Madaktari wanaziona Sana sehemu za Siri , haiwaathiri kweli hii?

Madaktari wanaziona Sana sehemu za Siri , haiwaathiri kweli hii?

Mkuu hii niliwahi kusimuliwa kuwa jamaa alikua akifanya huduma ya massage kwa wanawake zaidi. Hisia za kufanya tendo la ndoa zilimuisha na sio kwamba alipatwa na ugonjwa ila lilikua imemuathiri kisaikolojia.

Basi akapewa case kuwa amekua hanithi ila jamaa hakukubali maana huko nyuma alikua sawa tu, ndio kumuona huyo mtaalamu wa saikolojia aliyekua akisimulia kisa hiki.

Akashauriwa kuacha kazi hiyo ya massage na akashauriwa kujipa likizo kwenda huko kijijini kwao mkoa wa Pwani ambako stara ni kubwa, alikaa huko kama miezi miwili mabadiliko yakaanza na baada ya miezi kadhaa mbeleni akarudi hali ya kawaida japo haikua kwa ufanisi wa awali.
Hili ni tatizo huwapata hata wale vijana wa kuremba kucha wanawake na madaktari wanaohusika na wanawake na maungo yao ni vile watu hukimbilia kusema kuwa hawana nguvu za kiume kumbe tayari wameshaathirika kisaikolojia hawasisimki tena maana vinavyosisimua ni sehemu yao ya kazi kila siku tena huchezea kwa kiasi wapendavyo.
Sasa ili kwenda sawa na kazi, wanailazmisha akili kuchukulia hilo jambo ni la kawaida kumbe jinsi muda unavyoenda ndio anazidi kujiharibu pasipo kujua hadi inafika hatua anamfanyia massage mwanamke mrembo lakini hasisimki tena na hii inamtafuna hadi kwa wanawake wengine kias cha kupelekea kushindwa kabisa kusisimka kimapenzi.
Hatari sanaaa.

Wapo hatarini sana
 
Back
Top Bottom