Madaktari wauaji Mt. Meru Hospital arusha

Aisee nimekumbuka!ile video ya hili sakata bado haijakamilika kutengenezwa?hebu ilete jamvini tuwekane sawa!

huyu mara amerekodi mara ataleta mgojwa yani anachanganya!huyu ni wale relatives wanaokuwa na dharau kwa sababu ya vijisenti!anatia kinyaa anapokiri walitoa rushwa for what?anachefua anaposema hakuongea na dr kwa sababu angetengeneza mazingira ya rushwa!ina maana wewe unazo sana au dk ana njaa sana?mara ngapi wagonjwa tunawanunulia dawa chakula na nauli za kurudi kwao?au kwa vile umeamua kuongelea uuaji wetu ambao umetupandikizia?hakuna mwanadamu mkamilifu ila huwa nasema MUNGU anaona yote na ndie hakimu mwaminifu!
 
Waswahili wana akili sana,walifahamu kuna watu wanaweza kuwatukana madaktari mfano mzuri ni mvumbuzi.

Usitukane wakunga........

Huyo mgonjwa wako akitoka oceanroad atarudi hapo hapo mt meru,mark my words!!

what a stupid comment, so what if he comes back to Mt Meru. What is it that you are trying say? You dont have to comment if you are empty headed.

In case you are confused this thread has nothing to do with the patient. Get it.
 
Nikuambie tu ndugu yangu wengi wanaopingana na mimi hapa ni madokta wa hii hospitali na wengine ni nawafahamu. Kujibu ninavyojibu nina fanya deliberately na sio kwamba sina majibu lakini sio kila kitu ni cha kutolea jibu. Hivi unataka nikiulizwa i ninapokutana na mke wangu kitandani huwa ninafanya nini basi nijibu kirahisi tu? Mimi siyo zuzu kwani kuna siri za mgonjwa hapa na mimi siwezi kujibu kila kitu hata ambacho hakitajenga wala kusaidia. Kwa hiyo usitegemee nijibu kila swali hata ambalo halina maana kwani hapa hatufanyi job interview.
i dont believe this post!!!

You must have some serious issues somewhere................
 
what are a stupid comment, so what if he comes back to Mt Meru. What is it that you trying say here? You dont have to comment if you are empty headed.

In case you are confused this thread has nothing to do with the patient. Get it.

wahenga wana busara kuliko wewe!ndio maana waliyasema hayo,sio maneno yangu bali ni ya wahenga.

Chukua na hii hapa...
"USITUKANE MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO"
 
kwenye mahospitali kuna complaining boxes ni vyema ukatoa complaining hizo utasaidia kuokoa maisha ya watu kwa haraka zaidi.

Baadhi ya madaktari na Manesi katika hospitali ya Mt .Meru Arusha wamethibitika kufanya kile ambacho watu wengi wamekuwa wakikilalamikia licha ya wao kuendelea kukana uovu huo. Imedhihirika kwamba baadhi ya madaktari wamekuwa wakitumia taaluma yao vibaya kwa kuharakisha vifo vya wagonjwa badala ya kuwapa huduma itakayo wawezesha kuongeza angalau siku kadhaa za kuishi na kufurahiwa na watoto, wake, waume, wazazi na hata ndugu zao.

Uchunguzi uliofanywa siku tatu mfululizo katika wodi namba 6 ya wanaume umeshuhudia madaktari vijana wakishawishiwa na manesi wazoefu wa kuua (a.k.a watoa roho za watu) ili kuwanyima baadhi ya wagonjwa drip makusudi ili zibaki za kuuza kwa kisingizio kwamba ugonjwa wake hauwezi tibika na kwamba drip haimsadii chochote. Hali hii ilijidhihirisha pale mgonjwa mmoja aliyekuwa na tatizo la kumeza chakula alipoletwa na ndugu zake ili angalau apate drip ya Glucose zimwongezee nguvu huku wakitafuta utaratibu wa kumpeleka KCMC. Siku alipoletwa ndugu hawa waliwapa Manesi Shilingi 2000 na ndugu yao akawekewa drip tatu. Siku iliyofuata manesi hawakupewa hela kwa hiyo wakamwekea drip moja tu kwa masaa 24 ilihali wakijua kabisa mgonjwa huyu alikuwa anategemea drip kama chakula.
Tatizo la mgonjwa lilikuwa ni chakula tu kwani alikuwa anaongea vizuri na kutembea mwenyewe bila shida yoyote. Nesi mmoja aliyekuwa zamu siku ya Jumanne saa sita na nusu mchana tarehe 3/5/2011 katika wodi 6 ya wanaume na Dk aitwaye Israeli Kasago wakaenda mbali na kumpa discharge kuliko wampe drip ambazo siyo mali yao bali zimegharamiwa na fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwasaidia watanzania.

Mgonjwa alipoomba kuwekewa drip ili ake angalau apate nguvu kidogo yule nesi akamkataza Dr. Israeli Kasago na alipoulizwa kwa nini anafanya hivyo akasema huyu mgonjwa amechanganyikiwa. Niliposikia hivyo nilitaka kumzaba kofi au ngumi ila hekima ikanizuia.
Wasifu wa huyu Nesi aliyekuwa zamu siku ya tarehe 3/5/2011 saa sita na nusu mchana hadi saa 7:20 ni Mnene mweupe aliyekuwa amevalia white . Sikufanikiwa kupata jina lake ila niliambiwa ni mmachame feki kwani wamachame ninavyowafahamu hawana roho mbaya hivyo.

Ndugu zake wakamwomba angalau mgonjwa apewe drip wakati wanajipanga kifedha kumhamishia KCMC lakini huyu Dr. Akamsikiliza zaidi huyu Nesi muuaji badala ya kutumia taaluma yake na hivyo kwa makusudi wakam-discharge mgonjwa akafie mbali. Katika siku hiyo hiyo wagonjwa wengine watatu ambao pia hali zao zilikuwa mbaya wakaandikiwa discharge waondoke wodini kwa sababu tu Manesi hawapati chochote kutoka kwao.

Katika hali kama hii sichelei kusema kwamba Wataalam hawa waliosoma kwa kodi za wagonjwa haohao na watanzania kwa ujumla balala ya kutumia taaluma yao kutetea uhai wa watanzania wamekuwa wakiharakisha mauti yao.
Hii ni dhambi na ninajua vyama vyao vitawatetea ila ukweli utabakia kuwa ukweli kwa ninayooandika hapa nimeyashuhudia mimi mwenyewe na nathubutu kuwaita hawa “madaktari wauaji kwani kwa siku tatu za uchunguzi mambo waliokuwa wakiwafanyia wagonjwa yamethitisha kwamba ndiyo tabia yao.”.
 
mvumbuzi si madaktari wote hawako makini,wapo mdaktari wanaopenda kazi yao, lakini pia ni kweli kuna baadhi hovyo na sijui ni uzembe,kuna baba tumemzika majuzi tu kwasababu ya uzembe wa madaktari, alikuwa anajisikia vibaya akaenda hospitali akapimwa na kuenda kuchukua majibu akaambiwa ana kifua kikuu basi wakamwandikia madawa akaanza kumeza,badala ya kupata nafuu mgonjwa akazidiwa sana ikabidi apelekwe hospitali tena wakagundua kuwa yule baba ana tatizo la ini na sababu ni hizo dawa alizotumia maana hakuwa na huo ugonjwa wa kifua kikuu madaktari walimpa majibu ya mtu mwingine.

Madaktari na wauguzi ndio wanatakiwa watu-prove wrong kwa kuonyesha kuwa malalamiko lukuki ya wagonjwa si ya kweli na si kusema mtoa mada aombe radhi. hakuna radhi hapa kwani tayari kuna tatizo. angalia na wewe inawezekana ni Nurse au doctor kwani huna hata uwezo wa kufikiri sawa. Who told you kwamba mgonjwa alikotoka kulikuwa na zahanati karibu au ulifikiri ndugu zake wamemleta Mt. Meru kumekuwa Ngurdoto Hoteli au Mbuga za wanyama kutalii?. Kimbilio lilikuwa ni hapo Mt. Meru lakini waka mwa-abuse mgonjwa pamoja na taaluma yao.

Its very ridiculous unawatetea watu ambao kwa judgement yangu hawana raha wakiona mortuary iko tupu. Ipo siku nao wataingia.

It seem hujafanya utafiti sawasawa it seem wewe nawe ni daktari ila kama hauko hivyo basi niliokutana nao within this time ni wa aina ninayoelezea hapa.
 
Heshima kwako Mvumbuzi,

Mkuu leo nimepita Mt Meru Hospital nimedodosa habari ulizozileta jamvini nimegundua mambo yafuatayo.

Dr Israel simwajiriwa wa Mt Meru Hospital yuko kwaajili ya mazoezi [Internship].

Mkuu Dr Israel ni mchapakazi na hodari sana hana sifa mbaya ,mambo uliyoandika yana lengo la kumharibia.Nimeuliza watu wengi tena vitengo tofauti eg Maabara,X-Rays na Paramedical ilikujiridhisha na uchunguzi wangu usiokuwa rasmi.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu wetu Ngongo,

Salaam Maridhawa!

Aidha natoa shukran nyingi kwako kwa uchunguzi wako katika jitihada za kujaribu kufuatilia sakata hili la Dr. Israel!
Ila ninachokushauri, uchunguzi wako wa siku moja, na zaidi sana huenda ni kwa dakika 30 or so, haufai kudraw conclusion uliyofikia!
Kwa muda uliotumia naamini hukupata aina za watu wanaostahiki kuwekwa katika samples za uchunguzi....
Kuna mahali umesema kuwa uliuliza watu wa maabara...(GOOSH!!!!), unategemea nini na watu wa maabara ambao ni staff wenzie?, ni kesi ya nyani hii mkuu!
Aina nzuri ya uchunguzi ingehusisha simulation ya kuwa na mgonjwa, na apatikane huyo Dr Israel mwenyewe ili ashikishwe mgonjwa 'ghost'!
Lakini hata hivyo si guaranteekwamba atamtreat vibaya.

Aidha uchunguzi wako, hata kama ungekuwa ni wa aina ya questionaire ungefanywa kwa wagonjwa waliowahi kutibiwa naye, na si kuwauliza staff wa maabara as you did!
Vinginevyo nakushukuru kwa kutoa taarifa za awali za maelezo binafsi ya Dr Israel!
 
Visioner poleni kwa huyo mgonjwa wenu..mambo mengi hutokea hospitalini and some individuals mismanage their patients.but don loose faith in this generation ya sasa coz we know why we chose this proffesion and kiasi flani serikali inajitahidi coz kwa serikali si ndo tunapokea the highest amount of salary so money is no longer an issue when it comes to treating my patients..
 
Kaka umeniuliza nina uhakika gani na hizo transfer.umejikanyaga mwenyewe ndugu yangu,umeandika walisuspect ana escc(esophageal squamous cell carcinoma).mgonjwa kama huyo direct watakuambia uende ocean road coz escc is radiosensitive.nina uhakika mgonjwa wako alikuwa na uwezo wa kumeza liquid foods otherwise usingeandika kuwa mgonjwa ana uwezo wa kutembea coz mtu ambaye angekuwa hypoglycaemic kutokana na kutokula angekuwa weak and bed ridden.also i believe ungeongea na dr.israel personally umueleze malalamiko yako coz kulalamika hapa does not gurantee kwamba ataiona hii thread so point yako kuwa hii ni changamoto kwake is invalid

Mkuu Dr Chichi,

Mkuu binafsi simjui Dr Israel ila nimeongea na baadhi ya maDr hapo Mt Meru ambao wamenihakikishia watamfikishia ujumbe.
 
Mkuu wetu Ngongo,

Salaam Maridhawa!

Aidha natoa shukran nyingi kwako kwa uchunguzi wako katika jitihada za kujaribu kufuatilia sakata hili la Dr. Israel!
Ila ninachokushauri, uchunguzi wako wa siku moja, na zaidi sana huenda ni kwa dakika 30 or so, haufai kudraw conclusion uliyofikia!
Kwa muda uliotumia naamini hukupata aina za watu wanaostahiki kuwekwa katika samples za uchunguzi....
Kuna mahali umesema kuwa uliuliza watu wa maabara...(GOOSH!!!!), unategemea nini na watu wa maabara ambao ni staff wenzie?, ni kesi ya nyani hii mkuu!
Aina nzuri ya uchunguzi ingehusisha simulation ya kuwa na mgonjwa, na apatikane huyo Dr Israel mwenyewe ili ashikishwe mgonjwa 'ghost'!
Lakini hata hivyo si guaranteekwamba atamtreat vibaya.

Aidha uchunguzi wako, hata kama ungekuwa ni wa aina ya questionaire ungefanywa kwa wagonjwa waliowahi kutibiwa naye, na si kuwauliza staff wa maabara as you did!
Vinginevyo nakushukuru kwa kutoa taarifa za awali za maelezo binafsi ya Dr Israel!

Heshima kwako PakaJimmy.

Mkuu uko sawa kabisa.
Nilizungumza na watu wa maabara,X-ray,Medical Records,Drs,baadhi ya wagonjwa wodi namba 6 na Clinic Officers ambao wamefanya kazi kwa karibu sana na Dr Israel.Sikuishia hapo tu bali niliwataka wamfikishie ujumbe Dr Israel awe makini na kazi yake hasa ukizingatia ndio kwanza anaanza safari yake ndefu katika fani ya uDr.Nikiri wapo walioshangaa Dr kupokea na kutekeleza amri ya Nurse wengine waliconclude inatokana na uzoefu mdogo.
 
Chichi, Jackbour, Mchapakazi najua ninyi ni madakatari na kinachowafanya muwe wagumu kuelewa ni uzalendo kwa kazi yenu.

Nataka nieleze muelewe kilichofanya mgonjwa kufikishwa mount Meru kwanza. Mgonjwa alishindwa kupitisha chakula kwenye koo na akashinda njaa siku tatu na ikaonekana apelekwe mt. Meru hospitali siyo kutibiwa bali wafanye namna aweze kula au kwa uwezo wao kama madaktari watafute alternative ili apate nguvu huku mipango mingine ya kumsaidia ikiendelea. Ieleweke kwamba familia ya mgonjwa siyo matajiri bali watu wa kima cha chini ambao wasingeweza kuwa na fedha ya haraka kuweza kumpeleka mgonjwa aidha KCMC au Ocean road kama Chichi anavyosema. Hii familia ilihitaji angalau wiki kadhaa kuwasiliana na ndugu zao ili kupata michango ya fedha ya kuwezesha kufanya hilo zoezi lakini wakaona ni vema wamkimbize mgonjwa kwenye hospitali ya Mt. Meru ambayo kwa kawaida ndiyo kimbilio la watanzania wa kada ya kati na chini kiuchumi. Ndivyo ilivyo pia kwa hospitali nyingi za serikali pia. Siku ya kwanza kuwa admitted kwa kipindi cha masaa 24 akawa amepatiwa drip 3 ambazo hazikutoka tu hivihivi bali kuna Nurse alipewa kitu kidogo cha Tshs. 2000 ndo akawajibika. Baada ya hizo drip 3 mgonjwa akawa amechangamka kiasi na akawa anaongea vizuri na pia kuanza kwenda maliwato mwenyewe.

Mgonjwa alijua fika kwamba kilichompatia nguvu ile ni drip na ikawa imepita siku moja bila mgonjwa kupewa drip nyingine na alipowaomba ma nurse wampatie drip walimpuuzia na mara nyingine walimjibu ovyo. Nini kimetokea hapa mbona siku ya kwanza walipopewa rushwa ya Tsh. 2000 wali cooperate vizuri tu ila sasa hawajapewa chochote wanaanza vitimbi kwa mgonjwa?

Siku ya tatu hamna treatment yoyote aliyopewa mgonjwa ilihali wakijua alitakiwa apate walitakiwa watumie utu angalau mgonjwa apate nafuu na ndugu zake wawe wamepata fedha za kum transfer mgonjwa.
Siku ya nne mgonjwa akiwa anasubiri round ya madaktari akaambiwa anakuwa discharged aende KCMC kana kwamba hospitali ilikuwa imefanya arrangement zozote. Mgonjwa alipojaribu kumsihi nurse kusubiri angalau siku mbili ili apate nguvu kidogo ndo mpe discharge nurse akakataa na kuanza ku- tease kwamba amechanganyikiwa. Yeye mgonjwa alisema drip ilimsaidia sana na alimwomba nurse angalau ampe nyingine lakini nurse akasema NO.

Ndugu wa mgonjwa walipofika hospitalini kumjulia hali mgonjwa tukamkuta mgonjwa analalama kwamba wamemlazimishia discharge wakati bado hajisikii vema na kwamba Dr. Israeli Kassago alipotaka awekewe drip nurse aliyekuwa na toroli cha dawa akamkataza basi Dr. Israeli Kassago akaghairi na kukubali ushauri wa huyu nurse kumdischarge. Ndugu walipofika walipewa tu taarifa bila consultation yoyote ya kwa nini wanaharakisha discharge namna hiyo huku akisisitiza apelekwa KCMC bila kutoa muda kwa mke wa mgonjwa kujiandaa wakati wanajua arrangement zote hizo zingehitaji fedha ambazo hazikuwepo.

Ninasikitishwa sana na comments za hao ndugu hapo juu wanaoona kuwa alichofanyiwa mgonjwa ni sawa kwani inadhihirisha ni jinsi gani hawana chembe ya utu haswa ukizingatia kazi wanayofanya ni ya ku-serve maisha ya binadamu wenzao. Hapa sifanyi siasa wala visasi bali nimeamua kuujulisha umma wa watanzania na wahusika wakuu katika ngazi husika ya maamuzi mistreatment ambazo watu wa kada za chini na wasio kuwa na sauti wanafanyiwa na watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia.

Wakati umefika kwa vyombo husika kuchukua hatua stahiki ili kuondoa watu wa namna hii ambao wanakuwa kikwazo kikubwa si tu cha kuongeza matumaini ya watanzania kwenye idara au taasisi hii nyeti kwa afya ya nguvu kazi ya taifa bali wanaorudisha nyuma juhudi za Wizara ya afya kuboresha utendaji wake katika kuwahudumia watanzania.
 
Kaka i rest my case.you are beyond an intelectual discussion.we took an oath and by God we shall stand by it.we shall treat every patient with dignity respect and love despite of what you call us or say about us,sioni umuhimu wa kuwaonea wagonjwa because of your pathetic opinions.kaka hata ukimrudisha mgonjwa wako we will welcome him with both hands.watu wana mentality that we doctors are heartless and after money but God knows we do feel your pain and we try our best to help u.mvumbuzi nimejaribu kukueleza management ya mgonjwa wako it seems u r still arrogant,anywayhukunisomesha wewe wala hukunipa degree wewe mimi nitatibu kama nilivyofundishwa na walimu wangu.case over

I agree with your desperate comments!!!!
 
Mkuu wetu Ngongo,

Salaam Maridhawa!

Aidha natoa shukran nyingi kwako kwa uchunguzi wako katika jitihada za kujaribu kufuatilia sakata hili la Dr. Israel!
Ila ninachokushauri, uchunguzi wako wa siku moja, na zaidi sana huenda ni kwa dakika 30 or so, haufai kudraw conclusion uliyofikia!
Kwa muda uliotumia naamini hukupata aina za watu wanaostahiki kuwekwa katika samples za uchunguzi....
Kuna mahali umesema kuwa uliuliza watu wa maabara...(GOOSH!!!!), unategemea nini na watu wa maabara ambao ni staff wenzie?, ni kesi ya nyani hii mkuu!
Aina nzuri ya uchunguzi ingehusisha simulation ya kuwa na mgonjwa, na apatikane huyo Dr Israel mwenyewe ili ashikishwe mgonjwa 'ghost'!
Lakini hata hivyo si guaranteekwamba atamtreat vibaya.

Aidha uchunguzi wako, hata kama ungekuwa ni wa aina ya questionaire ungefanywa kwa wagonjwa waliowahi kutibiwa naye, na si kuwauliza staff wa maabara as you did!
Vinginevyo nakushukuru kwa kutoa taarifa za awali za maelezo binafsi ya Dr Israel!

Nafikiri umempata vema ngongo ambaye ni home boy wangu pia . Utafiti uliofanya umesaidia kujua Dr. Isareli Kassago ni nani ila please atusaidie kumpata yule Nesi aliyem-mislead na kusababisha kuibuka kwa mjadala huu
 
Chichi, Jackbour, Mchapakazi najua ninyi ni madakatari na kinachowafanya muwe wagumu kuelewa ni uzalendo kwa kazi yenu.

Nataka nieleze muelewe kilichofanya mgonjwa kufikishwa mount Meru kwanza. Mgonjwa alishindwa kupitisha chakula kwenye koo na akashinda njaa siku tatu na ikaonekana apelekwe mt. Meru hospitali siyo kutibiwa bali wafanye namna aweze kula au kwa uwezo wao kama madaktari watafute alternative ili apate nguvu huku mipango mingine ya kumsaidia ikiendelea. Ieleweke kwamba familia ya mgonjwa siyo matajiri bali watu wa kima cha chini ambao wasingeweza kuwa na fedha ya haraka kuweza kumpeleka mgonjwa aidha KCMC au Ocean road kama Chichi anavyosema. Hii familia ilihitaji angalau wiki kadhaa kuwasiliana na ndugu zao ili kupata michango ya fedha ya kuwezesha kufanya hilo zoezi lakini wakaona ni vema wamkimbize mgonjwa kwenye hospitali ya Mt. Meru ambayo kwa kawaida ndiyo kimbilio la watanzania wa kada ya kati na chini kiuchumi. Ndivyo ilivyo pia kwa hospitali nyingi za serikali pia. Siku ya kwanza kuwa admitted kwa kipindi cha masaa 24 akawa amepatiwa drip 3 ambazo hazikutoka tu hivihivi bali kuna Nurse alipewa kitu kidogo cha Tshs. 2000 ndo akawajibika. Baada ya hizo drip 3 mgonjwa akawa amechangamka kiasi na akawa anaongea vizuri na pia kuanza kwenda maliwato mwenyewe.

Mgonjwa alijua fika kwamba kilichompatia nguvu ile ni drip na ikawa imepita siku moja bila mgonjwa kupewa drip nyingine na alipowaomba ma nurse wampatie drip walimpuuzia na mara nyingine walimjibu ovyo. Nini kimetokea hapa mbona siku ya kwanza walipopewa rushwa ya Tsh. 2000 wali cooperate vizuri tu ila sasa hawajapewa chochote wanaanza vitimbi kwa mgonjwa?

Siku ya tatu hamna treatment yoyote aliyopewa mgonjwa ilihali wakijua alitakiwa apate walitakiwa watumie utu angalau mgonjwa apate nafuu na ndugu zake wawe wamepata fedha za kum transfer mgonjwa.
Siku ya nne mgonjwa akiwa anasubiri round ya madaktari akaambiwa anakuwa discharged aende KCMC kana kwamba hospitali ilikuwa imefanya arrangement zozote. Mgonjwa alipojaribu kumsihi nurse kusubiri angalau siku mbili ili apate nguvu kidogo ndo mpe discharge nurse akakataa na kuanza ku- tease kwamba amechanganyikiwa. Yeye mgonjwa alisema drip ilimsaidia sana na alimwomba nurse angalau ampe nyingine lakini nurse akasema NO.

Ndugu wa mgonjwa walipofika hospitalini kumjulia hali mgonjwa tukamkuta mgonjwa analalama kwamba wamemlazimishia discharge wakati bado hajisikii vema na kwamba Dr. Israeli Kassago alipotaka awekewe drip nurse aliyekuwa na toroli cha dawa akamkataza basi Dr. Israeli Kassago akaghairi na kukubali ushauri wa huyu nurse kumdischarge. Ndugu walipofika walipewa tu taarifa bila consultation yoyote ya kwa nini wanaharakisha discharge namna hiyo huku akisisitiza apelekwa KCMC bila kutoa muda kwa mke wa mgonjwa kujiandaa wakati wanajua arrangement zote hizo zingehitaji fedha ambazo hazikuwepo.

Ninasikitishwa sana na comments za hao ndugu hapo juu wanaoona kuwa alichofanyiwa mgonjwa ni sawa kwani inadhihirisha ni jinsi gani hawana chembe ya utu haswa ukizingatia kazi wanayofanya ni ya ku-serve maisha ya binadamu wenzao. Hapa sifanyi siasa wala visasi bali nimeamua kuujulisha umma wa watanzania na wahusika wakuu katika ngazi husika ya maamuzi mistreatment ambazo watu wa kada za chini na wasio kuwa na sauti wanafanyiwa na watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia.

Wakati umefika kwa vyombo husika kuchukua hatua stahiki ili kuondoa watu wa namna hii ambao wanakuwa kikwazo kikubwa si tu cha kuongeza matumaini ya watanzania kwenye idara au taasisi hii nyeti kwa afya ya nguvu kazi ya taifa bali wanaorudisha nyuma juhudi za Wizara ya afya kuboresha utendaji wake katika kuwahudumia watanzania.

mkuu huna haja ya kurudia rudia kilichotokea kwa sababu huaminiki.
Nachotaka ukielewe ni kwamba mchukulie daktari kama fundi makenika ambaye akimaliza kutengeneza gari na kulipiga stata likawaka bila tabu basi fundi huyu huona raha na mara nyingine hujisifu.
Ukweli ni kuwa daktari hupata faraja once anapoona mgonjwa wake hana hatari ya kufa.
Wapo baadhi ya madaktari(quacks) ambao hawaendani na misingi ya udaktari sio hapa tanzania pekee bali ulimwenguni kote,kuna madaktari wanaotumia ujuzi wao kutengeneza biological weapons n.k.
Pamoja na mapungufu haya huwezi kusikia mtu muungwana akisema madaktari wa dunia hii ni wauaji.
Jaribu kuwa makini na kauli zako kuna siku utasema waislamu ni wauaji au wakristu ni wachawi,hapa utaspark vita ya kidini na hutapata muda wa kuexplain.
 
Hapa tayari unaafikiana na mimi kuhusu tukio lenyewe ila ukisema problem ni lugha iliyotumika kwenye heading ya hii habari naweza sema imekuwa kali sana kwenu madaktari. Mlitaka pengine ni specify nipunguze harshness ya lugha. Inawezekana ningetumia lugha tofauti hata wewe usingeoona hii habari kama inakuhusu lakini kwa lugha hii ime- catch your attention na ukaamua kuchangia. Ukweli ni kwamba kitendo alichofanya Dakatari hakikuwa cha kiuaji ila dhamira ya huyo daktari ndiyo ilikuwa ya aondoke akafie mbali kwani he is too close to the grave" . Nikupeni tu taarifa ni kwamba mgonjwa tulimpeleka hospitali nyingine na hadi sasa ameweza kunywa uji bila tatizo huku akiwa na nguvu kubwa tu tayari hata tukimtransfer tunajua atasafiri na kufika salama. Ila tungem transfer wakati ule alipofanyiwa discharge Mt. Meru ingewezekan saa 1 jioni isingefika kwani hata kama angeondoka kwenda KCMC kuna procedures ambazo lazima angepitia including registration n.k na zingesababisha hali yake iwe mbaya zaidi. Tunamshukuru Mungu hakufa kama walivyokuwa wanataka!!
 
Heshima kwako PakaJimmy.

Mkuu uko sawa kabisa.
Nilizungumza na watu wa maabara,X-ray,Medical Records,Drs,baadhi ya wagonjwa wodi namba 6 na Clinic Officers ambao wamefanya kazi kwa karibu sana na Dr Israel.Sikuishia hapo tu bali niliwataka wamfikishie ujumbe Dr Israel awe makini na kazi yake hasa ukizingatia ndio kwanza anaanza safari yake ndefu katika fani ya uDr.Nikiri wapo walioshangaa Dr kupokea na kutekeleza amri ya Nurse wengine waliconclude inatokana na uzoefu mdogo.
Ngongo,
Ulifanya kazi ya heshima kama uliweza kutoa maagizo hayo hapo kwenye 'red"!
Naamini kama anaamini katika Nguvu ya Umma, na kujali viapo vyake, basi atageuza tabia yake ya kusikiliza mashauri ya Nesi badala ya kutumia maadili ya udaktari!
Nakushukuru tena kiongozi!
 
Hapa tayari unaafikiana na mimi kuhusu tukio lenyewe ila ukisema problem ni lugha iliyotumika kwenye heading ya hii habari naweza sema imekuwa kali sana kwenu madaktari. Mlitaka pengine ni specify nipunguze harshness ya lugha. Inawezekana ningetumia lugha tofauti hata wewe usingeoona hii habari kama inakuhusu lakini kwa lugha hii ime- catch your attention na ukaamua kuchangia. Ukweli ni kwamba kitendo alichofanya Dakatari hakikuwa cha kiuaji ila dhamira ya huyo daktari ndiyo ilikuwa ya aondoke akafie mbali kwani he is too close to the grave" . Nikupeni tu taarifa ni kwamba mgonjwa tulimpeleka hospitali nyingine na hadi sasa ameweza kunywa uji bila tatizo huku akiwa na nguvu kubwa tu tayari hata tukimtransfer tunajua atasafiri na kufika salama. Ila tungem transfer wakati ule alipofanyiwa discharge Mt. Meru ingewezekan saa 1 jioni isingefika kwani hata kama angeondoka kwenda KCMC kuna procedures ambazo lazima angepitia including registration n.k na zingesababisha hali yake iwe mbaya zaidi. Tunamshukuru Mungu hakufa kama walivyokuwa wanataka!!

nashukuru kuona hatimaye unanielewa!
Kubali lugha uliyotumia si ya kiungwana ni lugha ambayo hutumiwa na magazeti ya udaku,jitahidi sana kuepuka lugha hiyo kwani itakushushia credibility.naona sasa hata dr.israel unamuondoa kwenye 'tendo' la uuaji na unaanza kusema juu ya 'dhamira' yake ambayo kuithibitisha ni ngumu zaidi.
Naamini mgonjwa wako yuko vizuri kama ulivyosema,akizidiwa usisite kumrudisha mt meru na 'ukihisi' hatendewi vizuri report immidiately kwa incharge wa wodi,incharge wa hospital,RMO,Polisi halafu ndio ulete bandiko hapa!
Wewe ni msomi(naamini hivyo) na approach yako ya kutatua tatizo ni lazima itofautiane na wahuni wa mtaani.
 
Back
Top Bottom