physical checkup, sasa nikaenda hospital tofauti safari hii. Kupima wakasema mkojo mchafu nikauliza kwanini mkojo mchafu wakasema kunywa maji mengi. Na wakanipa madawa nikatumia yale madawa ya kawa yananizidi nguvu wiki 2 sijatoka ndani. Nikaanza kufanya ganzi mkono mara ganzi ya mguu sijui kiuno kimeganda. Nikaona acha nitoke nje ya nchi nimekwenda huko nimeambiwa nina protein nyingi kwenye mkojo, kwahio niangaliwe liver na kidney naam hilo ndio lilikuwa tatizo. Lakini huku nyumbani nimeambiwa mkojo mchafu tena ninywe maji tu[emoji1787][emoji1787]
level ipi ya hospital mkuu uliyotibiwa hapa? mkojo mchafu? how?
 
Utakuwaje Prof wa Medicine na hujasoma MMED au MSc huko na PhD!??
Ndivyo ilivyo kwenye Medical schools nyingi za Tanzania; ukihesabu maprofesa wa mwedicine ambao wana Ph.D unaweza usipate hata mmoja. Wenye masters pia ni wachache sana. Kuna mtu aliwahi kutoa takwimu zao halsi hapa hata mimi nikashangaa; nimandika hivi kwa kufuata takwimu hizo.
 
mzee heshima yako ni kubwa humu JF ... pls check source yako .. then rekebisha.
 
Hii topiki iliwahi kujadiliwa hapa JF siku nyingi sana sisi wengine tukiwa spectators, na takwimu zikawekwa kavu kavu ambazo zilinitisha hata mimi. Nobody disputed the validity of those arguments then, hivyo they are still valid. Wale wachache wenye Ph.D ni viongozi kama vile Deans na Directors hasa waliostaafu kutoka Muhimbili College of Medicine ya Wakati huo; ile wanaofundisha madarasani wengi ni MD tu.

Hata hivyo nitachukua muda kutajitafutia facts zaidi ya kukubaliana na arguments hizo tu.
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Ma MD wengi wa miaka hii, wako substandard na wamejaa ego ya kishamba.

Kwa kifupi ni ma CO waliochangamka tu, uwezo wao unatia shaka sana.

Ukiweza katibiwe na specialist tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wakati Sasa kupitia forum ya wanataaluma wenzio muhamasishane kuipenda kazi yenu

Wiki iliyopita manusura nimpoteze mwanangu kwa uzembe wa daktari aliyemu attend mwanzo

Mtoto alikuwa na mafua, kikohozi lakini kila akijaribu kula alikuwa anatapika

Kwa hali hiyo nikampeleka hizi mnazoita polyclinic

Cha kushangaza, naelezea history ya mgonjwa aliposikia mafua na kikohozi hakuona haja hata ya kumchukua vipimo. Alichofanya ni kuandika dawa za centrizen, ya kikohozi na Panadol tu

Dawa hizo hazikumpa ahueni yoyote mwanangu
Baada ya siku mbili baada ya kuona hawezi kula chochote nikaona nirudi tena pale pale wanapofahamu history ya mgonjwa

Nikajaribu kuforce angalua apimwe damu, choo na mkojo (hii ni baada ya Dr kusema mtoto shida.ni mafua tu)

Vipimo vya lab vikaje negative vyote

Siku iliyofuata mchana mtoto akakakamaa, hajiwezi kwa.lolote, kifupi tulimkimbiza hospital akiwa hajitambui na viungo vyote vimelegea hadi kufumba mdomo hawezi

Kwenda hospital ya rufaa, waliompokea.emegency ilibidi waanze na sindano ya.kurudisha uhai (feno)

Vipimo vya awali vikaonyesha alikuwa na homa kali ambayo endapo tunge delay matokoea yasingekuwa mazuri

Hapo ndo nilipochoka.na.kujiuliza.kwanini hii homa haikuonekana.siku zote wakati nilieleza.mtoto kila akila.ana tapika kiasi cha Dr aliyenipokea.kusema tumezembea kumpeleka mtoto hospital mapema

Kuna madktari wanafanya kazi bila.kujali weledi wa kazi yao hasa hasa hivi vituo binafsi ambavyo Zamani tuliviamini
Pole sana mkuu..imenisikitisha hii!
 
Hawa matabibu vijana hata akijuchukua damu labda ya typhoid, anachomachoma anarudia Mara nyingi, alafu unasikia maimivu, Ila ukichomwa na watu wazima Mara moja tu na maumivu hakuna.
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Shida ya kumeza Viagra halafu demu asije ingeweza kukuletea tatizo kubwa sana la moyo.
 
Pole sana mkuu,hii ndio aina ya Wasomi tulionao nchini mwetu.
 
Jana nilikutana na classmate wangu mmoja MD pale Kinyerezi Park anakula bia kama hana akili, totoz ndo usiseme.

kila mtu ashinde mechi zake.
Kama anakula bia mda sio wa kazi haina noma
 
Swala sio mganga hajigangi.

Swala ni kuwa unaweza jua tatizo kwa kuhisi tu maana tayari wewe ni daktari unajua kabisa kuwa hapa tatizo ni hili na lile na sio swala la kuona pulse rate au kutumia steto kusikiliza mapigo ya moyo na sauti.

Mi si daktari ila huwa naweza fanya diagnosis ya mwenyewe.

Kama matatizo ya moyo unayo maana yake utakuwa na dawa ndani.
Hayo unayoyafanya huna tofauti na waganga wa kienyeji

Ungekuwa una ABC za taaluma hyo ungeelewa haraka
 
Back
Top Bottom