Madaktari wengi ni misukule walio hai

Madaktari wengi ni misukule walio hai

A very constructive discussion though katika lugha ngumu sana. Kama una kisukari/presha ukisoma lugha anazotumia mleta mada na ni daktari utakata moto mapema. Though kwa akina sie tunajifunza no mara waah!!!

Diskasheni iendereeee.....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbe cancer ndo inakua hivi? Sasa kwann wataalamu wasitafute suluhisho la hizo cells kukua hovyo au tofauti na mpangilio unaotakiwa?
Jitihada zimefanyika nyingi ikiwemo Dawa za Chemotherapy na hata Radiotherapy kuua hizo cells maana autoimune na Apoptosis mara nyingi zinakuwa Inhibited kwahyo inabidi External mechanism itumike Kuua hizo cells zilizokwisho kuharibika..
 
ukiumwa uendag hosptal unaenda kwa wich dr? oya pombe so sigara uzi uliandika umekunywa robot za kutosha mayb
 
Nimetumia neno msukule kwa makusudi maalumu. Msukule sio tusi ni nomino, ni jina la mtu aliyetekwa nyara kiroho na kupotezwa kimazingara.

Kwanini madaktari ni misukule? Nitafafanua kwa ufupi na kwa kiwango kinachoeleweka.

Madaktari wengi akili zao zimefungwa minyororo, hawana wazo huru, wala hawana ujuzi huru. Wamebeba furushi la elimu ya kukaririshwa na kumezeshwa kama makinda ya bundi-mwitu.

Nikizungumza daktari, kwa muktadha wa kitanganyika, namaanisha watu wote wanaojiita wataalamu wa sayansi ambao kimsingi wala sio wataalamu, wengi wao wana diploma za D mbili kisha wakaunga unga mpaka Kairuki University au Bugandooh kisha wakavaa makoti meupe wakaanza kujiita madaktari na wanasayansi.

Kiukweli wako mbali sana na sayansi. Hawaijui wala hawaielewi sayansi. Ukimuuliza daktari wa kitanganyika kwanini kansa haina dawa anakwambia kansa haina dawa kwa sababu mabeberu hawajaleta chanjo.

Mfumo mzima wa daktari wa kitanganyika umejengwa katika muhimili wa kukariri na kusubiri maagizo ya mabeberu.

Beberu likiamuru kwamba kansa haina dawa basi ujue daktari wa kitanganyika hapindui meza. Ni mwendo wa kansa haina dawa hadi pale beberu litakapoamua vinginevyo.

Huu ni msukule wa kitanganyika katika mavazi meupe. Akili imefungwa minyororo ya chuma.

Corona ilituaibisha. Wanasayansi wetu wa kitanganyika walijificha uvunguni wakisubiri kuokolewa na mabeberu. Alhamdulillah mabeberu wakatutupia magunia ya chanjo tuyafakamie tupendavyo.

MY TAKE: Madaktari wote wafutiwe leseni zao wakawe wachimbaji wa kawaida wa mitaro ya barabara.

Una pointi, lakini kabla ya kurusha haya malalamiko sina uhakika kama umefanya ufuatiliaji wowote.

Nakubali kutokufanya vyema kwa sekta ya afya, matatizo ni mtambuka.

Mtaalamu wa afya yoyote, hawezi kutumia utaalamu aliougundua pekee. Bali atatumia na waliyoyagundua wenzie na yakapitishwa kitaalamu kwa kukidhi vigezo.
Si kosa kutumia ugunduzi wa sehemu nyingine kwenye kupata suluhusho la tatizo la msingi katika nyanja yoyote.

Kuhusu utafiti wa dawa au vifaa tiba:

1: Hii ni kazi ya msingi ya Taasisi za tafiti. Hata kama wazo likipatikana kwenye utendaji kazi wa mtaalamu wa afya, wazo husika hutakiwa kusajiriwa kwenye tasisi husika na kuendelezwa chini ya usimamizi mahsusi. Kuna ngazi ikifikiwa ndo kilichovumbuliwa huweza kuja kwenye viwango vya hospitali tena na kundelezwa au kutumika.

Ugunduzi wa molecule/s mpaka kupata dawa ni wastani wa miaka 10-18. Hapo ni pesa inafanya kazi. Kwenye pipeline kuna mawazo mengi, na si yote hufanikiwa kulingana na vigezo mbalimbali.

Kama ungefika kwenye hizi taasisi na kukuta hakuna mawazo ya wataalamu basi tungesema hii shida ni ya wataalamu:

1: National Institute of Medical Research(NIMR) na matawi yake pamoja na kitengo cha tiba asili.

2: Ifakara Health Institute(IHI) na matawi yake.

3: Kilimanjaro Clinical Research Institute(KCRI).

Kutaja kwa chache, kuna makabrasha huko watu wanasubiri pesa na kwa kiasi kikubwa toka kule usikotaka kusikia.

Sisi tumeamua kuwaacha viongizi wetu watembee wamekalia shilingi milioni 250,000-400,000/=, wakati wanaitupatia hela za tafiti wanatembea wamekalia milioni 50,000-100,000/=.
Bado tumeandika policy hizi juu ya thamani ya magari ya viongozi wetu.

Kupanga ni kuchagua, soma kipande hiki kinahusu mabepari wenyewe, je kwetu? 👇

Modern drug discovery is thus usually a capital-intensive process that involves large investments by pharmaceutical industry corporations as well as national governments (who provide grants and loan guarantees).

Despite advances in technology and understanding of biological systems, drug discovery is still a lengthy, "expensive, difficult, and inefficient process" with low rate of new therapeutic discovery.[6]

In 2010, the research and development cost of each new molecular entity was about US$1.8 billion.[7]

In the 21st century, basic discovery research is funded primarily by governments and by philanthropic organizations, while late-stage development is funded primarily by pharmaceutical companies or venture capitalists.[8]

To be allowed to come to market, drugs must undergo several successful phases of clinical trials, and pass through a new drug approval process, called the New Drug Application in the United States.
 
Kiongozi;
Naomba nikusahihishe kuwa, hakuna kozI yoyote ya Afya inayopelekea kutibu mtu unayoweza kusoma ukiwa na Chini ya pass 4 zikiwemo Chem, Bio, Phy na Maths (na sio pass mbili kama ulivyo andika)
Lakini pia, Nikutoe wasiwasi kuwa, Nimefuatilia data za miaka ya hivi karibuni waliochaguliwa kusoma kozi hizo ngazi ya Diploma ni wale wanye pass za juu sana (Div ONE) na ninauhakika hakuna mwenye Chini ya Div 3 amechaguliwa kwenye chuo chochote hata huko Private.
Kuhusu magonjwa ya Virusi
Wale waliosoma PCB (Form Six) wanaelewa vizuri kwa nini ni vigumu sana kutengeneza dawa ya Ugonjwa unaosababishwa na Virusi, sidhani kama ni suala la udaktari; pengine ni mtu mwenyewe uliye ongea naye
By the way; Sio kIla anayevaa Koti Jeupe ni Dactari (MD) hata hivyo huwezi kufanya Research kwa kuongea na mtu mmoja au wawili halafu uiite research.....
Mwisho: Nikumegee tu kidogo kuwa, virusi vinatabia nyingi za kuonesha kuwa haviko hai na tabia chache za kuonesha kuwa vipo hai. Hivyo hutegemea kwa asilimia zote Cell ya kiumbe hai ili kuishi; sasa mara nyingi kuua kirusi/kutibu kirusi, inabidi uue cell ili kisipate pa kuishi ambapo ni karibia sawa na kuua kiumbe......matokeo yake mathara yanakuwa makubwa kuliko faida....hivyo tafiti mbalimbali bado zinaendelea.....
Mimi sio Dactari ila nilisoma hayo masomo yakanipa uelewa kiasi....
Tatizo letu sisi Watanzania hatunatafiti zetu wenyewe karibia nyanja zote zakitaalamu tunatumia tu tafiti za wengine labda tunatafiti zetu binafsi kwenye siasa majitaka tu.

Kizazi Cha 40,50,60 na hata Cha miaka ya 70 Cha tz nimeyeyusho tukiwalinganisha na kiza hichohicho Cha Cha Asia(India,China, Singapore n.k).

Mkituhadithia mnasema mlianza harakati zenu za viwanda na tafiti mkiwa na ufanano mkubwa lakini Sasa hivi HAKUNA SHUGHULI yani sisi ndo tunatumia vitu vya Wachina, engineers wakichina na matibabu ya Kihindi. Sisi KIKUBWA tua yamenteini maisha yaende sawa na Dunia inavyoenda ila atuna nyongeza tunayo ongeza katika maisha yetu.

Basi ata tuone kuajaribu na kukosea kwenu katika nyanja hizo za kitafiti hakuna Bali tunawaona katika siasa tu,Sasa hapo mnaacha msingi wa ainagani .Au kuendeleza fikra za kitafiti inahitaji kafara nzito alafu nyie ni walokole hamuwezi kufanya hivyo
 
Umenifurahisha sana ase leo mkuu ingawa siamini hizo mambo za misukule na roho ......ila ulichongelea kimeeleweka sana na ndio ukweli kama wanabisha wabishe tu.

Nawakibisha tunawaacha.
 
Jitihada zimefanyika nyingi ikiwemo Dawa za Chemotherapy na hata Radiotherapy kuua hizo cells maana autoimune na Apoptosis mara nyingi zinakuwa Inhibited kwahyo inabidi External mechanism itumike Kuua hizo cells zilizokwisho kuharibika..
Hapana dokta!

Chemotherapy ni hatari sana.
 
Umewahi kuugua ukatibiwa na daktari kisha ukapona? Tuanzie hapo,maana huenda wewe ni marehemu uliyetunukiwa hicho cheo kwa uzembe wa daktari akiwa anatimiza wajibu wake.
 
Umeongea kiundani, lakini bado mtoa mada kama ana hoja ya msingi, kada ya afya kama kada nyingine tu bado tupo nyuma sana.

Baadhi ya vifo ni uzembe tu, huduma zipo hovyo kabisa, watu wanakatwa miguu lakini mguu huo huo ukienda nje unarudi safi kabisa au hatuna podiatrist.

Anyway yapo mambo mengi sana, nimeyaona kimsingi bado tuko nyuma, hasa decision zinazofanywa na watumishi wa afya.
Chuki hizi,ungepiga kitabu acha kulialia,au ulinyang'anywa demu nn
 
Nimetumia neno msukule kwa makusudi maalumu. Msukule sio tusi ni nomino, ni jina la mtu aliyetekwa nyara kiroho na kupotezwa kimazingara.

Kwanini madaktari ni misukule? Nitafafanua kwa ufupi na kwa kiwango kinachoeleweka.

Madaktari wengi akili zao zimefungwa minyororo, hawana wazo huru, wala hawana ujuzi huru. Wamebeba furushi la elimu ya kukaririshwa na kumezeshwa kama makinda ya bundi-mwitu.

Nikizungumza daktari, kwa muktadha wa kitanganyika, namaanisha watu wote wanaojiita wataalamu wa sayansi ambao kimsingi wala sio wataalamu, wengi wao wana diploma za D mbili kisha wakaunga unga mpaka Kairuki University au Bugandooh kisha wakavaa makoti meupe wakaanza kujiita madaktari na wanasayansi.

Kiukweli wako mbali sana na sayansi. Hawaijui wala hawaielewi sayansi. Ukimuuliza daktari wa kitanganyika kwanini kansa haina dawa anakwambia kansa haina dawa kwa sababu mabeberu hawajaleta chanjo.

Mfumo mzima wa daktari wa kitanganyika umejengwa katika muhimili wa kukariri na kusubiri maagizo ya mabeberu.

Beberu likiamuru kwamba kansa haina dawa basi ujue daktari wa kitanganyika hapindui meza. Ni mwendo wa kansa haina dawa hadi pale beberu litakapoamua vinginevyo.

Huu ni msukule wa kitanganyika katika mavazi meupe. Akili imefungwa minyororo ya chuma.

Corona ilituaibisha. Wanasayansi wetu wa kitanganyika walijificha uvunguni wakisubiri kuokolewa na mabeberu. Alhamdulillah mabeberu wakatutupia magunia ya chanjo tuyafakamie tupendavyo.

MY TAKE: Madaktari wote wafutiwe leseni zao wakawe wachimbaji wa kawaida wa mitaro ya barabara.
Spot on! Nimecheka mpaka daladala nzima wameshituka, "anko madevu umepatwa na nini"?
 
Jitihada zimefanyika nyingi ikiwemo Dawa za Chemotherapy na hata Radiotherapy kuua hizo cells maana autoimune na Apoptosis mara nyingi zinakuwa Inhibited kwahyo inabidi External mechanism itumike Kuua hizo cells zilizokwisho kuharibika..
Sasa mbona wanasema cancer haina tiba, na wee hapa umeeleza hivi? Hebu nieleweshee tafadhari.
 
Sasa mbona wanasema cancer haina tiba, na wee hapa umeeleza hivi? Hebu nieleweshee tafadhari.
Tiba Means cure..Kitu ambacho Advance Cancer haina....

Cancer inaweza kupata Suluhisho la kutibika ikiwa kwenye Early Diagnosis, sana sana in cancer in situ na early first stage...

Magonjwa mengi Hambayo hayana Cure huwa yanatibiwa kwa Paliative care tu...

Na chemotherapy na Radiotherapy ni kwa ajili ya kuzuia Athari ya cancer isiwe kubwa sana
 
Misukile hyo hyo ndo inatibu ndugu zako wakapona na wakaamka vitandani hebu heshima hata kidogo jitihada zao kwenye kusaidia jamii na suala la ugunduzi Hilo hata usilaumu mana wengi wao toka wakiwa mwaka wa kwanza wa udaktari Hadi kuwa maprofesa elimu bado n Ile ile na n mfumo kila mtu ameukuta

Wanatibu kwa kufuata miongozo ya mabeberu,hakuna daktari bongo mwenye dawa yake au anatibu kufuata miongozo yake hayupo,bora hata waganga wakienyeji kuliko hawa misukule ya mabeberu.
 
Mleta mada ameandika vizuri ila kwa kuchanganya mambo, kila kada ina kazi yake na kazi ya daktari sio hiyo uliyotaja. Daktari hahusiki kabisa kwenye uvumbuzi wa dawa wala vifaa tiba, wenzetu ni kweli Mungu kawapa uwezo zaidi yetu ila daktari sio kazi yake kugundua dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani.

Labda ungetupia lawama kwa pharmaceutical scientists, lakini sio daktari.

Madktari wanamchango mkubwa kwenye uvumbuzi wa magonjwa na tiba.
 
Back
Top Bottom