Madaktari wauaji Mt. Meru Hospital arusha

Aisee nimekumbuka!ile video ya hili sakata bado haijakamilika kutengenezwa?hebu ilete jamvini tuwekane sawa!

huyu mara amerekodi mara ataleta mgojwa yani anachanganya!huyu ni wale relatives wanaokuwa na dharau kwa sababu ya vijisenti!anatia kinyaa anapokiri walitoa rushwa for what?anachefua anaposema hakuongea na dr kwa sababu angetengeneza mazingira ya rushwa!ina maana wewe unazo sana au dk ana njaa sana?mara ngapi wagonjwa tunawanunulia dawa chakula na nauli za kurudi kwao?au kwa vile umeamua kuongelea uuaji wetu ambao umetupandikizia?hakuna mwanadamu mkamilifu ila huwa nasema MUNGU anaona yote na ndie hakimu mwaminifu!
 
Waswahili wana akili sana,walifahamu kuna watu wanaweza kuwatukana madaktari mfano mzuri ni mvumbuzi.

Usitukane wakunga........

Huyo mgonjwa wako akitoka oceanroad atarudi hapo hapo mt meru,mark my words!!

what a stupid comment, so what if he comes back to Mt Meru. What is it that you are trying say? You dont have to comment if you are empty headed.

In case you are confused this thread has nothing to do with the patient. Get it.
 
i dont believe this post!!!

You must have some serious issues somewhere................
 
what are a stupid comment, so what if he comes back to Mt Meru. What is it that you trying say here? You dont have to comment if you are empty headed.

In case you are confused this thread has nothing to do with the patient. Get it.

wahenga wana busara kuliko wewe!ndio maana waliyasema hayo,sio maneno yangu bali ni ya wahenga.

Chukua na hii hapa...
"USITUKANE MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO"
 
kwenye mahospitali kuna complaining boxes ni vyema ukatoa complaining hizo utasaidia kuokoa maisha ya watu kwa haraka zaidi.



 
mvumbuzi si madaktari wote hawako makini,wapo mdaktari wanaopenda kazi yao, lakini pia ni kweli kuna baadhi hovyo na sijui ni uzembe,kuna baba tumemzika majuzi tu kwasababu ya uzembe wa madaktari, alikuwa anajisikia vibaya akaenda hospitali akapimwa na kuenda kuchukua majibu akaambiwa ana kifua kikuu basi wakamwandikia madawa akaanza kumeza,badala ya kupata nafuu mgonjwa akazidiwa sana ikabidi apelekwe hospitali tena wakagundua kuwa yule baba ana tatizo la ini na sababu ni hizo dawa alizotumia maana hakuwa na huo ugonjwa wa kifua kikuu madaktari walimpa majibu ya mtu mwingine.





 
Mkuu wetu Ngongo,

Salaam Maridhawa!

Aidha natoa shukran nyingi kwako kwa uchunguzi wako katika jitihada za kujaribu kufuatilia sakata hili la Dr. Israel!
Ila ninachokushauri, uchunguzi wako wa siku moja, na zaidi sana huenda ni kwa dakika 30 or so, haufai kudraw conclusion uliyofikia!
Kwa muda uliotumia naamini hukupata aina za watu wanaostahiki kuwekwa katika samples za uchunguzi....
Kuna mahali umesema kuwa uliuliza watu wa maabara...(GOOSH!!!!), unategemea nini na watu wa maabara ambao ni staff wenzie?, ni kesi ya nyani hii mkuu!
Aina nzuri ya uchunguzi ingehusisha simulation ya kuwa na mgonjwa, na apatikane huyo Dr Israel mwenyewe ili ashikishwe mgonjwa 'ghost'!
Lakini hata hivyo si guaranteekwamba atamtreat vibaya.

Aidha uchunguzi wako, hata kama ungekuwa ni wa aina ya questionaire ungefanywa kwa wagonjwa waliowahi kutibiwa naye, na si kuwauliza staff wa maabara as you did!
Vinginevyo nakushukuru kwa kutoa taarifa za awali za maelezo binafsi ya Dr Israel!
 
Visioner poleni kwa huyo mgonjwa wenu..mambo mengi hutokea hospitalini and some individuals mismanage their patients.but don loose faith in this generation ya sasa coz we know why we chose this proffesion and kiasi flani serikali inajitahidi coz kwa serikali si ndo tunapokea the highest amount of salary so money is no longer an issue when it comes to treating my patients..
 


Mkuu Dr Chichi,

Mkuu binafsi simjui Dr Israel ila nimeongea na baadhi ya maDr hapo Mt Meru ambao wamenihakikishia watamfikishia ujumbe.
 

Heshima kwako PakaJimmy.

Mkuu uko sawa kabisa.
Nilizungumza na watu wa maabara,X-ray,Medical Records,Drs,baadhi ya wagonjwa wodi namba 6 na Clinic Officers ambao wamefanya kazi kwa karibu sana na Dr Israel.Sikuishia hapo tu bali niliwataka wamfikishie ujumbe Dr Israel awe makini na kazi yake hasa ukizingatia ndio kwanza anaanza safari yake ndefu katika fani ya uDr.Nikiri wapo walioshangaa Dr kupokea na kutekeleza amri ya Nurse wengine waliconclude inatokana na uzoefu mdogo.
 
Chichi, Jackbour, Mchapakazi najua ninyi ni madakatari na kinachowafanya muwe wagumu kuelewa ni uzalendo kwa kazi yenu.

Nataka nieleze muelewe kilichofanya mgonjwa kufikishwa mount Meru kwanza. Mgonjwa alishindwa kupitisha chakula kwenye koo na akashinda njaa siku tatu na ikaonekana apelekwe mt. Meru hospitali siyo kutibiwa bali wafanye namna aweze kula au kwa uwezo wao kama madaktari watafute alternative ili apate nguvu huku mipango mingine ya kumsaidia ikiendelea. Ieleweke kwamba familia ya mgonjwa siyo matajiri bali watu wa kima cha chini ambao wasingeweza kuwa na fedha ya haraka kuweza kumpeleka mgonjwa aidha KCMC au Ocean road kama Chichi anavyosema. Hii familia ilihitaji angalau wiki kadhaa kuwasiliana na ndugu zao ili kupata michango ya fedha ya kuwezesha kufanya hilo zoezi lakini wakaona ni vema wamkimbize mgonjwa kwenye hospitali ya Mt. Meru ambayo kwa kawaida ndiyo kimbilio la watanzania wa kada ya kati na chini kiuchumi. Ndivyo ilivyo pia kwa hospitali nyingi za serikali pia. Siku ya kwanza kuwa admitted kwa kipindi cha masaa 24 akawa amepatiwa drip 3 ambazo hazikutoka tu hivihivi bali kuna Nurse alipewa kitu kidogo cha Tshs. 2000 ndo akawajibika. Baada ya hizo drip 3 mgonjwa akawa amechangamka kiasi na akawa anaongea vizuri na pia kuanza kwenda maliwato mwenyewe.

Mgonjwa alijua fika kwamba kilichompatia nguvu ile ni drip na ikawa imepita siku moja bila mgonjwa kupewa drip nyingine na alipowaomba ma nurse wampatie drip walimpuuzia na mara nyingine walimjibu ovyo. Nini kimetokea hapa mbona siku ya kwanza walipopewa rushwa ya Tsh. 2000 wali cooperate vizuri tu ila sasa hawajapewa chochote wanaanza vitimbi kwa mgonjwa?

Siku ya tatu hamna treatment yoyote aliyopewa mgonjwa ilihali wakijua alitakiwa apate walitakiwa watumie utu angalau mgonjwa apate nafuu na ndugu zake wawe wamepata fedha za kum transfer mgonjwa.
Siku ya nne mgonjwa akiwa anasubiri round ya madaktari akaambiwa anakuwa discharged aende KCMC kana kwamba hospitali ilikuwa imefanya arrangement zozote. Mgonjwa alipojaribu kumsihi nurse kusubiri angalau siku mbili ili apate nguvu kidogo ndo mpe discharge nurse akakataa na kuanza ku- tease kwamba amechanganyikiwa. Yeye mgonjwa alisema drip ilimsaidia sana na alimwomba nurse angalau ampe nyingine lakini nurse akasema NO.

Ndugu wa mgonjwa walipofika hospitalini kumjulia hali mgonjwa tukamkuta mgonjwa analalama kwamba wamemlazimishia discharge wakati bado hajisikii vema na kwamba Dr. Israeli Kassago alipotaka awekewe drip nurse aliyekuwa na toroli cha dawa akamkataza basi Dr. Israeli Kassago akaghairi na kukubali ushauri wa huyu nurse kumdischarge. Ndugu walipofika walipewa tu taarifa bila consultation yoyote ya kwa nini wanaharakisha discharge namna hiyo huku akisisitiza apelekwa KCMC bila kutoa muda kwa mke wa mgonjwa kujiandaa wakati wanajua arrangement zote hizo zingehitaji fedha ambazo hazikuwepo.

Ninasikitishwa sana na comments za hao ndugu hapo juu wanaoona kuwa alichofanyiwa mgonjwa ni sawa kwani inadhihirisha ni jinsi gani hawana chembe ya utu haswa ukizingatia kazi wanayofanya ni ya ku-serve maisha ya binadamu wenzao. Hapa sifanyi siasa wala visasi bali nimeamua kuujulisha umma wa watanzania na wahusika wakuu katika ngazi husika ya maamuzi mistreatment ambazo watu wa kada za chini na wasio kuwa na sauti wanafanyiwa na watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia.

Wakati umefika kwa vyombo husika kuchukua hatua stahiki ili kuondoa watu wa namna hii ambao wanakuwa kikwazo kikubwa si tu cha kuongeza matumaini ya watanzania kwenye idara au taasisi hii nyeti kwa afya ya nguvu kazi ya taifa bali wanaorudisha nyuma juhudi za Wizara ya afya kuboresha utendaji wake katika kuwahudumia watanzania.
 


I agree with your desperate comments!!!!
 

Nafikiri umempata vema ngongo ambaye ni home boy wangu pia . Utafiti uliofanya umesaidia kujua Dr. Isareli Kassago ni nani ila please atusaidie kumpata yule Nesi aliyem-mislead na kusababisha kuibuka kwa mjadala huu
 

mkuu huna haja ya kurudia rudia kilichotokea kwa sababu huaminiki.
Nachotaka ukielewe ni kwamba mchukulie daktari kama fundi makenika ambaye akimaliza kutengeneza gari na kulipiga stata likawaka bila tabu basi fundi huyu huona raha na mara nyingine hujisifu.
Ukweli ni kuwa daktari hupata faraja once anapoona mgonjwa wake hana hatari ya kufa.
Wapo baadhi ya madaktari(quacks) ambao hawaendani na misingi ya udaktari sio hapa tanzania pekee bali ulimwenguni kote,kuna madaktari wanaotumia ujuzi wao kutengeneza biological weapons n.k.
Pamoja na mapungufu haya huwezi kusikia mtu muungwana akisema madaktari wa dunia hii ni wauaji.
Jaribu kuwa makini na kauli zako kuna siku utasema waislamu ni wauaji au wakristu ni wachawi,hapa utaspark vita ya kidini na hutapata muda wa kuexplain.
 

Hapa tayari unaafikiana na mimi kuhusu tukio lenyewe ila ukisema problem ni lugha iliyotumika kwenye heading ya hii habari naweza sema imekuwa kali sana kwenu madaktari. Mlitaka pengine ni specify nipunguze harshness ya lugha. Inawezekana ningetumia lugha tofauti hata wewe usingeoona hii habari kama inakuhusu lakini kwa lugha hii ime- catch your attention na ukaamua kuchangia. Ukweli ni kwamba kitendo alichofanya Dakatari hakikuwa cha kiuaji ila dhamira ya huyo daktari ndiyo ilikuwa ya aondoke akafie mbali kwani he is too close to the grave" . Nikupeni tu taarifa ni kwamba mgonjwa tulimpeleka hospitali nyingine na hadi sasa ameweza kunywa uji bila tatizo huku akiwa na nguvu kubwa tu tayari hata tukimtransfer tunajua atasafiri na kufika salama. Ila tungem transfer wakati ule alipofanyiwa discharge Mt. Meru ingewezekan saa 1 jioni isingefika kwani hata kama angeondoka kwenda KCMC kuna procedures ambazo lazima angepitia including registration n.k na zingesababisha hali yake iwe mbaya zaidi. Tunamshukuru Mungu hakufa kama walivyokuwa wanataka!!
 
Ngongo,
Ulifanya kazi ya heshima kama uliweza kutoa maagizo hayo hapo kwenye 'red"!
Naamini kama anaamini katika Nguvu ya Umma, na kujali viapo vyake, basi atageuza tabia yake ya kusikiliza mashauri ya Nesi badala ya kutumia maadili ya udaktari!
Nakushukuru tena kiongozi!
 

nashukuru kuona hatimaye unanielewa!
Kubali lugha uliyotumia si ya kiungwana ni lugha ambayo hutumiwa na magazeti ya udaku,jitahidi sana kuepuka lugha hiyo kwani itakushushia credibility.naona sasa hata dr.israel unamuondoa kwenye 'tendo' la uuaji na unaanza kusema juu ya 'dhamira' yake ambayo kuithibitisha ni ngumu zaidi.
Naamini mgonjwa wako yuko vizuri kama ulivyosema,akizidiwa usisite kumrudisha mt meru na 'ukihisi' hatendewi vizuri report immidiately kwa incharge wa wodi,incharge wa hospital,RMO,Polisi halafu ndio ulete bandiko hapa!
Wewe ni msomi(naamini hivyo) na approach yako ya kutatua tatizo ni lazima itofautiane na wahuni wa mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…